Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,956
Kijana mmoja baada ya kufunga ndoa,baba yake
alimtaka alete kalamu ya risasi karatasi na ufutio.
Baada ya kijana huyu kuja na vifaa hivi, baba akamwambia
mwanae andika:
Kijana akauliza:Niandike nini?
Baba akamjibu:Andika unacho taka.
Kijana akaandika sentesi.
Baba akamwambia kijana wake:Ifute,akaifuta.
Kisha baba akamwambia kijana wake andika sentesi nyingine.
Yule kijana akaandika sentesi nyingine.
Akamwambia:Ifute,akaifuta.
Kisha akamwambia kwa mara ya tatu:Andika sentesi nyingine.
Kijana akaandika sentesi nyingine mpya.
Akamwambia:Ifute,akaifuta.
Kisha baba akamuuliza kijana wake:Je karatasi bado ni nyeupe(ina sehemu ya kuandikia)?
Kijana akajibu: ndio,
Lakini baba umekusudia nini???
Baba akamshika kijana wake begani,akamwambia:
Kijana wangu, ndoa yahitaji ufutio.
Iwapo kama huto kuwa na ufutio katiaka ndoa yako,
ili uweze futa baadhi ya mambo au matukio ambayo
hufurahishwi nayo kutoka kwa mkeo, na mkeo vile vile
ikiwa hoto kuwa na ufutio ambao anaweza futia
baadhi ya mambo na matukio ambayo hafurahishwi
nayo toka kwako,basi ukurasa wa ndoa utajaa maandishi
kwa siku chache sana!
na kupelekea ndoa kuvunjika.
