Kama Arushaone hupo DAR, basi duniani wawili wawili…!

Kama Arushaone hupo DAR, basi duniani wawili wawili…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
Leo majira ya mchana nikiwa natokea Gymkhana Club kupitia Ghana Avenue nilikuwa nimefuatana na Rav4 moja ya rangi ya kijivu ikiwa mbele yangu, tulipokatibia makutano ya Ohio tulikutana na jam moja ya magari yanayotaka kuingia hiyo barabara ya Ohio, mara nikamuona binti mmoja mwenye ngozi ya maji ya kunde ambayo haikuharibiwa kwa mikorogo wala caro lite ambaye kwa ukweli ni mzuri kwa sura na umbo. Alikuwa akitembea kwa miguu kuelekea barabara ya Ohio tena kwa mwendo wa madaha utadhani Twiga wa Serengeti. Hakuwa mrefu wala mfupi na unene wa wastani na umbo maridhawa la namba nane. Nilijikuta nikisafisha kiwi cha macho lakini kwa tahadhari kubwa maana nilikuwa nikiendesha.

Hamadi! nikasikia breki za ghafla na kishindo, na nilipotazama mbele yangu niliona ile Rav4 ikiwa imeigonga kwa nyuma gari nyingine aina ya Toyota Harrier hapo kwenye makutano ya Ohio na Ghana avenue. Ilibidi niambae pembeni ya uzio wa Gymkhana ili niwahi ofisini kwa mkoloni wangu. Nilipokaribia hapo ilipotokea hiyo ajali nilimuona jamaa mmoja ambaye amefanana sana na Arushaone akishuka kwenye hiyo Rav4 nilitamani sana kusimama ili nithibitishe kama niko sahihi, lakini nilipopunguza mwendo nilianza kupigiwa honi na watu wenye haraka zao. Hata hivyo nilisikia watu waliokuwa karibu wakati ile ajali ikitokea wakimshutumu huyo jamaa ambaye nimemfananisha sana na Arushaone kwamba alikuwa amemkodolea macho yule binti niliemzungumzia hapo juu hadi akasababisha ajali. Wakati wapambe wakimshutumu huyo jamaa wa Rav4 aliyesababisha ajali ambayo hata hivyo haikuwa kubwa sana, yule binti alikuwa akichanja mbugga kuelekea jengo la Amani Place lililopo barabara ya Ohio huku wanaume wakware wakimpigia miluzi kama kawaida ya vijana wa mjini.

Hata hivyo niliendelea kushuhudia waendesha magari na wapitao kwa miguu wakikata shingo kushuhudia uumbaji wa mwenye enzi Mungu.

Hebu mkuu Arushaone nijuze ndugu yangu, hivi uko Dar ama ni haya mawani yangu yamenilaghai…?

Hebu kina Mr Rocky, PakaJimmy, Filipo, LiverpoolFC, marejesho, Preta, Mungi, Erickb52 naomba mnithibitishie kama jamaa yuko huko Arusha au ni huyu niliyemuona kwenye hili tukio la ajali...

CC: Asprin, Ruttashobolwa, KakaKiiza, amu, Paloma, Babu DC Dark City, Madame B, Smile, Kipipi, Asnam, Kipaji Halisi, cacico, ladyfurahia, Kaunga, sweetlady,
 
Ngoja kwanza nimalizie kufuturu. Afu Mtambuzi hapa DAR naona hata ambao hawakufunga + kobez wote wanafuturu as if nao walikuwa wamefunga, plus me!
 
Last edited by a moderator:
Kaka mkubwa hako kanjia huwa kana kawaida ya kuwa na warembo haswa hapo Amani Place lol...usipokua makini unaweza kuwa msababisha ajali kila leo...
 
Back
Top Bottom