Kama CHADEMA ni Saccos basi CCM ni kioski

Kama CHADEMA ni Saccos basi CCM ni kioski

mafutamingi

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
2,775
Reaction score
2,198
Kwa muda mrefu katika ukumbi huu CHADEMA imekuwa ikiitwa (reffered to) kama saccos. Wanaoiita CHADEMA saccos nadhami wana maana kwamba chama kinaendeshwa kwa matakwa ya watu wachache tofauti na matakwa ya Wanachama kwa ujumla.

Kwa mtazamao wangu kama ni hivyo basi CCM ni kioski. Kwa nini nasema hivyo? Kioski ni biashara inayomilikiwa na mtu mmoja. Maamuzi yote yanafanywa na mtu mmoja.

Tofauti na saccos ambayo ina katiba, kioski hakina katiba. Tofauti na saccos ambayo ina kanuni kioski haina kanuni. Mwenye kioski akisema mtu yeyote anayetaka kumiliki kioski hii lazima awe na umri chini yangu. Kama tunalingana au amenizidi hawezi kumiliki.

Maskini CCM imefanywa kioski, CCM haina kanuni inayozuia mwanachama wa miaka 65, 67 au 70 asigombee nafasi yoyote. Lakini kwa kuwa mwenye kioski amesema.... basi ndo imetoka hiyo!

Si Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa wala Mkutano Mkuu unaweza kuja na mawazo tofauti ya mwenye kiosi!
 
CCM imedharaulika sana duniani, kitendo hiki walichokifanya kwa kawaida hakitakiwi kufanywa na mwanadamu.
 
CCM sio Chama Cha SiaSa kwa Sasa, Maana Hawafanyi SiaSa Bali ni Umafia tu Kwa Jina la SiaSa. Nyerere kuna Wakati Kwenye Speech zake alipata Kusema ."Kwa ilivyokaa KATIBA ya Tanzania, Ikatokea akaingia Madarakani.... Mtajuta.
 
Wewe hahahah sifa kubwa ya Sacco's Ni kwamba ni chama Cha kuweka na kukopa...Tena sio tu kuweka, Ni kukopa tu...chama watu walikuwa wapeana mikopo ya magari , nyumba biashara za kilimo

Kununua matrekta na marejesho hakuna..hukumbuki mwenyekiti alijikopesha trekta liakaenda kufia ifakara...khaaa...jomba..fuatilia Kama fedha za deni zitarudishwa kwenye chama..na bahati mbaya chama chenyewe kinakufa.hakuna mwenye kudai Wala kudaiwa...hahahaha...we unazungumzia Mambo gani..??
 
Wewe hahahah sifa kubwa ya Sacco's Ni kwamba ni chama Cha kuweka na kukopa...Tena sio tu kuweka, Ni kukopa tu...chama watu walikuwa wapeana mikopo ya magari , nyumba biashara za kilimo.

Kununua matrekta na marejesho hakuna..hukumbuki mwenyekiti alijikopesha trekta liakaenda kufia ifakara...khaaa...jomba..fuatilia Kama fedha za deni zitarudishwa kwenye chama..na bahati mbaya chama chenyewe kinakufa.hakuna mwenye kudai Wala kudaiwa hahahaha we unazungumzia Mambo gani?
 
Huwezi kukopa kama hakuna kuweka. Kwa kuwa kuna watu wanakopa ina maana pia kuna watu wanaweka. Watu wanaoweka hawawezi kuendelea kuweka kama wao hawawezi kukopa. Talk about win-win situation. Mpo wanakioski na mmiliki wenu?
 
Ccm ni Mali binafsi ya mwenyekiti na familia yake thus ubunge wamepewa na tume na sio wamechaguliwa, ubunge ni Mali ya chama ukienda kinyume unatupwa dirishani
 
Back
Top Bottom