Kama CHADEMA walitaka watanzania wapate mateso ya Lockdown, hawastahili kupata hata kura moja

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Watanzania tar 28 mwezi huu ndio siku ya kufanya maamuzi ya msingi,lakini pia ndio siku ya kuadhibu wanasiasa ambao wanaojali matumbo yao tu,sio wananchi.

Fikiria muuza kahawa,mama ntilie,machinga fundi ujenzi au fundi Carpentry umfungie ndani kwa miezi minne bila kufanya shughuli,maisha yake yatakuwa vipi?

Fikiria mama muuza karanga,muuza mihogo kwenye beseni na muuza maji ya kandoro umfungie miezi minne bila kufanya kazi maisha yake yatakuwaje?

Chadema walisimama kidedea watanzania tufungiwe ndani tusitoke nje kama njia ya kupambana na Coronavirus na ilifikia hatua wabunge wao walivuta posho na kwenda kuzitanua huku wakidanganya watu wapo lockdown.

Hiki chama hakikuwa na nia njema na watanzania,sababu waliacha kumtegemea Mungu ili atuepushe na Corona virus,bali walileta siasa mbovu ili watanzania wapate mateso ya Lockdown. Angalia jirani zetu Kenya na Uganda walivyoteseka. Ndivyo hivyo Chadema walitaka tuteseke.

Kwa hiyo sababu walikuwa hawana nia njema na watanzania wanyonge,basi adhabu yao ni moja tu. Hakuna kukipa hiki chama hata kura moja.

Hapa wakitoka nje huku tayari wamevuta posho za kujikimu,je wanafaa?
2400394_IMG_20200515_154853.jpg
 
Yani wewe matope kweli. Kwahiyo yule aliyeenda kujificha Chato kwa wiki sita huku wabunge wa chama chake wakiteketea Dodoma ndiye mwenye upendo? Shukuru Mungu hukufa maana wala hakuna ambaye angekujali. Kama wabunge wa chama chake walikufa na bado anaona ni sawa na wewe unashabikia basi umejaa matope!
 
Yani wewe matope kweli. Kwahiyo yule aliyeenda kujificha Chato kwa wiki sita huku wabunge wa chama chake wakiteketea Dodoma ndiye mwenye upendo? Shukuru Mungu hukufa maana wala hakuna ambaye angekujali. Kama wabunge wa chama chake walikufa na bado anaona ni sawa na wewe unashabikia basi umejaa matope!
Hakujificha,bali alikuwa anafanya kazi akiwa Chato. Kuna waziri aliapishwa akiwa Chato.
 
Meko wako hana uwezo wa kushinda kwa kura kwa halali. Muulize kwanini anaogopa tume huru ya uchaguzi kama ana uwezo wa kushinda kwa kura halali?. Kwanini anaengua wapinzani?.

Kwanini kwenye mikutano yake anatumia wasanii,kusomba watu, kufunga mashule ili ajaze uwanja?. Why?
 
Jpm mwenyewe kipindi cha korona alikula kona kwenda chato akaiacha ikulu, kura safari hii kwa lissu, ccm wameongoza miaka 60, sasa basi tuwape na wengine
 
Waliyouawa Ukerewe, Tunduma, Songwe na waliokatwa mapanga Pemba tayari watu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani, na uchunguzi unaendelea. Je lile la Dodoma 7/9/2017 lilifanywa na nani na uchunguzi ukoje ?!.
Police case,jinai haina mwisho pia.
 
Back
Top Bottom