Ni kama asemavyo KITILA MKUMBO, tufanye vita na ulaghai wa kisiasa.

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
Katika hoja zake Profesa Kitila Mkumbo, mwanachama mwenzangu wa kale wa Chadema amewahi kuandika "Kumuenzi Mwalimu Nyerere: Tufanye vita dhidi ya ulaghai wa kisiasa" na katika hoja yake hiyo Prof Kitila anaandika;
Pengine ulaghai mkubwa kabisa wa kisiasa kuwahi kutokea hapa nchini ni ule uliofanywa na chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kwa kushirikiana na washirika wake katika vyama vinavyounda Ukawa
Baada ya kumnyanyasa, kwa miaka mingi, kwa kila aina ya kejeli na matusi, na kufanikiwa kuiaminisha jamii kwamba Edward Lowassa ndiye alikuwa taswira halisi ya ufisadi nchini, wakaibuka naye kuwa mgombea katika mchakato ambao wataalamu wa sayansi ya siasa watahitaji kuufanyia utafiti maalumu

Katika kumalizia andiko lake baada ya aya kadhaa Profesa Kitila Mkumbo anaendelea kuandika akisema;
Katika kitabu chake Mwalimu Nyerere anaita tabia hii katika uongozi kuwa ni unafiki. Kwamba kosa ni kosa likifanywa na mtu mwingine, lakini kosa hilo hilo linakuwa si kosa likifanywa na wewe au likifanywa na jamaa yako!

Binafsi nimevutiwa na maandiko haya ya Profesa huyu mchanga, maandiko yake haya bila shaka yametokana na ukweli kuwa si tu ni mtu mwenye taaluma kubwa na ueledi mpana kwenye masuala ya siasa za nchi hii bali ameyaishi maisha yaliyoguswa na ULAGHAI mkubwa uliopo katika vyama vya upinzani nchini.

Nadhani mimi nitaongeza jambo kuhusu ulaghai unaopaswa kupigwa vita ili kuimarisha demokrasia ya kweli nchini.

Ulaghai mwingine wa hovyo sana ni kule kujaribu kuwaaminisha watu kuwa upinzani wa kweli ni wa CHADEMA pekee na kwamba chama kingine chochote cha upinzani ambacho hakikubaliani na chadema hao ni CCM B na kwamba wanatumika na CCM. Iliwahi kuwa hivi kwa CUF pale Mheshimiwa TUNDU aliposimama na hoja yake maarufu bungeni "HAKUNA NDOA YA WANAUME WENGI" akiwatuhumu CUF kuwa wameolewa na CCM na kwamba ndoa yao hiyo inawaweka mbali na CHADEMA na kwamba chadema haiko tayari kushirikiana chochote na CUF katika kuunda Kambi ya Upinzani Bungeni wakati huo. Ni kama vile leo ACT wazalendo wanavyozamishwa kwenye bahari hiyo ya U-CCM B kwa fikra, hila na ulaghai ule ule wa miaka 5 iliyopita.

Wakati mwingine nashawishika kuwa UCHAWI UPO na una nguvu kubwa sana katika siasa za nchi yetu. Maana kama si upungufu wa akili basi ni nguvu ya giza pekee ambayo inaweza kumfanya mtu kama TUNDU kusimama jukwaani kumnadi EDWARD LOWASSA kuwa ni mtu safi, hakuwahi kula rushwa na mwenye maamuzi ya kuwaletea mabadiliko watanzania....LOWASSA..eti Lowassa ni mwanamabadiliko anayesemewa na LISSU, MNYIKA, MDEE etc.

Katika Video Clip maarufu Mwenyekiti wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe anasikika akiapa kwa Mungu wake akisema "LOWASSA CHADEMA, yaani lowassa ajiunge na Chadema, OVER MY DEAD BODY"' lakini leo Lowassa sio tu ni mwanachama wa CHADEMA bali ndio KAULI KUU ya chadema, ndio mfanya tathimini na ndio mwenye maamuzi. Tusipopiga vita Ulaghai huu na UNAFIKI wa kiwango hiki, Taifa hili litaangamia.

Kimsingi nimekata tamaa na Vijana wa BAVICHA na supporters wa Chama hiki ambao watu wengine wanawaita majina mabaya ya wanyama fulani hivi, maana wao si watu wenye kuhoji na kutafakari, wanachoambiwa na wakubwa zao wao wanakibeba na kukinadi. Siku nikijiunga na CHADEMA hii (MUNGU wangu aepushie mbali) mtaona maajabu, maana Thread ya Kwanza hapa JF italetwa na John Heche yenye kichwa cha habari "JULIANA, MWAMBA USIOYUMBA" na wale waliokuwa wakikesha kuandika matusi hapa watakuwa wakwanza kuandika kwa mbwembwe za kunisifia...kama wamelogwa hivi.

TUACHE UNAFIKI WA NAMNA HII.
 
Naunga mkono hoja.
Pasco
 
siasa ni mchezo wa "KINAFIKI" hasa siasa hizi za nchi za kiafrika...mwandishi wa uzi huu ni mmoja wapo wa hao "WANASIASA WANAFIKI" so the rules of the game are clearly derived from the hypocrisy.

sorry juliana...nawe ni kati ya hao "wanafiki".....kaa tafakari na utaniambia ulipo, ulikotoka na ulipokuwa kabla ya ulipotoka.....huo ndio unafiki halisi na katika rangi zake zote.
 
Yale Yale. ..anashambuliwa mtoa mada.
 
Yale Yale. ..anashambuliwa mtoa mada.

naomba nieleweke...sijamshambulia mtoa mada...."NIMEMKUMBUSHA AWE NA AKIBA YA MANENO MAANA NAYE ANAFANYA SIHASA HIZOHIZO ANAZOWALALAMIKIA AU KUWAKEJELI WENZAKE...." namuona kama anatukana WAKUNGA NA UZAZI UNGALIKO...shonza namuona kama ANATUKANA MAMBA ILIHALI HAJAFUKA HUO MTO ULIOJAA MAMBO...akiba ya maneno na hekima ya wapi ayatumie ni kitu muhimu kwa mwanasiasa makini kuwa nacho.

CHUO CHA DIPLOMASIA NA SIASA KINAWAHUSU SANA WANASIASA WA KIZAZI HIKI....sikumbuki na wala sijawahi kusikia mzee lowassa akitukana nyumba iliyomkuza...pamoja na yote yale tunayoyajua...pia hata mzee kingunge sijawahi kumsikia.
TUJIULIZE TUU...JE NI KWELI HAWANA CHOCHOTE CHA KUUTUKANA AU HATA KUUKASHIFU UPANDE WALIOTOKA?.....shonza na kitila wote wametoka huko wanakoku-kashifu lakini wanasahau kuwa ipo kesho na keshokutwa upepo unaweza kubadilika na wakajikuta wamerudi kulekule walikokuwa wakipakashifu.

HITIMISHO:- AKIBA YA MANENO IWEKWE NA SIO AKIBA YA CHAKULA TUU....
 
kati ya vitu vinavyowafanya chadema wasiaminike Kwenye jamii ni kitendo chao cha kumtukana Mzee wa watu kwa miaka nane zeni Leo hii ndo top layer wao aisee
 
siasa ni mchezo wa "KINAFIKI" hasa siasa hizi za nchi za kiafrika...mwandishi wa uzi huu ni mmoja wapo wa hao "WANASIASA WANAFIKI" so the rules of the game are clearly derived from the hypocrisy.

sorry juliana...nawe ni kati ya hao "wanafiki".....kaa tafakari na utaniambia ulipo, ulikotoka na ulipokuwa kabla ya ulipotoka.....huo ndio unafiki halisi na katika rangi zake zote.
Unapomtuhumu mtu kwa unafiki bila kusema kwa jambo gani alilisema ama kulifanya ambalo kwalo unamtuhumu kwa unafiki kimsingi kauli inakurudia kuwa wewe msemaji ndio MNAFIKI.

Niliposema kuwa CHADEMA kwa maana ya Viongozi wake wakuu ni walaghai na wanafiki nilileta na maelezo ya unafiki wao, nikaenda mbali zaidi nikatoa na quotes za maneno yao ambayo leo yamedhihirisha unafiki wao kwa namna walivyoyakana na kuyakanyaga.

Hivyo ndugu yangu, nikiwa natanguliza ustaarabu mbele naomba unitajie jambo ama neno moja tu, na ni moja tu ambalo nimelifanya ama kulisema ambalo kwa neno hilo ama jambo hilo unanituhumu kwa UNAFIKI..??? Otherwise utanilazimisha nikupuuze, nikudharau na kibaya zaidi nikujumuishe katika lile jina la kuudhi wanaloitwa baadhi ya wafuasi wa CHADEMA.
 
Kuna mwingine aliwahi kusema tusiwaamini wanasiasa....naweza kumuunga mkono pia!

upload_2016-10-27_14-39-3.jpeg

Wengine wanaita miujiza tu na sio ulaghali wa kisiasa!

Kijana tena mdada unamawazo ya Hovyo kama mzee....ni lini utajadili maendelea, kutwa kujadili watu na matukio tu....
 
Ulijiunga lini chadema, zama za mafuriko au..???

sikuwahi na sitawahi kuwa na chama chochote cha siasa hadharani, nilikusikia sana ulipokuwa chadema na pia ulipoingia ccm, kwa msingi huo nadhani unauelewa mpana kuhusu mambo ya kisiasa hapa nchini

swali sasa unafiki tuweke pembeni, chama kipi kiko moyoni mwako Mdada, na pia kuna balance yoyote ya kisiasa nchini?
 
naomba nieleweke...sijamshambulia mtoa mada...."NIMEMKUMBUSHA AWE NA AKIBA YA MANENO MAANA NAYE ANAFANYA SIHASA HIZOHIZO ANAZOWALALAMIKIA AU KUWAKEJELI WENZAKE...." namuona kama anatukana WAKUNGA NA UZAZI UNGALIKO...shonza namuona kama ANATUKANA MAMBA ILIHALI HAJAFUKA HUO MTO ULIOJAA MAMBO...akiba ya maneno na hekima ya wapi ayatumie ni kitu muhimu kwa mwanasiasa makini kuwa nacho.

CHUO CHA DIPLOMASIA NA SIASA KINAWAHUSU SANA WANASIASA WA KIZAZI HIKI....sikumbuki na wala sijawahi kusikia mzee lowassa akitukana nyumba iliyomkuza...pamoja na yote yale tunayoyajua...pia hata mzee kingunge sijawahi kumsikia.
TUJIULIZE TUU...JE NI KWELI HAWANA CHOCHOTE CHA KUUTUKANA AU HATA KUUKASHIFU UPANDE WALIOTOKA?.....shonza na kitila wote wametoka huko wanakoku-kashifu lakini wanasahau kuwa ipo kesho na keshokutwa upepo unaweza kubadilika na wakajikuta wamerudi kulekule walikokuwa wakipakashifu.

HITIMISHO:- AKIBA YA MANENO IWEKWE NA SIO AKIBA YA CHAKULA TUU....
Nasikitika sana pale ambapo naandika kitu halafu anatokea mtu ambaye anashindwa kabisa kuelewa nilichokiandika. Kwanza sio kweli kwamba nimewakejeli viongozi wa CHADEMA bali nimeelezea uhalisia wa matendo na matendo yao...kuwa sio watu wa kuaminika, wanaweza kusema A na watu wakaamini A na baadae kugeuka na kutaka kuifanya iwe B.

Kuniambia kuwa natukana wakunga kabla sijavuka mtu ni maneno ya jumla sana, ingependeza ukanieleza ni upi mto huo na huyo mamba akawekwa wazi, unless otherwise tutakuwa tumejiingiza kwenye majungu.

Kimsingi ninachokisema kuhusu viongozi wa chadema sio kukashifu kama unavyodai, ama kwa Lowassa kutoisema CCM hilo halishangazi, unataka aiseme kwa lipi..? Kuna baya gani la CCM ambapo Lowassa anaweza kulisema, ila CCM inamsema Lowassa kwa sababu wanayo mabaya ya kuyasema na kuyakemea.

Ukitaka hili nalo tulifanye AKIBA basi waswahili walishatutangulia na maneno yao, MFICHA MARADHI, KIFO UMUUMBUA.
 
Anatutoa kwenye mstari huyu...Watu wanawaza maendeleo yy anaendelea na siasa zake za mtaroni.

Badala ya kumpigia kura Mwenyekiti wake ashinde hyo tuzo,yy ndo kwaaanzaa yupo busy na chadema

Si ulishaondoka huku lkn...!!! Tuache sisi wanafki tuendelee na unafiki wetu.

Ninyi watiifu endeleeni kuchangisha pesa ya maafa Kagera.
 
Back
Top Bottom