Kalenda ya Elimu iheshimiwe

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Nadeclare interest.

Mamlaka husika zimetoa Kalenda ya Elimu: siku ya kufungua shule; siku ya kufunga shule; likizo fupi; likizo ndefu; siku za mitihani na kadhalika. Lakini zipo shule zinazopuuza Kalenda ya Elimu hasa inapokuja kwenye suala la likizo fupi na likizo ndefu kwa wanafunzi, hususan walio kwenye madarasa yenye mitihani ya taifa. Shule hizo huwanyima wanafunzi hao haki yao ya kimsingi ya kupumzika likizo na kuondoka kwenye mazingira ya shule kwa kipindi kifupi.

Kwa mtazamo wa wenye shule hizo, kadiri unavyomuweka mwanafunzi shuleni, ndivyo anavyozidi kupata elimu. Wanavyoona, likizo ni kitu kinachorudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi; likizo ni kipengele cha hiari kwenye Kalenda ya Elimu na ambacho wanaweza kukivuruga wapendavyo.

Jambo hili si la kuachiwa tu hivihivi. Kama ambavyo shule za umma na za binafsi zinalazimishwa kufuata tarehe za kufungua shule, na kuzingatia urefu wa mihula, basi pia mamlaka izilazimishe shule za umma na za binafsi kuheshimu haki ya wanafunzi kwenda likizo.

Katika kitabu cha Kufikirika, mwandishi Shaaban Robert, alimtumia mhusika Utubusara Ujingahasara kufikisha ujumbe wa haki, umuhimu na ulazima wa likizo kwa wanafunzi kwani afya na hata uhai wao unategemea likizo. Aidha, hata uwezo wa kuelimika unategemea fursa ya kupumzika kuingia darasani. Bila shaka walioweka likizo kwenye Kalenda ya Elimu wanalifahamu hili ndio maana wakaweka likizo kwenye Kalenda ya Elimu. Tatizo linakuja kwa wenye shule kuamua kupuuza kalenda ya elimu with impunity.
 
Mlenge mada yako ni rahisi lakini ina neno zito.
Sheria na taratibu huwekwa kwa kutambua wapo waliowahi kukiuka, wanaokiuka au watakaokiuka

Kudharauliwa kwa kalenda ya elimu ni matokeo wala si tatizo. Zipo mamlaka zinazoshughulika na elimu katika maeneo mengi na wigo wake ni mpana. Kudharauliwa kwa kalenda kunatokea kwa sababu zipi?
Kwamba kuna upungufu wa taasisi! sikweli zipo lukuki. Kwamba, kuna upungufu wa sheria, jibu ni hapana

Kama majibu yote ni hapana,hali inatokeaje with impunity? Kuna tatizo zaidi ya kudharauliwa kalenda kunakopelekea matokeo ya kudharauliwa kwa kalenda
 
Nguruvi3, pengine pana mkanganyiko wa nani mwenye mamlaka ya kuhakikisha Kalenda ya Elimu inafuatwa
 
Ni kweli,mapunziko kwa wanafunzi hata walimu yana umuhimu wake na kuna uhitaji wa kufuata kwa malengo ya kuwapa nafasi walimu kufanya maandalizi kwa muhula unaofuata lakini pia kuwaandaa wanafunzi kuingia katika muhula husika.
Naungana nawe mdau wa elimu kuwa ni vyema kalenda hizi kuheshimiwa.
 
Back
Top Bottom