Korean Air Lines Flight 007: Ndege ya abiria iliyoruka juu ya anga la chuo cha siri cha usalama ikiwa na kamera za upelelezi (Surveillance Cameras)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Korean Air Lines Flight 007: Ndege ya abiria iliyoruka juu ya anga la chuo cha siri cha usalama ikiwa na kamera za upelelezi (Surveillance Cameras)

119991797_7208666286429.jpg

Ndege namba 007 (almaarufu kama Korean Air Lines Flight 007) ya shirika la ndege la nchi ya Korea Kusini ilikuwa ni ndege ilikuwa katika ratiba ya kuruka kutoka jiji la New York nchini Marekani mpaka jiji kuu la Soul nchini Korea ya Kusini ikiwa imefungwa kamera ya upelelezi (surveillance camera) upande wa chini kwa lengo la kufanya upelelezi katika kisiwa ambamo kulikuwa na chuo cha siri sana cha kufunza mashushushu wa jeshi la Soviet (USSR) kwa wakati huo.

Mnamo mwezi wa September mwaka 1983 ndege hiyo ya Korea ilipigwa kombora zito sana na kushambuliwa na ndege vita ya Soviet aina ya Su-15 interceptor.

Ndege hiyo ya Korea aina ya Boeing 747 ilikuwa safarini ikielekea jiji ya Seoul huko Korea lakini kwa bahati mbaya ikapotea njia yake kuu na kujikuta imeingia mkenge katika anga mbalo Soviet walikataza ndege wasizokuwa na taarifa nazo kupita maeneo hayo kwa maana ingetengeneza mwanaya kwa Marekani kuweza kurusha ndege zao za upelelezi.

IMG_20180126_141538.jpg

Baada ya kuona hivyo, jeshi ya anga la Soviet likaamua kuifuatilia ndege ile kama ni ndege ya upelelezi ya Marekani iliyokuwa imefungwa camera kwa sehemu ya chini na kisha kuamua kuvurumisha kombora moja hatari sana la angani, baada ya kutoa kuwa walikwisha rusha makombora ya onyo mara kadhaa ambayo inaonekana rubani wa ndege ile ya kiraia hakupata nafasi ya kuyaona.

Hatimaye ndege ile ya Korea ikaangukia baharini katika bahari ya Japan karibia na kisiwa cha Moneron. Abiria wote wapatao 269 pamoja na wahudumu wote waliuawa. Urusi walikuja kufanya operation ya utafutaji na kufanikiwa kupata kile kisanduku cheusi cha kutunza kumbukumbu za taarifa za ndege mwezi October lakini taarifa zile zikafichwa na kufanywa kuwa siri sana kwa maana walijua walitenda kosa kubwa sana la kibinadamu mpaka ilipofika mwaka 1993.

Mwanzoni kabisa warusi walikataa kata kata kuhusika na utunguaji ule lakini baadaye wakaja wakakiri kuhusika na kosa kwa kisingizio kwamba ndege ile licha ya kwamba ilionekana ni ya kiraia lakini ilikuwa katika mission ya upelelezi kwa niaba ya Marekani na washirika wake wa Magharibi (NATO)

IMG_20180126_141611.jpg

Idara ya usalama ya USSR walikuja kusema kuwa hilo tukio lilikuwa ni tukio la makusudi na la uchokozi la Marekani pamoja na NATO ili kupima utajari wa kijeshi na kimapambano wa Soviet pamoja na kutaka kuzua vita kibwa saanaaaa.

Marekani ikaja kuishutumu Soviet kwa kukandamiza na kudhoofisha juhudi na shughuli nzima za utafutaji na uokozi ili kupoteza evidence za tukio zima, kisha jeshi la Soviet likaja kuchakachua ushahidi pamoja na report za tukio zima zilizotafitwa na kuandaliwa na chama cha kimataifa cha usafiri wa anga na ndege za abiria ikiwa ni pamoja na kuficha kifaa cha kutunza kumbukumbu za taarifa za ndege, ambazo zote kwa pamoja zikaja kuwekwa hadharani mnamo miaka ya 1990 baada ya kuvunjika kwa umoja wa nchi za kisovieri (USSR)

Tukio hili lilikuwa ni moja kati ya matukio mazito na yaliyoleta mvutano mkubwa sana wakati wa vita baridi na kupelekea kuongezeka kwa chuki zaidi thidi ya Soviet huhusan ndani ya Marekani.

images (62).jpg

Baada ya tukio ili Marekani ikaamua kubadili utaratibu wa njia ya ndege zake zinazoruka zikitokea Alaska.

Hii issue ilikuwa imekaa hivi wakuu. Mfumo wa anga pamoja na rada za ulinzi ulifanikiwa kuiona hii ndege kwa mbali sana takribani kilometers 400 mbali kabisa na Kingo za bahari za Soviet.

Kwa mwanzoni sana walinzi wa baharini walidhaniwa ilikuwa ni ndege za kwao iliyokuwa inatoka kwenye mission flani hivi ambayo kwa bahati mbaya rubani wake alisahau kubadili "transponder code" yake.

images (60).jpg

Sasa wakati ndege hiyo ya kikorea ilipokuwa inavuka peninsula ya Kola muda kama wa saa tatu usiku, kamanda wa jeshi la anga akamtuma rubani Alexander Bosov kwenda kuizuia ndege ile ya abiria ya kiraia.

Sasa kwa bahati mbaya rubani bosov akaifananisha ndege ile na ndege ya upelelezi ya Marekani pamoja na NATO. Kulingana na maelezo ya baadhi ya mashuhuda wa tukio, ndege vita ya Soviet alisogelea ndege ya Korea kutokea upande wa kulia na sio upande wa kushoto kama ambavyo kama ambavyo taratibu na sheria za kimataifa zinavyohitaji.

Inasemekana rubani wa ndege ya Korea alipunguza speed ya ndege kisha akawasha taa za nje za ndege akishiria ya kwamba alikuwa tayari kufuata maelekezo ya ndege vita ili ende kutua wapi salama salmin bila mikwaruzano wala kugombana.

images (63).jpg

Kulingana na taarifa za jeshi inaonekana rubani wa ndege ya raia ya uvamizi alikuwa mbishi sana huku akikataa commands zilizomtaka aifuate ile ndege ya vita ili imuelekeze wapi ni sehemu anapotakiwa kutua kwa usalama wake, badala yake yule rubani mvamizi akaongeza speed na kuanza kukimbia kwa kasi ya ajabu kuelekeza ndege kwenda Finland.

Rubani wa Soviet bwana bosov alijaribi sana sana tena sana kuwasihi na kuwashawishi makamanda wake wa juu ya kwamba ile ndege haikuwa na uwezo wa kuleta tishio lolote lile la kijesho kwa usalama wa taifa lao, ila baada ya kupata amri kutoka juu ya kutaka ndege itunguliwe akawa hana jinsi tena zaidi ya kuvurumisha kombora la ndege yani ile vuuuuuuup.

Kombora la kwanza lilipita pembeni mwa ndege, la pili likapiga bawa la kushoto na kufanya ndege iyumbe na kutoka kwenye njia yake kama mita nne hivi kisha moja kati ya engines zake kuzimika.

IMG_20180126_141642.jpg

Baada ya kupigwa makombora ya kutosha, ile ndege ilishuka chini ghafla kutoka futi 30,000 mpaka chini kabisa ardini na kupotea katika rada za jeshi za urusi. Rubani mwingine akatumwa kwenda kufanya shambulizi la pili akichukua nafasi ya Bosov ambaye ndege yake ilikuwa imeishiwa kibisa mafuta.

Dakika kama arobaini baadaye, ndege hiyo iliruka mpaka peninsula ya Kola kwa chini chini kidogo huku rubani akitafuta sehemu salama ya kutua.

Baada ya kujaribu kutua kwa mara kadhaa bila mafanikio, rubani akaamua kuituisha ndege juu ya lundo la barafu karibia na mpaka wa Finland.

Wataalam wa upande wa Finland walisema ya kuwa mifumo ya ulinzi wa anga wa Russia hawakuwa na taarifa yoyote ya wapi ile ndege ilikuwapo baada ya kupotea kutoka kwenye radar zao za ulinzi wa anga.

Serikali ya urusi hatimaye ikaamua kutoa helicopters kwa ajili ya uokozi........
===============
Itaendelea wiki ijayo. Stay tuned.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mkuu fanya masahihisho kidogo sana kwenye hii story yako. Ina mapungufu madogo. Kwanza route siyo hiyo uliyoisema. Pili hiyo sehemu hakuna chuo cha usalama wa Urusi. Hapo ni Sakhalin ambapo kuna Naval Base ( Nuclear submarines) inayojumlisha pia Military Districts za Far Eastern Front ya Russia. Tatu sequence ya events ni hivi. Kwanza crew wa KAL 007 walikuwa the most exeperienced na Kapteni wa hiyo ndege alikuwa amependekezwa kuwa Pilot wa ndege ya Rais wa Korea Kusini. Kama ujuavyo route ya ndege haswa 747 inakuwa programmed before take off na ndege kama hiyo inakuwa monitored hata kutoka Boeing Hq kwenyewe. Baada ya takeoff kilichowashtua warusi ni ile "pattern" ya flight. Ukiangalia jiografia ya Sakhalin ni kuwa ndege ilikuwa "inadeviate" na kuingia kwenye anga la Sakhalinski halafu inakaa kwa muda halafu inarudi kwenye route yake ya kwaida. Wakati huo huo kulikuwa na "geostationary satellite: kwenye orbit hiyo hiyo kiasi cha kwamba kuna wakati ndege hiyo na satellite hiyo vilikuwa kwenye mstari mmoja. Kamanda wa Eastern front alituma ndege Mig-25 ili aiteremshe kwenye uwanja wo wote wa kiraia kwa ajili ya uchunguzi. Pilot wa Mig-25 aliswitch on international frequency na kuiita lakini pilot wa KAL hakujibu. Akatangulia mbele yake na kumwashia taa kama "follow me" lakini KAL 007 hawakutii. Pilot akaarifu Moscow kwamba ndege hiyo ilikuwa imekaidi jitihada zote na ilikuwa ni ya abiria. Wakati huo KAL 007 walikuwa wamemaliza "pass ya tatu" juu ya Sakhalin na muda si mrefu wangekuwa kwenye "international airspace", hapo ndipo General aliyekuwa zamu Moscow akatoa amri "Take out the target". Ilitunguliwa na makombora mawili.
 
Thanks so much brother. Every source on my books tells its own stories. Asante kwa kuongezea nyama mkuu. Be blessed.
 
Back
Top Bottom