GE2025 Kaliua: Mwenge wa Uhuru wazindua, na kuweka mawe ya msingi miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 2

GE2025 Kaliua: Mwenge wa Uhuru wazindua, na kuweka mawe ya msingi miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 2

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dk. Garald Mongela, amewaongoza maelfu ya wananchi wa wilaya hiyo kushiriki uzinduzi wa miradi ya kimkakati iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Katika mwaka huu Mwenge wa Uhuru umezindua, umeweka mawe ya msingina umetembelea miradi tisa ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi 2,275,516,058.60.

Miradi hiyo ni uzinduzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya

Sekondari Mwongozo, Ujenzi wa Nyumba ya Walimu ya Familia Mbili (Two in One) Shule ya Msingi Dk. Charles Msonde Shilingi 110,000,000 na Ujenzi wa Kitakasa Mikono Shule ya Msingi Dk. Charles Msonde Shilingi 10,205,313.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) Zahanati ya Usigala Shilingi 72,400,000, Ujenzi wa Shule ya Sekondari Makingi

Shilingi 603,890,563 na Mtambo wa Kutengeneza Barabara (Motor Grader) Shilingi 1,227,000,000.

Miradi mingine iliyozinduliwa ni Barabara ya Kuelekea Kituo cha Afya Ulyankulu (km. 2) Shilingi 1,603,040.00, Mradi wa Maji Kijiji cha Ulindwanoni Shilingi 219,817,142.60 na Mradi wa Kikundi cha Bodaboda (Boma Road) Shilingi 30,600,000.
IMG-20250729-WA1183.jpg
IMG-20250729-WA1182.jpg
IMG-20250729-WA1181.jpg
IMG-20250729-WA1180.jpg
Chanzo: Malunde
 
Back
Top Bottom