Kama email yako imekuwa hijacked | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama email yako imekuwa hijacked

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Oct 14, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  KAMA EMAIL YAKO IMEKUWA HIJACKED

  Kuna wale ambao email zao zimevamiwa na maharamia wa mtandao kisha kuanza kutuma emails kwa watu wengine ambao wako ndani ya contacts zao bila idhini ya mhusika mkuu

  Tatizo hili limekuwa kubwa sana kwa siku za karibuni haswa kwa wale wanaotumia email za mtandao wa yahoo au ile ambayo inahusiana na yahoo kwa namna moja au nyingine .

  Endapo utapatwa na sakata hili unachotakiwa kufanya ni kureport suala hili haswa kwa vyombo vya usalama vilivyo karibu yako na pia kuwapa taarifa kwa njia ya mtandao kutumia anuani nyingine watu walio kwenye contact zako pamoja na kutumia njia zingine kama simu ili kuwaataarifu na kama email yako imeunganishwa kwenye group au forum yoyote hakikisha unatoa taarifa pia kwa wanachama wengine ili wajue kuhusu tukio hilo .

  Kuna wengine ambao hujaribu kufungua email hizo kwa kutumia njia mbali mbali mara kadhaa halafu kushitukia email hiyo imefungwa kwa masaa kadhaa na yahoo na ukijaribu zaidi inaweza kufungwa moja kwa moja .

  Ikitokea hivyo hakikisha unasoma maelezo ya kutosha kutoka kwenye mtandao wa yahoo jinsi ya kurecover password yako kama tatizo linahusiana na password ukifuata maelezo hayo unaweza kurudisha email yako kwa mara nyingine .

  Ukiweza kuirudisha hakikisha una ongeza email ya pili ambayo inaweza kutumika pindi tukio hilo likitaka kufanyika tena utapatiwa email kwenye email hiyo , pamoja maswali yako ya siri jaribu kubadilisha mara kwa mara .

  Pia kwa siku za karibuni umeona unatakiwa kuongeza taarifa zaidi kuhusu accont yako ya yahoo na mitandao mengine tafadhali ongeza taarifa hizo lakini udhibitishe ni yahoo ukweli , kwa google kwa mfano wanahuduma ambayo inaweza kukutumia udhibitisho kutumia namba yako ya mkononi .

  Mwisho usipenda kutuma chain emails zile ambazo watu wanaforward kwa watu mbali mbali , maharamia wengi wanatumia njia hiyo pia kwa ajili ya kukusanya emails pia njia hiyo ni rahisi kuvunja baadhi ya masuala binafsi ya mawasiliano kwa mtu kujua watu wako kwenye contact list , usipende kujisajili kwenye huduma za bure na kuacha email zako humo , unapojisajili email yako inaweza kutumika kwa shuguli zingine ambazo wewe hujaridhia .

  Usiku mwema , nimeandika bandiko hili haraka haraka kwahiyo mengine nimeacha njiani au nimeeleza kwa udogo , wengine wanaweza kuendeleza zaidi kwa sababu tumezidiana katika uelewa wa vitu na mambo
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Asante kaka kwa ujumbe huu murua.
   
 3. apakati

  apakati Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imetulia
   
Loading...