Kakobe amponza muumini wizarani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe amponza muumini wizarani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Mar 1, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,018
  Likes Received: 6,830
  Trophy Points: 280
  na Betty Kangonga

  MFANYAKAZI wa Wizara ya Nishati na Madini, Doroth Mtweve, amehamishwa kutoka makao makuu ya wizara hiyo baada ya kudaiwa kuvujisha siri za ofisi kuhusiana na sakata linaloendelea baina ya Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

  Mtweve ambaye alikuwa Katibu Muhtasi Daraja la Tatu katika ofisi hiyo, pia anadaiwa kuhamishwa katika ofisi hiyo na kupelekwa Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki, baada ya kugundulika kuwa ni muumini wa kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Zakaria Kakobe.

  Muumini huyo aliyekuwa Katibu ya Wizara ya Nishati na Madini alikabidhiwa barua hiyo Februari 22 mwaka huu na kutakiwa kuhama.

  Habari za kuaminika ambazo Tanzania Daima imezipata zinaeleza kuwa Mtweve alikabidhiwa barua ya uhamisho Februari 22 mwaka huu yenye kumbukumbu namba Na . MEM/PF.216/52 iliyosainiwa na C.M Musika kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara.

  Chanzo hicho kinaendelea kueleza kuwa mfanyakazi huyo anadaiwa kuvujisha baadhi ya barua zinazohusiana na mgogoro huo ambazo zimekwa zikimfikia askofu huyo bila wizara kuelewa.

  Hata hivyo inadaiwa pamoja na barua hizo kufika kwa Kakobe, pia Mtweve amekuwa akionekana mara kadhaa akiwa amevaa fulana maalum ambazo huvaliwa na waumini wa kanisa hilo zenye maandishi ya kupinga upitishaji wa nguzo za umeme wa kilovolti 132. Fulana hizo kwa mbele zimeandikwa ‘TANESCO Muogopeni Mungu’ na ‘Badala ya Richmond sasa Mmeligeukia Kanisa’ kwa nyuma.

  Habari hizo zinaeleza kuwa Februari 22 mwaka huu kabla ya kukabidhiwa barua ya uhamisho, Mtweve aliitwa na mkurugenzi wa masuala ya utawala aliyefahamika kwa jina moja la Musika na kumwomba amuulize swali aliloliita ‘chafu’.

  “Huyu dada aliitwa na bosi wake ambaye alimuomba amuulize swali chafu, kuwa ni muumini wa kanisa gani, ndipo Mtweve alijibu kuwa anaabudu katika Kanisa la Askofu Kakobe lililopo Mwenge,” kilieleza chanzo hicho cha habari.

  Chanzo hicho kieleza kuwa kitendo hicho kilimfanya mkurugenzi huyo kumweleza kuwa aliliita swali chafu kwa kuwa kazi haihusiani na masuala ya dini ya mtu na kumruhusu kuendelea na shughuli zake.

  Hata hivyo, inaelezwa kuwa baada ya dakika 10 toka Mtweve atoke ofisi za Musika ndipo alimfuata Katibu Mhtasi wake na kumtaka aonyeshe lilipo jalada lake la kazi.

  “Huwezi kuamini lakini ndiyo ukweli; huyo dada amefanyiwa fitina kama siyo mtego, kwani baada ya kutoka ofisi za mkurugenzi alifuatwa na kuambiwa aonyeshe lilipo jalada lake la kazi wakifikiri atakuwa amelificha ndipo alipowaambia lipo kwa mhasibu wa wizara,” kilifafanua chanzo chetu.

  Chanzo hicho kinaeleza kuwa ilipofika majira ya saa 10 siku hiyo hiyo, Mtweve alipewa barua ya uhamisho ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake.

  “Ili kuimarisha kazi, imeamuliwa uhamishiwe ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki. Upatapo barua hii unatakiwa kukabidhi kazi zako kwa mkuu wako wa kazi na kuripoti kwa Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa Kamishna wa Madini, Kanda ya Mashariki.

  Tanzania Daima ilipowasiliana na Mtweve, alikiri kupewa barua ya uhamisho na kwamba ni kweli ni muumini wa Kakobe.

  “Baada ya kuhamishwa na kwenda kuripoti bosi wangu mpya aliniuliza kwa nini nimekuwa nikivujisha siri za ofisi kwa Askofu Kakobe? Nilimjibu kosa langu ni kukubali kupeleka barua kwa watu, kwani mara kadhaa nimekuwa nikitumwa na kupeleka barua sehemu mbalimbali ikiwamo kwa Askofu Kakobe,” alisema.

  Alisema baada ya siku chache alitakiwa kujieleza kwa maandishi kuhusiana na tuhuma hizo na kuongeza kuwa mpaka sasa bado hajaandika maelezo hayo.

  Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, David Ngairo, kuzungumzia suala hilo, alishindwa kukubali wala kukanusha na badala yake kumtaka mwandishi wa habari hizi kumweleza ni wapi alikozipata taarifa hizo.

  “Kwanza sina la kujibu, iwapo unataka nizungumze niambie aliyekuletea taarifa hizo ili niweze kujibu,” alisema na mwandishi alipokataa kumweleza alikopata habari hizo alikata simu.

  Mgogoro wa Kakobe na TANESCO ambao umedumu kwa zaidi ya siku 60 sasa bado hatma yake haijajulikana licha ya Waziri William Ngeleja kukaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa wiki hii angeweza kutoa ripoti kamili kuhusu upitishwaji wa waya katika eneo hilo.
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sijaelewa amehamishwa kwa sababu ya kuabudu huko kwa kakobe au kwa kuvujisha siri za wizara?
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,258
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  breking nyuzi nyingine zimekaa kiaina!
   
 4. T

  Tom Lyimo Member

  #4
  Mar 1, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo kali kuabudu tu kanisa tatizo?
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Kulingana na maelezo ya mwandishi inaonekana ni vyote viwili kwa pamoja.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  No comment. Piga ua garagaza.......lakini hii habari imekaa kiudaku zaidi....inajichanganya
  Kama ni kweli kavujisha siri basi anahitaji kutiwa nidhamu. Lakini kwenye mavazi kuna code of conduct ya mavazi kwa waajiriwa wa serikali. Tshirts zenye maneno yasiyothibitishwa hazitakiwi.
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Duh! what was the secret?
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,187
  Likes Received: 2,712
  Trophy Points: 280
  Kakobe kweli kiboko "Badala ya Richmond sasa Mmeligeukia Kanisa"
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280


  Kama alipeleka barua kwa Kakobe kama mojawapo ya majukumu yake ya kazi,basi inawezekana hakuna ushahidi kuhusiana na yeye kuvujisha siri, if thats the case then muumini huyo anaweza kuwafungulia mashtaka Wizara husika.
   
 10. senator

  senator JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mdau hapo upo sawa kabisa na nadhani hicho ndo kimechangia kwa asilimia kadhaa kwake kuhamishwa ila kuna uwezekano mkubwa akawa anavujisha habari za wizara kwa kakobe.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,018
  Likes Received: 6,830
  Trophy Points: 280

  umesahau""TANESCO MWOGOPENI MUNGU""
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Hilo hapo juu ni kweli ila haionyeshi kama hilo ni sawa na kuvujisha siri,tuhuma za kuvujisha siri ni lazima uprove beyond reasonble doubt kwa ushahidi.
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,971
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Katendewa haki yake. aendelee kumtukuza Mungu.atamlinda juu ya kuvujisha siri au kutotambua ethics za kaisari. Na Mungu ni mkubwa kweli angekuwa taasisi binafsi ndo angejua mungu anahitaji watu wenye nidhamu.
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kuna mtu nilibishana sana nae asubuhi ofisini kuhusu hili swala mwishoe ikaja hoja ya udini ila lazima tuweni wakweli katika hili ni kitu kibaya sana mfanyakazi wa sehemu ukachukua siri ya sehemu kwenda kuwapelekea watu wasio na uhusiano na hiyo sehemu.

  Mfanyakazi yeyote akija kugundulika amevujisha siri hukumu yake sio kuhamishwa bali kufukuzwa kazi. Sasa kwa hili kama wanazo evidence mie nadhani wamemuonea huruma maana sheria za kazi ni kwamba ufukuzwe kazi. Sasa inawezekana mambo mawili either jamaa wamekosa evidence but wanamsuspect kuwa amevujisha siri. Kama wamefanya hivyo basi itakuwa ni jambo baya sana. However, ikiwa bibie ni kweli alifanya hayo manyago na akawa anafanya out of jazba huku akijua anaweza kufukuzwa basi watakuwa wamemuhamisha kwasababu hawana evidence na ashukuru mungu kwani wangelikuwa na evidence halina mjadala ni kwamba unachukua chako
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  alikuwa anajua kilichomo kwenye hizo barua?
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Inasemekana alikuwaga akipeleka barua za mwaliko bila ya kuzisoma but hii ni kwamba alikuwa akichomoa zile memos, na barua za ndani zinazoenda idara moja to nyengine na kupeleka kanisani kwa ajili ya kuliokoa kanisa according to Tanzania daima.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kama umeisoma hii statement inaonekana dada anataka sympathy kwakuwa amefanyiwa fitna but hajibu kwanini amehamishwa kazi???
   
 18. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 2,020
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Bila shaka TANESCO wametibuliwa na Kakobe connection ila wamejihadhari kujifunga rasmi na sababu hiyo ya kumuhamisha huyo dada. Hiyo ya kuwa muumini wa Kakobe na/au kuvujisha siri vimeachwa vielee na kutafsiriwa vyovyote na yeyote kwani Taneso hawana ubavu wa kuvifikisha mahakamani na pia ni hatari kisiasa kwa shirika na serikali hususan katika enzi hizi mijadala ya udini inapojiinua upya.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Kama hakuna ushahidi kuwa amevujisha siri basi amebaguliwa kwa vigezo vya dini.
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  That is true but je hajavujisha siri maana tusikimbilie katika dini pasina kuwa kwanza tujue alivujisha siri au la
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...