Kama CCM inataka kushinda uchaguzi kabla ya kupiga kura, Magufuli ndiyo mtu sahihi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, tumewaona watangaza nia wote na tumewasikia nini wanataraji kukifanya wakipata ridhaa ya kutuongoza Watanzania. Hakika niseme kwa dhati ya moyo wangu kuwa karibu wote waliotangaza nia kwa mbwembwe wamejipalia mkaa kwani wameenda kabisa kinyume na misingi ya chama ambapo wao wamejifanya wakubwa kuliko chama. Pia wengi wao wamo serikalini na chama tawala lakini wamejikuta wakiiponda serikali yao katika mambo ambayo wao ni sehemu ya matatizo.

Binafsi nilikuwa simpi nafasi kabisa John Pombe Magufuli. Si kwa sababu nachukia jina lake la Pombe tu bali ni kwa jinsi alivyo mbali na wafanya maamuzi ndani ya CC, NEC na MM. Kwa ujumla Magufuli yupo mbali sana na politics ndani ya chama. Hali hii inamfanya aonekane kama mtu ambaye hatakuwa na msaada kwa watu ambao wamezoea kujipendekeza ndani ya chama kwa lengo kuwa wanakisaidia kumbe wanataka kupiga deal zao. Hayo tumeyaona kwa Rostam na wengi ambao leo ndio friends of Lowasa.

Kwa nini nasema Magufuli ndio jibu sahihi?

  1. Magufuli hana kashfa kubwa za rushwa na ufisadi ambazo zinaweza kumfanya ashindwe kunadi vema sera ya chama ya kupambana na rushwa na ufisadi. Kwani ni ukweli ulio wazi kwamba ukitaka kupambana na rushwa ipasavyo, wewe mwenyewe unapaswa usiwe sehemu ya wala rushwa au usizungukwe na mchwa ambao wanaweza kuharibu utawala wako. Mengi yanayosemwa kama yale ya uuzwaji wa nyumba za serikali kwa watu wasiohusika na sub standard ya barabara zetu huwezi kumuingiza Magufuli moja kwa moja kwani tumeshuhudia jinsi anavyofukuza makandarasi wabovu kila kukicha
  2. Magufuli hakutangaza nia kabla ya kuchukua fomu. Hali hii imemsaidia kwani angeongea mambo ambayo yangemchanganya yeye na wakati mwingine angeishia kujisifu na kuwachafua wenzake.
  3. Magufuli anatoka kanda ya ziwa ambayo ina wapiga kura wengi sana hapa nchini. Ikiwa Magufuli atateuliwa, kanda ya ziwa watakuwa na imani na chama tawala kwani ni muda mrefu wamekuwa na kilio cha kuwekwa kando inapofika wakati wa kuwapata wagombea ilhali wanaamini kwamba wana majembe mengi yanayoweza kuiongoza vema nchi na chama tawala
  4. Ikiwa Magufuli atateuliwa katika hatua ya tano bora, upo uwezekano wa wagombea wote wa kanda ya ziwa na maeneo mengine kama yamkusini, mashariki na kati kujitoa na kumuunga mkono magufuli hali itakayomsaidia kushinda kwa kishindo kikubwa.
  5. Magufuli amefanya mambo mengi yanayoonekana katika jamii kama vile ujenzi wa nyumba bora na za kisasa pamoja na ujenzi wa barabara. Bahati nzuri ni kwamba barabara hizi zinaonekana kwa macho na wananchi wanazitumia. Kubwa zaidi ni kwamba wananchi wanaona juhudi anazofanya Magufuli kutatuaa changamoto za barabara pale zinapojitokeza. Watu wa mikoa ya kusini hawatamsahau Magufuli jinsi alivyosimamia ujenzi wa kipande korofi kutoka Muhoro hadi Somanga barabara ambayo ndiyo ilikuwa kilio cha muda mrefu. Kwa sasa kwenda Lindi inachukua masaa sita tu tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inachukua siku nzima. Pia tumeona jinsi alivyosimamia kurejesha mawasiliano baada ya narabara kuharibiwa na mvua zilizonyesha Aprili 2014 na hivyo barabara za Morogoro na Bagamoyo kutopitika. Magufuli alikuwa anakesha kuhakikisha barabara zinakamilika ndani ya muda mfupi huku akishirikiana vema na Jeshi la Ulinzi. Ujenzi wa daraja la Kigamboni ni jambo jingine linalomuongezea credit.
  6. Magufuli amejipa muda wa kusoma na kuelewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015 hadi 2020. Amesema baada ya kusoma na kuielewa, atawaita waandishi wa habari na kueleza msomamo wake na wa chama chake. Hilo ni bao jingine ambalo amewapiga washindani wake. Wengi walikuwa wanabwabwaja tu bila kuwa na kitendea kazi. Kumbuka Mgombea Urais anawakilisha chama ambacho huandaa Ilani ambayo ndiyo itatumika kuomba kura kwa wananchi. Waswahili wanasema kuwa mkono mtupu haulambwi.
  7. Wakati anaenda kuchukua fomu, Magufuli kaambatana na watu watatu tu akiwemo mbunge wa Nkenge Assumpter Mshama. Hapa pia kawapiga bao wapinzani wake. Wengine wameenda kwa mbwembwe na kuambatana na watu ambao tashwira zao katika jamii ni mbaya. Huwezi kufuatana na watu kama akina Karamagi, Chenge nk then utegemee kupata ushirikiano kwa wananchi.
  8. Magufuli hajawa na shauku ya kuwa Rais wa Tanzania. Ni wananchi na wapenda maendeleo ndio walioona umuhimu wa Magufuli. Tofauti na hawa wengine ambao wanataka kwenda Ikulu kufilisi rasilimali zetu, kulipa fadhila za maswahiba wao na kulipa visadi.
  9. Magufuli si mkurupukaji. Anafanya mambo kwa mujibu wa sheria za nchi. Sote tumeshuhudia jinsi alivyokwaruzana na viongozi wake wa juu katika kusimamia sheria za nchi. Mnakumbuka lile sakata la jengo la TANESCO pale Ubungo? Mnakumbuka sakata la malori kuzidisha uzito kinyume na sheria?
  10. Magufuli hana makundi. Tofauti na hawa wagombea wengine ambao wana kundi ambalo litataka kuona linafaidi kwa kumsaidia mgombea wao. Magufuli hatafungwa na siasa za makundi na hivyo kumfanya awe huru zaidi katika utendaji wake. Pia Magufuli atasaidia kukomesha siasa za makundi kwani wengi wataanza kuona kuwa kumbe mtu anaweza kuwa Rais wa nchi pasi na kuwa namkundi lolote.

Wadau, huu ni msimamo wangu binafsi na sijafungwa na msimamo wowote. Nipo huru kukosolewa na nipo tayari kupokea changamoto zitakazojitokeza kwenye mjadala huu. Narudia kusema kuwa Magufuli ndiye jibu sahihi. Hao wengine hawana vigezo vinavyotakiwa na wananchi. Mtawapa bure UKAWA hoja za kusema kwa wananchi. Nawahakikishia ikiwa Magufuli atateuliwa na chama kugombea, hawa UKAWA hawatasimamisha kabisa mgombea Urais kwani hawana mtu wa hali kama ya Magufuli
 
Huyo mwizi mkubwa, aeleze ufisadi wa nyumba za serikali, aeleze umma ufisadi ukiopo miundombinu
Hizi hoja zako nilitegemea kuzisikia. Ndo maana nikaweka mwanzo kabisa wa mjadala huu. Haya nieleze mengine
 
magufuli ni jembe, mchapakazi, mwadilifu, mwenye maamuzi na anayeshaurika.
ana record nzuri tangu awe mbunge na waziri wa serikali tangu utawala wa mkapa. ameweza kusimamia vyema wizara zote alizoongoza na bado anaendelea na utendaji makini na wa kutukuka.

Magufuli ameshachukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais. kama ccm kitamteua basi watanzania watapata rais wa kihistoria wa kupita bila kupingwa ndani ya mfumo wa vyama vingi.
 
"Magufuli hana kashfa kubwa ya rushwa" by Lizaboni.

Sawa atapatiwa huyo mwenye kashfa ndogo mkuu.
 
Hata akiingia Magufuli ikulu mfumo wa rushwa ulio asisiwa na ccm hawezi kupambana nao. CCM kinachowanyonga ni kutopata nguvu ya kupambana na ufisadi na makundi. Believe me UKAWA mwaka huu wana nguvu sana
 
Mimi nilimuamini sana huyu ndugu. amenilet down big times alipohusishwa kwenye kashfa za uuzwaji wa nyumba za serikali na hivi karibuni kutolipa wahandisi na hatimaye kwenye suala la mradi wa mabasi yaendayo kasi. Unakumbuka barabara hizi zimemegwa mita nzima kila upande?

fedha hizo zimeenda wapi? nani anahusika na umegaji huo wa fedha za barabara za magari yaendayo kasi? je, budget aliyowasilisha majuzi kule Dodoma si ukweli kuwa anaandika mambo yanayojirudia? si barabara za juu alishasema tangu mwaka jana zingeshaanza kujengwa? si kweli kuwa anaturubuni mpendwa huyu? Ajibu kwa ufasaha maswali haya ili tumwamini upya...nje ya hapo...hamna kitu!

Iwapo huyu bwana akijibu hayo hata mimi nitakuwa nyuma yake.
 
In short huyu jamaa urais hatauweza na tukimpa hataweza kubadili chochote. Business as usually
 
Hizi hoja zako nilitegemea kuzisikia. Ndo maana nikaweka mwanzo kabisa wa mjadala huu. Haya nieleze mengine

Magufuli huyu huyu au kuna mwingine kazaliwa ? Seriously? Huyu huyu wa barabara za lami big g ama acha zarau aisee.
 
Hata akiingia Magufuli ikulu mfumo wa rushwa ulio asisiwa na ccm hawezi kupambana nao. CCM kinachowanyonga ni kutopata nguvu ya kupambana na ufisadi na makundi. Believe me UKAWA mwaka huu wana nguvu sana
Mkuu, huku ni kukata tamaa.
 
Magufuli huyu huyu au kuna mwingine kazaliwa ? Seriously? Huyu huyu wa barabara za lami big g ama acha zarau aisee.
Acha dharau Mkuu. Kwani kama barabara zinajengwa ka big g ni kosa lake? Unaona zile za Strabag zilivyo imara? Tatizo Watanzania tunataka vitu vya bei chee.
 
magufuli ni jembe, mchapakazi, mwadilifu, mwenye maamuzi na anayeshaurika.
ana record nzuri tangu awe mbunge na waziri wa serikali tangu utawala wa mkapa. ameweza kusimamia vyema wizara zote alizoongoza na bado anaendelea na utendaji makini na wa kutukuka.

Magufuli ameshachukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais. kama ccm kitamteua basi watanzania watapata rais wa kihistoria wa kupita bila kupingwa ndani ya mfumo wa vyama vingi.

Kipofu akimwongoza kipofu woote shimoni.
 
Back
Top Bottom