Pre GE2025 CHADEMA mko wapi? CCM wanapita mashuleni na kuandikisha watoto wa shule za msingi na sekondari wote kama wanachama wao kwa mfumo wa kidigitali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
1,996
4,332
CHADEMA na ACT WAZALENDO mko wapi nyie? Msije mkasema hatukuwaambia...

Watoto wangu wawili (kidato cha 1 & 2) wanaosoma shule moja ya kutwa hapa Shinyanga Manispaa wamefika nyumbani jana na kuniambia kuwa CCM walifika shuleni na pikipiki zao za kijani na kumtumia mwalimu mkuu wao awalazimishe waandikishwe kuwa wanachama wa CCM kwa mfumo wa kidigitali...

Nilikasirika sana. Sikuwahi kuipenda CCM maisha yangu yote. Watoto wangu pia sitaki kabisa wajihusishe na uchafu huu hata kwa dakika moja na nitalisimamia hilo kwa kuwaambia ubaya wake. Hii taarifa kwa kweli ilinikera sana. Nitafanya jambo hakika kurekebisha hili.

Wameniambia kuwa, CCM wameweka kambi kwenye shule yao. Na bila shaka zoezi hili linafanyika ktk shule zote za sekondari na msingi Tanzania. Kinachosikitisha ni kuwa hawajali umri. Wanangu umri wao ni kati ya miaka 13 na 14 respectively.

Hili ni kosa kisheria kulazamisha watoto wadogo kuwa wanachama wa chama cha siasa wakiwa chini ya umri wa maamuzi ya hiari kisheria wa miaka 18.

Kitendo hiki kinachofanywa na CCM kwa watoto wetu ni cha kibakaji na kuwanajisi watoto wetu na siasa zao za kitekaji, utesaji na uuaji....

Wazazi tukatae huu ujinga na upumbavu wa CCM wa kulazimishwa wapendwe wakati walishachuja na hawawezi kupendeka tena...

Na kwa sababu hii, tuchukue hatua kali za nguvu ya umma dhidi yao kwa sababu shule hizi ni mali ya jamii ya mahali husika, sio mali ya CCM...

Natoa wito kwa wazazi, waelewe kuwa "these local community schools are the property of the people in their localities " kijiji au mtaa. Ni mali yenu na si mali ya CCM. Wananchi mna haki na mamlaka ya kuhoji kila kitu kinachoendelea ndani ya shule wanazosoma watoto wenu kuhakikisha ustawi na usalama wao....

Hivyo natoa wito kuitishwa kwa vikao/mikutano ya wazazi ktk shule zenu, jadilini kitendo hiki na walimu wakuu walioruhusu watoto wenu kufanyiwa hivi waitwe na watoe maelezo ya kuridhisha na huyo mwalimu mkuu aende CCM kuwafuta watoto wetu bila masharti yoyote au la, CCM wamchukue wakampe kazi nyingine kwenye ofisi zao...


Uanchama wa chama cha siasa hufanywa na watu wazima kuanzia miaka 18. Kwanini CCM mnawabaka watoto wetu kisiasa...???

Hawa wanaofanya kazi hii wanatembea kwa kutumia zile pikipiki za Samia Suluhu Hassan alizohongwa na DP World na wale waarabu wa Oman wanaoitaka Loliondo na Ngorongoro kwa gharama ya kuwafukuza wamasai alizozisema Tundu Lissu zenye lebo ya "SAMIA2026".

Fuatilieni na mtaona. Mkithibitisha, nanyi fanyeni hivyo. Nendeni mashuleni, andikisheni wanachama ili kama ni vurugu basi iwe vurugu tu tuone panapovuja.
 
Bado wanaandamana, ndio strategy yao, wakishtuka matokeo hapa hapa, wanaanza kulia
 
Taarifa zao zote tunazo
hilo sio siri gentleman,

na hata kua na taarifa hizo hakusaidii wala kubadili chochote.

Infact ,
zoezi hilo la kisayansi liko hatua za mwisho kabisa na lilienda sambamba na kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura,

Lakini pia kujiandikisha kwajili ya uchaguzi muhimu sana wa kihistoria wa serikali za mitaa baadae nov.27 2024🐒
 
Badala ya kukata hao wanaofanya unataka na wengine wajiunge kwenye huo upuuzi...

Nishasema na nasema tena huenda politics za Tanzania ndio cancer inayoliangamiza taifa...
 
Sababu hasa za kuichukia CCM ni zipi? Na Je, unadhani wakitawala chama chako chadema mambo hayo yatabadilika?
Mimi sina na sitakuwa mwanachama wa chama cha siasa lkn NINAICHUKIA CCM NA WANA CCM WOTE KWA SABABU HICHO CHAMA NA WANA CHAMA WAO NDIO MAADUI WAKUBWA NA NAMBARI MOJA WA TANGANYIKA NA MAENDELEO YA TANGANYIKA.
 
Back
Top Bottom