Kama hali ni Hii Arumeru CCM basi

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Wana JF jana katika kumnadi mgombea wa CCM (Siyoi)Sumari katika kata ya Maji ya Chai,muda mwingi Meneja Kampeni Mwigulu Mchemba alikuwa akijitetea Shutuma zake ndani ya JF,nakusema anamchukia sana SLAA huku akisema Nassari hana NGO ila anamlisha mbwa wa Mzungu..
MY TAKE:kama hizo ndo hoja za CCM basi tunaongozwa na watu Hatari sana vichwani
 
Hicho ni chama legelege na dhaifu CCM,hakiaminiki tena machoni mwa watanzania.
 
yaani wewe ndounajua nilegelege sasa ivi wakati tangu kianze kuitwa ccm ndokilianzia apo ulege lege.
 
Huyu Mwigulu Nchemba si ndie mwizi wa wake za watu huyu? Kichwani mwake anawaza uzinzi tu, hana lolote. Mashavu yake!
 
Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)
 
Huyu Mwigulu Nchemba si ndie mwizi wa wake za watu huyu? Kichwani mwake anawaza uzinzi tu, hana lolote. Mashavu yake!

Kwa hiyo tumwambieje siyoyi amweke mywaif wake mbali na mwiguluuu! Hakiyanani mmasai atampa poloniam dozi dabo ya ile ya mwakyemb
 
CCm itaendelea kuwa juu tu. Tanzania hakuna chama cha siasa hata kimoja vyote ni vyama vya harakati na kutangaza harakati badala ya sera. CCM oyeeeeeeeeeee!
 
Ni kweli ccm ni chama kubwa kwa kuwa na viongozi wengi wenye skendo za kifisadi na mafisadi. Hakuna chama kingine kikubwa kilicho watenda watanzania kama ccm.
 
ndugu yangu wakuti usitoe hoja kama hujui unacho waza,ujenge hoja nasio ushabiki usio kuwa na Tija,huu wakati si wakushabikia kama simba na yanga,hoja ya msingi ni kwamba CCM kama chama tawala kinatupeleka wapi?ifike mahali tusiwe shabiki wa vyama tu huu ni ujinga na ni ubwanyenye,tuangalie kuwa serikali iliyopo madarakani inawasaidieje wananchi,ukweli ni kwamba serikali yetu inatupeleka kuzimu na kama tuko ndani ya boti basi hilo boti lina zama, tajiri kalala mafisadi wameamka,watu tunaishi maisha yasiyo eleweka kama kesha kutakucha,ifike mahali tuoneane huruma jamani!hv wee tajiri utalala mpaka lini maisha ya wanachi wako ni magumu kila kona hv wewe unafurahia kweli unako tupeleka,mm sio shabiki wa vyama lakini napata taabu is some thing paradox my life style.nafikiri watanzania tumelishwa libwata kali sana. basi Mh tumwachie Mungu,wasije wakanipeleka india
 
Usichanganye mpira na siasa !!!
Usifikirie tumbo lako leo, fikiria wanao na wajukuu wako, fikiria miaka 50 mbele, kwa kuangalia miaka 50 nyuma.

Heri ya mwigulu nchemba kuliko SLAA ambaye alinogewa na mke wa mtu akaamua kutangaza uchumba wa milele..cdm hawaoni madhambi yao pia hawataki kukosolewa. BADO NATAKA JIBU KWA NINI DAVID CAMERON ALIINGIA UBIA NA CDM?
 
SISI tumeshaohakikisha kuwa Ni KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI, NI NGUMU KABISA FIKRA ZA MWENYEKITI ( ZA KUVUA GAMBA)
Ni ngumu siasa ya sasa ya Unyama na Kujitegea,
Ni ngumu hata siasa ya Kunyamaa na kujimegea.
 
...ni mazuzu wachache sana walobaki CCM,wenye akili washajiunga na wana-ukombozi wa taifa. PEOPLE's...........!!!
 
Heri ya mwigulu nchemba kuliko SLAA ambaye alinogewa na mke wa mtu akaamua kutangaza uchumba wa milele..cdm hawaoni madhambi yao pia hawataki kukosolewa. BADO NATAKA JIBU KWA NINI DAVID CAMERON ALIINGIA UBIA NA CDM?

kwasababu alishamaliza kuwashikisha ukuta wote wa ccm ndo akataka kuanza na cdm ikashindika
 
Back
Top Bottom