Kala Pina kugombea Ubunge Kinondoni

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
23,599
2,000
Jana akihojiwa East Africa Radio amesema uchaguzi ujao atagombea ubunge Kinondoni ili aungane na makamanda wenzake mjengoni.

Pia wiki iliyopita hii radio ilimhoji afande sele akasema atagombea Morogoro Mjini.

Profesa Jay naye amekiri atagombea kwa tiket ya CHADEMA jimbo la Mikumi Morogoro.

Nadhani jinsi siku zinavyoenda wasanii wengi watatangaza nia kupitia CHADEMA.

Uwezekano pia upo wakaingia bungeni.

Kugombea ni haki ya kila mtu ila uongozi wa juu wa CHADEMA waliangalie vizuri hilo swala wanapopitisha majina ya wagombea,maana chama kitajaa wasanii.

Wakuu nye mna maoni gani!!

Msanii maarufu wa muziki wa kufoka foka (hiphop) anasema baada ya kumzingua na kumletea uzinguzi katika nafasi ya udiwani aliyoigombea uchaguzi uliopita, sasa amejipanga vema katika idara zote ili kulinyakua jimbo la Kinondoni na kuwapigania wanyonge wa Kinondoni wanaoliwa vya kwao na wachache.

Hayo ameyasema leo wakati akihojiwa katika kipindi cha Leo Tena (clouds fm). Ameongeza kuwa angekuwepo bungeni wakati wa sakata la escrow angewapigania wanakinondoni by any means hata kama ni kwa kuwapa vitasa wahusika.
 
stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,630
2,000
niliposoma kwa haraka nikajua anagombana, kumbe anagombea, maana hulka yake huwa ni kugombana, sawa mbunge mgomvi.
 
LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,129
2,000
Viol Kalapina ametangaza kugombea kupitia Chadema au Cuf?
 
Last edited by a moderator:

Mdakuizi

Senior Member
Dec 11, 2014
162
0
LIKUD

hajataja chama ila kasema ''nitakuwa na makamanda'',nadhani wanaojiita makamanda ni chadema.
Jamaa ni CUF damu kama alivyo Juma Nature, nadhani alishagombea Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa au Udiwani kupitia CUF lakini akaanguka katika mchujo wa ndani ya chama.
Huyu jamaa alikuwa mshikaji wake sana Miraji wakati huo mkuu wa kaya akiwa Waziri. Yeye ndiye alimuingiza Miraji kwenye uteja wa bangi na sembe, kama ilivyokuwa kwa marehemu Langa (RIP). Kama hajabadilika mpaka sasa, basi huyu ni kijana wa kuogopa kama ukoma, usiruhusu kijana wako akawa na urafiki naye.
Ova
 
Last edited by a moderator:

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
23,599
2,000
Jamaa ni CUF damu kama alivyo Juma Nature, nadhani alishagombea Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa au Udiwani kupitia CUF lakini akaanguka katika mchujo wa ndani ya chama.
Huyu jamaa alikuwa mshikaji wake sana Miraji wakati huo mkuu wa kaya akiwa Waziri. Yeye ndiye alimuingiza Miraji kwenye uteja wa bangi na sembe, kama ilivyokuwa kwa marehemu Langa (RIP). Kama hajabadilika mpaka sasa, basi huyu ni kijana wa kuogopa kama ukoma, usiruhusu kijana wako akawa na urafiki naye.
Ova
jana wakati akihojiwa alisema yeye amewafundisha wengi kwa kupitia nyimbo zake,na pia alikuwa na harakati za kutokomeza vijana kuacha madawa ya kulevya kinondoni
 
kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,825
2,000
wavuta bangi wote wanaona njia rahisi ni cdm. Ukiöa ganja smokers wote wanatangaza nia kuptia cdm jiulze kunani
 
Mdakuizi

Senior Member
Dec 11, 2014
162
0
jana wakati akihojiwa alisema yeye amewafundisha wengi kwa kupitia nyimbo zake,na pia alikuwa na harakati za kutokomeza vijana kuacha madawa ya kulevya kinondoni
Maneno yake na vitendo vyake ni tofauti sana. Ndivyo alivyo huyo Kamanda wa kikosi cha mizinga.
Ova
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom