PAIY App: application ya kizawa inakusaidia kuzawadia kidigitali

muhogo_kiks

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,294
3,121
Habari zanu wana JF.
Leo naomba niwatambulishe application mpya ya kizawa inakuja kuleta mapinduzi makubwa kwenye mambo ya kupeana zawadi.

Hivi ushawahi kufikiria baada ya kuhangaika kariakoo kununua zawadi kumpa mtu basi utumiea simu yako janja tu kumaliza shughuli hiyo!? Basi PAIY App inafanya hiyo ndoti kuwa halisia.

Kwenye application hii kutakiwa na biashara mbali mbali kama migahawa maarufu, mahoteli, maduka ya nguo, supermarket na kadhalika. Wewe unachofanya ni kupakua Tu app kutoka playstore au apple store. Unajisajili kupitia email yako au namba yako ya simu. Ukishajisajili basi unaweza anza kununua hizo gift vouchers kwa raha zako.

Ukitaka kumzawadia mtu basi unaweka email yake au namba yake ya simu na yeye atapokea notification kwamba amezawadiwa gift vouchers ya sehemu kadhaa na anatakiwa apakue application ili aweze kuitumia.

Mambo ni rahisi kama hivyo tu.

Kwa sasa tupo katika mchakato wa kuifanya iwe inapatikana pia kwenye application ya mpesa ili kama wewe ni mteja wa voda basi huna haja ya kupakua playstore, yani hapo hapo kwenye mpesa app yako unanunua na kuzawadia mtu au pia unapokea gift voucher yako.

Kama wewe unabiashara yako na ungependa tukuwekee gift vouchers zako kwenye application yako Karibu sana. Ni bure kabisa.

Wasiliana kwa email rashid.kikala@4pesa.co.tz

Pia mnaweza kutufatulia kwenye mitandao ya kijamii.

X= @paiyapp_tz
Instagram= paiyapp_tz

Karibuni sana.


IMG-20231031-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom