Google kufuta email yako

Google kufuta email yako

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,281
Reaction score
2,573
Google kufuta Gmail yako desemba

Google imesema rasmi kuanzia desemba Moja mwaka huu 2023 itaanza kufuta email ambazo haziko active kwa Muda mrefu ikiwa hujaitumia email yako ndani ya Miaka miwili itaondolewa.

Sababu kubwa ya kupunguza akaunti za Gmail

Ikiwa Email haijatumiwa kwenye mawasiliano yoyote Yani kwenye kutuma au kupokea email.

Ikiwa email haijawahi kutumia Google drive kwa Muda mrefu.

ikiwa email haijaunganishwa na YouTube Pia haijatumika kwenye huduma ya soko la play store kwa Muda mrefu.

email yako haitumiki kupakua kitu chochote kwenye soko la play store au app store nk

Ikiwa mtu ameunda email halafu hajatumia kwa Muda mrefu kufanya shughuli yoyote basi email yake itafutwa na Google. Email zote zitakazo futwa wiki mbili kabla hazijaondolewa watapokea taarifa ya kuhamisha vitu vyao muhimu kabla haijafutwa.
 
Tofauti ya GMail na Email ni nini mwenye kujua tafadhari
images.jpeg
 
Back
Top Bottom