Hizi ndizo sababu za kuwapenda sana watu wasiopendeka

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Kuna watu huwa wanapitia maumivu makali sana katika ndoa zao na hawana ujasiri wa kuondoka wengine hupigwa mpaka kuvunjwa miguu au kulazwa lakini hawawezi kujiondoa.

Leo utajua chanzo na utajua kwanini haiwezekani mtu kujiondoa katika mahusiano hayo kirahisi tabia ya kupenda sana kupita kiasi huwa kwa watu wenye sifa zifuatazo:

Hawawezi kukaa katika upweke, anakuwa na hasira sana ambazo hawezi kujizuia, anakuwa na wivu kupita kiasi

Huwa hana furaha muda wote, hutumia pesa nyingi sana kumfurahisha mwenza wake bila kujali kesho yake

Hawana mahusiano mazuri na watu wengine,huwa wanapitia maumivu mara kwa mara kama vile maumivu ya kichwa, mgongo, kuugua mara kwa mara

Huwa wanaweza kumpenda sana mwenza ndani ya dakika chache anakuwa na hasira, chuki, wivu, kuchanganyikiwa, uchungu na kupata fikra za kumdhuru mwenza wake

Huwa wagumu sana kusamehe makosa ya mwenza wake, huwa wanajihisi kusalitiwa muda wote, hupenda kupekua simu, anatuma sms na kupiga simu kila wakati hasa akiona upweke unampa maumivu

Huwa sio muelewa hata kidogo, akiona mwenza wake amechelewa kurudi huwa anafikiria mwenza wake hampendi,amekwenda kusaliti na hata mwenza wake akitoa maelezo huwa hawezi kuyaamini

Hupenda sana kufanya mapenzi kama njia ya kuonyesha upendo, anaweza kuvunja mahusiano yenye furaha na kwenda kuzaa na mtu ambaye hana upendo wala hajali hisia zake

Akiwa na hasira anaweza kuvunja vitu vya mwenza wake kwa lengo la kukomoa, anaweza kujidhuru au kumdhuru mwenza wake kwa jambo dogo

Anaweza kutumia pesa nyingi sana kununua bidhaa za gharama kwa ajili ya mwenza wake na wakati wa kuachana hupata fikra za kumdhuru mwenza wake au kumuua au kumpa ulemavu wa kudumu

Wengi hutumia pombe,au ulevi wa aina yeyote, kucheza kamari, kuendesha vyombo vya moto kwa kasi sana, hufanya vitu bila kufikiria chochote na hujuta sana baadaye

Chanzo cha kupenda watu wasiopendeka ni nini?

1. UMETOKEA FAMILIA YENYE UGOMVI KILA SIKU

Wanawake na wanaume ambao wamezaliwa familia zenye vurugu, ugomvi, mapigano, lawama, migogoro ya kifamilia kila siku huwa wanapata tatizo hili la kupenda sana kupita kiasi

Wengi hutoka familia zenye unywaji sana wa pombe, mapigano ya wazazi kila siku, mzazi kuwa na uraibu wa pombe, madawa, kutumia sana pesa, kucheza kamari, kuendesha vyombo vya moto kwa kasi sana.

Familia zenye matukio kama mzazi kumuingilia kimwili mtoto wake,mtoto kuingiliwa na ndugu zake kisha kesi inamalizwa kimyakimya, talaka au migogoro ya kila siku baina ya wazazi

Mtoto ambaye anakuwa huku anaona ugomvi wa baba na mama kila siku huanza kuwa muoga wa watu wenye hasira hivyo hujitahidi kumfurahisha kila mwenye hasira ili kupata upendo wake

Wao hujichukia sana na kujiona hawana thamani mpaka wajitoe kwa watu wenye hasira, maumivu, watu wa mabavu na vurugu

Kuzaliwa familia ambayo mzazi mmoja ni mgonjwa sana na wao kulazimika kufanya kazi ya kumuuguza kwa muda mrefu, kukaa bila kumuona mzazi au wazazi tangu utotoni

Mzazi kuacha kuonyesha hisia za mapenzi kwa mtoto labda kwa sababu ya hasira, ugonjwa, kusafiri sana au mzazi akiombwa pesa za matumizi huanza kutoa maneno makali kwa hasira na kumpa mtoto vitisho

Familia ambazo wazazi huwakataza watoto kutaja maovu ya wazazi au kutaka mazungumzo kuhusu kutoweka amani ndani wengi huwa wenye kupenda kupita kiasi

Familia ambazo huwa wenye desturi za kuficha siri nzito zenye maumivu husababisha watoto wenye wivu kupita kiasi

Kumpata mzazi mwenye wivu sana, kupata mzazi ambaye anakugombeza sana nyumbani halafu akiona wageni anakuwa anakusifia ila wageni wakiondoka unapata maumivu makali sana, kwenye sherehe anakuja kupiga picha na kukupa zawadi ila ukiwa nae nyumbani ni maumivu kila siku.

Familia ambazo kuna sheria kali sana, yaani mzazi hana masihara huzalisha watoto wenye wivu kupita kiasi

2. KUANZA MAJUKUMU UKIWA BADO MDOGO SANA

Kama ulipata malezi ya mzazi mmoja au ulikuwa unafanya kazi ya kuuguza mzazi au mlezi wako tangu ukiwa na umri mdogo sana hivi sasa unavutiwa na mwanaume au mwanamke ambaye anapitia maumivu makali sana na huwa unajitoa sana kwake ukitaka kumuonyesha upendo ili akupende

Wanawake ambao walianza kulea ndugu zao au kuuguza wagonjwa wao wakiwa wadogo sana au kumhudumia mzazi ambaye alikuwa mlevi sana hujikuta wanavutiwa na wanaume wasiokuwa na kazi, hawana juhudi za kutafuta fedha, wenye hasira sana, wasiokuwa na huruma, wasiojali mke wala mtoto, wanaume wagonjwa sana huwa wanakuja haraka na kupata nafasi katika mioyo ya wanawake ambao wametoka familia zenye MAUMIVU ikiwemo tabia ya ulevi wa wazazi au mzazi kuwa mgonjwa sana wakati wa utoto

Wanawake wenye kutokea familia zenye maumivu sana huwa wanajikuta wanataka kuonyesha huruma na upendo kwa wanaume ambao hupenda kamari, ulevi, wasaliti sana, ambao hawana mawazo ya maisha yao,wanaume wasiojali familia zao

Kila mwanamke akitaka kuachana na mwanaume wa aina hiyo huruma huwa inazidi na kuona mwanaume huyo anastahili kuonewa huruma hivyo wao huishi kwa miaka wakiomba na kusubiri mwanaume kubadilika lakini huishia kuumia sana

3. WALITAKA KUMFURAHISHA MZAZI BILA MAFANIKIO

Kama mzazi wako alikuwa haonyeshi upendo kwako na ukifanya kazi ya kumfurahisha kila siku kwa kufanya vile anavyotaka bila mafanikio hivi sasa unafanya kazi ya kumfurahisha mwenza wako lakini unaishia tu kuumia

Upo unaomba na kutafuta ushauri wa jinsi ya kumsaidia huyo mwenza wako ambaye hakupendi wala hakujali

Vilevile huna hisia zozote kwa wanawake au wanaume wenye kujali, kuheshimu na kuthamini hisia zako bali unapenda wenye hasira sana

Unatumia nguvu,pesa,kumpa mahitaji,kumpa zawadi kwa lengo la kutaka kubadilisha tabia yake awe vile unataka lakini mwenza wako hana ushirikiano kwako hivyo umechanganyikiwa

4. UPO NA HOFU YA KUACHWA

Kwa sababu wazazi wako walikuwa wanakuacha bila kujali unalia kiasi gani ulipokuwa mdogo hivi sasa unaogopa kuachwa

Unajitoa kwa nguvu zote kuokoa mahusiano ambayo hayana dira wala maslahi lakini unajipa moyo kuwa ipo siku mwenza wako atakuwa tofauti lakini haiwezekani

Unaona chochote mwenza wako akisema umpe unaona ukimpa atakupenda lakini haonyeshi upendo kwako kila siku unaingia madeni kwa sababu ya huyo mwenza wako

Upo tayari kumpa mshahara wako wote ilimradi unajua ndio atakupenda lakini hatosheki

Upo tayari kuvumilia aachane na mwenza wake wa sasa kisha mtakuja kuishi wote kwa ahadi feki ambayo amekupa

Kwa wanawake wenye tatizo hili anaweza kutoa mahari, kununua nyumba, kununua gari kisha anampa mwanaume lakini huishia kuumia kwa sababu wao hupenda wanaume ambao hawana kazi, hawana huruma, wasiojali hisia zao, wenye historia za kuvunja sheria za nchi

Wao huwa wapo tayari kumtafutia mshauri ili mwenza kubadili tabia, kumpa mtaji, kumjengea, kumpa zawadi, kumfanyia surprize, kumtafutia kazi, kumsomesha lakini yote hayo huwaletea maumivu wao wenyewe Kuvumilia tabia zake mbovu zenye kujirudia, kuvumilia vipigo, usaliti, lugha chafu huku wakiamini atakuja KUBADILIKA

Maisha ya watu wenye kupenda sana huwa yenye mfululizo wa matukio yafuatayo:
  • Kulia sana
  • Kujuta
  • Kupoteza fedha nyingi
  • Kujichukia
  • Kujilaumu
  • Kujilazimisha kufanya kazi
Kusamehe kila siku makosa yenye KUJIRUDIA, kujifungia ndani, kufanya kazi chini ya viwango, kuvunja mahusiano na watu wengine kisa mapenzi thug life
 
Pia kukosa malezi ya wazazi inachangia kwenye hili mkuu unakuta mtoto had anakua hajui na hakuwah kulelewa na wazaz wake zaid hulelewa na ndugu has bibi na wajomba
 
Back
Top Bottom