Kala Jelemiah amliza Mama kwenye Basi

Kala Jelemiah amliza Mama kwenye Basi

Ngurubhe

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
1,840
Reaction score
1,049
Hivi ni kweli kuwa hip hop ni uhuni?
hatuwezi kupata mawezo ya kujenga na ya kimapinduzi kutoka kwenye hip hop?.

Si mwingine bali ni mama mmoja ambae jina lake haikuwa rahisi kufahamika,alikuwa kwenye basi la Shabib kutoka Dodoma kuja hapa dar.

Tulianza safari kama SAA 11:27 am hivi na safari yetu haikuwa ya kuchosha sana kwani tulisindkizwa na nyimbo za wasanii mbalimbali ndani ya basi letu.Zilichezwa nyimbo za kila aina yaani za dini,r&b,blues,bongoflavours nk.lakini kubwa zaidi na lilonifanya nitandaze uzi huu hapa ni kile nilichokishuhudia ndani ya gari baada ya wimbo wa Dear God wa kala J kuchezwa,na kabla haujaisha nikamuona mama mmoja akiangua kilio wakati mda wote..

Mama aliekuwa mda wote akilalama akidai kuwa hapendi anaposhuhudia nyimbo ambazo hazina hata tone la maadili zikichezwa mda wote kwenye gari.

Alienda mbali zaidi kwa kusema mbali na kutokuwa na maadili hazifundishi kitu chochote zaidi ya umalaya.aliongea maneno haya akitoa ushahidi kwa kuonesha kwenye skrini(wakati huo kulikuwa kunachezwa wimbo wa mfa maji wa Say nag).

Alikuwa amekaa kiti kimoja na mzee mmoja ambae bila shaka hakuwa mme wake,
kwani Mbaba huyu alionekana yeye anazukubakai baadhi tu ya nyimbo na kutoka kwa baadhi ya waimbaji(wasanii).

Lakini pia alimwambia nyimbo za kisasa nyingi ni burudani tu , mama yule hakika alionekana anatamani arudishiwe nauli apande gari jingine lakini alikuwa ameshachelewa.

Tulipofika maeneo ya mzani tulianza safari mpya na wimbo wa dogo Aslay,na baada ya mda mfupi ukafuata wa Walewale wa Kala Jelemiah.

Na muda mfupi ukawa unaimba wimbo wa Dear God kila mmoja alimshangaa mama huyu aliekuwa anapaza sauti akilalama kuwa nyimbo za vjana wa leo hata hazifai na kumuomba dereva abadilishe nyimbo au ikiweekana azime kabisa,sasa alikuwa analia akiomba wimbo huo wa kala uchezwe hadi mwisho wa safari yetu.

Tulibaki tunacheka baadala ya kumfta machozi kwani tulijifarji kuwa machozi yale yaliashiria uhondo wa wimbo wa kijana Kala. Mama aliiamini ni WAHUNI.

" kumbe haohao wahuni wanaimba vitu vya maana kabisa,ILA ATAKUWA NI HUYU TU JAMANI NA LAZIMA NIMTAFTE".alitamka maneno hayo mama huyo alioneka akili yake yote ameiweka kwenye runinga hata tuliposhuka morogoro kupata chochote yeye hakushuka zaidi ya kumuomba Konda asizime redio ili aendelee kula uhondo huku akidondosha machozi ya kushangaa!.

kila abiria alibaki anamuaangalia tu na kumshangaa nikiwemo mim mwenyewe.sjui anawawakilisha wangappi waliokariri ati hip hop au bongofavour ni uhuni!
 
Wewe unaona si uhuni ,unawajua wana hiphop wa bongo na hata huko america na visa vyao? wahuni wale japo wananiburudisha na kamwe siombei wawe mfano wa kuigwa kwa kizazi changu!
 
Promoo...anataka kutoa single nyingine nini?
 
Promoo...anataka kutoa single nyingine nini?

Ahaaaahaaa mkuu hata mshkaj,hanijui sema mshkj ni mwanaharakati kiaina ana mawazo adimu ujue so chozi la yule mother lilikuwa lazma litoke
 
Wewe unaona si uhuni ,unawajua wana hiphop wa bongo na hata huko america na visa vyao? wahuni wale japo wananiburudisha na kamwe siombei wawe mfano wa kuigwa kwa kizazi changu!

Mkuu sio uhuni,japo wengi wao kweli ni wahuni lakini nyimbo zao nyingi zna maudhui ya kimageuzi....
 
huu uzi umechangiwa na wasiojua muziki ndio maana
 
That is good hisia jambo ambalo kila mtu yuko tofauti na mwenzake hivyo simshangai mama huyo kwan wimbo huo nilivyo usikia kwa mara kwanza nilitaman ujirudie hata mara mia.
 
Wangemuwekea ya afande Sele alipopandisha mzuka jukwaani1
 
That is good hisia jambo ambalo kila mtu yuko tofauti na mwenzake hivyo simshangai mama huyo kwan wimbo huo nilivyo usikia kwa mara kwanza nilitaman ujirudie hata mara mia.

For sure,mshakaj aliona mbali.
 
Habari yenyewe fix tupu tu hii, lakini sishangai kwakuwa basi lilikuwa linatoka Dodoma.
 
Habari yenyewe fix tupu tu hii, lakini sishangai kwakuwa basi lilikuwa linatoka Dodoma.

Hakna cha fix wala salamander,ukweli kwani kuna haja ya kufix cho chote ili iweje?,lengo ni kushare na nyie nilichokiona sawa salamander
 
Mkuu sio uhuni,japo wengi wao kweli ni wahuni lakini nyimbo zao nyingi zna maudhui ya kimageuzi....
tatizo lenu wengi mnafikiri uhuni ni kukosa akili! wahuni ni watu wenye akili timamu ila wamekosa maadili,nidhamu na heshima,wanaweza wakatunga nyimbo nyingi tu zenye maana lakini bado tu wakabakia wakifanya vitendo vyao vya kihuni ndani ya sanaa na nje ya sanaa!sasa katika sanaa ya muziki ,hawa wana hiphop ni vinara wa uhuni wanaendana in par na wanabongo movie-uhuni tu,uzinzi,umalaya kutojitambua aargh!
 
Back
Top Bottom