MUSSA ALLAN
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 18,925
- 13,279
Mbona Kilain alisema Kikwete nichaguo la mungu akifaham fika anafanya dhambi kwa kudanganya umm
Lakini hakukuchaguliwa bunge la katiba je ummemsikia akisema chochote? bado unaendelea kupotosha
Unamaana ukiipendelea nakusema uwongo kuisifia ccm unapewa takrima mbalimbali kimagumashi?
ulichoandika ni hiki hapa chini.
kwa mujibu wa maelezo hayo uliyoandika leta majibu mm sihitaji propaganda nahitaji majibu kwa mujibu wa maelezo yako nikeleweshwa nikaelewa sina maneno.
Kakobe amesikika mara nyingi akilalamika kutochaguliwa kama mbunge wa bunge maalumu la katiba, mpaka akamwandikia rais waraka!
Sio kakobe tu aliye upande wa upinzani, rejea tamko la TEC na la CCT yoote yalisimamia katika kuyaheshimu maoni ya wananchi yaliyowakilishwa na tume ya wariba. Kimsingi watu hawa wanaonekana kuwa sambamba na upinzani lakini uhalisia sii kweli kwamba wao ni upinzani l hasha. Wao ni wazlendo kwa taifa lao na kila aliye na matendo ya kizalendo yupo ama wapo nae upande mmoja. Hivyo kwa uzalendo wa ukawa kusimamia matakwa ya wananchi tofauti na manyangau sisiem kukaa upande wa kifedhuli wa kuhujumu matakwa ya umma ulio mpana ili kufanikisha matendo yao maovu hakuna mwenye akili anaeweza kuwa upande wao. Sisi raia tunasema tuko bega kwa bega na viongozi wetu walio upande wa ukawa ambao kimsingi wapo upande wetu katika kuheshimu umiiki wa tunu za taifa letu na sisi wenyewe. Wafanye wawezalo kufanya hata kama wakipitisha katiba kwa hila zao hiyo itakuwa ni katiba ya wana ccm na kamwe sisi raia tusi ccm au kuwa na chama chochote hatutakubali kamwe ituongoze. Tutapigana kufa kopona kupata katiba ya nchi iliyoridhiwa na makundi yoote.
.
CCM ndio imepewa ridhaa na wananchi wa TANZANIA ili kuunda mamlaka halali inayoongoza nchi. Huyo Kakobe unayesema yuko upande wa wananchi, angekuwa wa kwanza kuisapoti CCM na serikali yake na sio hawa UKAWA.
Hisia zipi? Za kutokuchaguliwa bunge la katiba?
Nilikuwa nakuheshimu, ila No Longer!
hivi katiba ni ya chama gani...?
Katika hali ya kawaida haitakiwi kuwa ya chama chochote, ya sasa ni ya CCM. Maana yangu ni kuwa katiba ya Tanzania ya sasa ni katiba inayo cater kwa maslahi ya CCM na si ya taifa.
Ninachosema ni kuwa Kakobe anatakiwa kutoa maoni yake kama mtanzania, akianza kuingia kwenye siasa za UKAWA na CCM anakuwa anacheza siasa. Kitu ambacho hakifai.
Unamuonea kakobe ndugu Yangu! Yeye ameunga mkono rasimu kama ilivyopendekezwa na wananchi.
Bahati nzuri baadhi ya vyama vya siasa walikuwa wajanja sana wakaiunga mkono rasimu ya serikali tatu. Na ndicho Kakobe anachokubaliana nacho wala si maoni yake binafsi yeye kama mtumishi wa Mungu hapaswi kuonesha unafiki ni dhambi hongera sana baba askofu Kakobe.
Vyama vinavyounda UKAWA havikuwa na misimamo ya muundo isipokuwa vilikubaliana na kuheshimu maoni ya wananchi, ccm wakabaki na msimamo mkali wa serikali mbili ambayo ni nzee mpya itakuwa 3.
Nini kifanyike: mchakato umekwama na wakuukwamua alichakufa ambaye ni Mwl.Nyerere. sasa ni fursa kwa marais wastaafu kunusuru huu mchakato maana Rais wetu Kikwete amesongwasongwa na hana maamuzi kama yeye tena.
Mkapa na Mzee mwinyi hamna hata huruma mmekaa kimya wakati mnakula kodi zetu mnajifanya hamuoni nchi ilipo kwa sasa? Vunjeni bunge BMK joto la uchaguzi limepanda hakuna katiba mpya.
Poleni sana ccm kwa kushindwa kusoma alama za nyakati mnaangamia wenyewe.
Mkuu ukweli ni kuwa katiba ya serikali 3 itakuwa mwisho wa CCM na wananchi wanataka hiyo, serikali ya CCM ilifanya makosa kuruhusu tume ya Warioba ikusanye maoni.
Kuhusu Mzee Mwinyi na Mkapa kukaa kimya, ukweli ni kwamba hawawezi kusema lolote. Kumbuka tume kuhusu marekebisho ya katiba wakati wa mzee wa Mwinyi, walikataa kila kuti hadi Nyerere alipowaambia wakubali kuleta vyama vingi. Mwinyi aalikataa maoni, lakini yeye alikataa kwa msingi wa matokeo ya kura za maoni.
Mkapa alimwambia Jaji Kisanga (not sure) amekiuka hadidu za rejea, kwa hiyo akapuuza maoni ya watanzania, akaleta yake na ndio yamerudi tena kwa JK.
JK anachofanya sasa ni kusubiria tu muda na kucheza danadana na kumuachia janga hili rais ajaye.
Ingekuwa vizuri sana Mchungaji Kakobe angeweka mkazo kwenye dini. Siasa angewaachia wanasiasa. Uchungaji wake unaleta viulizo pale anapoanza kujiingiza kwenye siasa. Aamue moja awe kama Dk Slaa.
aliposema kikwete ni chaguo la mungu alikuwa mpinzanikakobe siku zote ni mpiga debe wa wapinzani.
aliposema kikwete ni chaguo la mungu alikuwa mpinzani
Kakobe siku zote ni mpiga debe wa wapinzani.
Yohana MBATIZAJI Alikemea WATAWALA Alipoona Wamekosea.Leo the so-called Watumishi Wanatumiwa kama CD.Keep it up KAKOBE !
Nilijua wewe utajitokeza kumpinga Kakobe maana wewe unachuki naye sana!!Je unajuwa mwisho wa yohana mbatizaji? Alishiawapi? Mwambie Kakobe aachane na siasa.
Kwa nini Ukawa wametoka Bungeni kama kauli ya Kikwete haikuwa Mbaya??Tulia Anko,
Kakobe siku zote amekuwa akitumia kanisa lake kufarakanisha wananchi wenye itikadi tofauti na yeye.
Tabia hii kwa kiongozi wa dini sio nzuri. Ni bora akavua joho la uaskofu na kuingia siasani kama alivyofanya Mzee Slaa.