Kala Pina kugombea Ubunge Kinondoni

Sipati picha hiyo mibange itakayovutwa kwenye viwanja na vyoo vya bungeni..........vile vile watasababisha kupanda kwa bei ya bange mkoani DODOMA......

Kama bei ya changudoa inavyopanda wanapokuwepo wabunge ccm dodoma.
 
Jamaa ni CUF damu kama alivyo Juma Nature, nadhani alishagombea Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa au Udiwani kupitia CUF lakini akaanguka katika mchujo wa ndani ya chama.
Huyu jamaa alikuwa mshikaji wake sana Miraji wakati huo mkuu wa kaya akiwa Waziri. Yeye ndiye alimuingiza Miraji kwenye uteja wa bangi na sembe, kama ilivyokuwa kwa marehemu Langa (RIP). Kama hajabadilika mpaka sasa, basi huyu ni kijana wa kuogopa kama ukoma, usiruhusu kijana wako akawa na urafiki naye.
Ova
...punguza uongo kdg ....
jana wakati akihojiwa alisema yeye amewafundisha wengi kwa kupitia nyimbo zake,na pia alikuwa na harakati za kutokomeza vijana kuacha madawa ya kulevya kinondoni
...harakati zinaendelea..tanzania bila dawa za kulevya inaendelea...zamani ilikua Hip Hop bila Dawa za kulevya inawezekana...
Maneno yake na vitendo vyake ni tofauti sana. Ndivyo alivyo huyo Kamanda wa kikosi cha mizinga.
Ova
...teh teh teh ...
 
Msanii maarufu wa muziki wa kufoka foka (hiphop) anasema baada ya kumzingua na kumletea uzinguzi katika nafasi ya udiwani aliyoigombea uchaguzi uliopita, sasa amejipanga vema katika idara zote ili kulinyakua jimbo la Kinondoni na kuwapigania wanyonge wa Kinondoni wanaoliwa vya kwao na wachache.

Hayo ameyasema leo wakati akihojiwa katika kipindi cha Leo Tena (clouds fm). Ameongeza kuwa angekuwepo bungeni wakati wa sakata la escrow angewapigania wanakinondoni by any means hata kama ni kwa kuwapa vitasa wahusika.
 
Jana akihojiwa East Africa Radio amesema uchaguzi ujao atagombea ubunge Kinondoni ili aungane na makamanda wenzake mjengoni.

Pia wiki iliyopita hii radio ilimhoji afande sele akasema atagombea Morogoro Mjini.

Profesa Jay naye amekiri atagombea kwa tiket ya CHADEMA jimbo la Mikumi Morogoro.

Nadhani jinsi siku zinavyoenda wasanii wengi watatangaza nia kupitia CHADEMA.

Uwezekano pia upo wakaingia bungeni.

Kugombea ni haki ya kila mtu ila uongozi wa juu wa CHADEMA waliangalie vizuri hilo swala wanapopitisha majina ya wagombea,maana chama kitajaa wasanii.

Wakuu nye mna maoni gani!!

Mbona komba yupo anauchapa usingizi bungeni na anaitwa mh?
 
Pia mtembea peku anagombea jimbo la namtumbo kwa tiketi ya ccm
 
Kwa jinsi hoja zinavyichakachuliwa nchi hii taratibu tunaelekea kuwakubali wastaarabu wa nakoz hoja nakoz hoja si imeshuhudiwa kwenye serekali za mitaa. Ukizubaa ushindi unaporwa, sasa kalaP kweli akishinda halafu aporwe ushindi.........!
 
kalapina rafiki yake ni KATANI mwenyekiti wa vijana cuf taifa, hawa jamaa wanafanana kwa kila kitu na wote ni wakorofi. Kalapina asikamie sn bunge maana atambue uongozi sio nguvu lazima ajipange kuweka program vzr ili kuwasaidia wananchi wa jimbo lako hata kwa kutafuta wafadhiri nje.

Km anaenda bungeni kurusha ngumi basi kilalakheri lkn km anaenda kwa lengo la kuwapigania wanyonge inapasa atulize akili. KALAPINA ajue hasira huondoa maarifa anaweza akaenda akapiga domo bungeni na akarusha ngumi au vitasa km anavyosema yeye na miaka mitano ikaisha bila ya yeye kufanya jambo lolote la maana ktk jimbo lake na nchi kwa ujumla.

HII NCHI HAINA MWENYEWE.
 
CCM kila mtu anataka kuwa Rais. Yaani cha ajabu hata mh wa mchoz a k a wapigwe tu naye anapataka Magogoni. Nchi imeozaa hii.
 
Back
Top Bottom