Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 12,993
- 38,353
nawatakia wakati mwema.
zamani kidogo niliwahi kuwa na mahusiano rasmi na binti mmoja kwa muda wa miaka minne.
alikuwa mwanamke wangu wa kwanza toka kwenye mahusiano.
tuliishi kwa ugumu sana,tulianza kulala chini, kula kwa shida sana ilifika wakati mpaka namwachia 500 kama hela ya kununua mahitaji.
alivumilia tulivumiliana na tulipendana sana.
ingawa ndugu zake na ndugu zangu walikuwa hawapatani kabisa na maombi yao kwa Mungu tuachane.
pamoja na changamoto kubwa za maisha ,umaskini ,kipato kidogo, maradhi, kukataliwa nk, lakini tuliishi kwa upendo ambao kila alietuona alisema hawa wamependana na wanaendana.
maombi ya ndugu yalianza kufanikiwa, tuliachana kizembe sana, alikutana na mr mmoja wakakubaliana aniache aende kwake na ikawa hivyo. aliniachia maumivu sio madogo na nyuzi zinazomhusu zipo hapa jukwaani kibao. ninachoshukuru Mungu wana jamii forum ni zaidi ya ndugu kwa kweli maana ushauri ule walionipa uliniwezesha leo kua na furaha na amaini.
siku zilienda sana sikuwahi kuwa na taarifa nae wala mawasiliano nae.
nikajaliwa kuoa nikajaliwa mtoto, maisha yakaenda vizuri sana.
lakini ukweli yule binti hakuwahi kunitoka moyoni, ndoto za kumuota zikichelewa sana miezi miwili.
nikawa napotezea tuu.
kama mwezi hivi katika kupitapita facebook nikakutana nae, nikamuomba urafiki akabubali, nikamtumia sms ya kumsalimu akajibu. leo nikachukua namba yake fb nikampiga sim ikapokelewa na hakupata shida kujua anaongea na nani, nimeshangaa sana baada ya miaka nane bado anaikumbuka sauti yangu.
tumeongea mengi sana sana lakini kwa kumsikiliza anajutia kuniacha naameniomba msamaha sana. nimemtakia mema na naendelea kumtakia mena na kumuombea.
ingawa nikimkumbuka roho inauma mno haswa leo nilvyosikia suti yake tena kadhalika nae pia. kwa kua yeye ni mke wa mtu kadhalika mimi ni mme wa mtu namba yake nimefuta na kule fb nimemu unfriend yaani total nimepoteza mawasiliano nae ila nimefajika sana kuongea nae.
ombi langu kwenu ndugu zangu kama umeona una upendo wa kweli na mwenzako na yeye hivyo hivyo nawaombeni sana msije kujaribu kuachana maana kuna maumivu yasiofutika kwa wepesi. kama hakua sababu ya kuachana kamwe msiachane.