Kakobe alitumwa?

Kakobe alitumwa?

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
KAKOBE ALITUMWA? MBONA WAPINZANI WAMEFANYA MASHAMBULIZI YAKE DHIDI YA RAIS MAGUFULI KUWA AGENDA ZAO? WAMEKOSA AGENDA ZA KUJISHINDANISHA NA SERIKALI YA CCM KWA WANANCHI?

Tangu Kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(FGBF), Zacharia Kakobe atumie Madhabahu kumshambulia rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe Magufuli, Wanasiasa wa Upinzaji wamedandia shutuma za Kakobe na kuzifanya agenda zao kuendeleza kwa kasi ya ajabu porojo za kutaka kuwafanya viziwi na vipofu Watanzania waache kuona na kusikia juhudi za Serikali chini ya Rais Mahiri kabisa, JPM za kuijenga Tanzania mpya na badala yake waamini uzushi, porojo na vimaneno maneno vya hovyo hovyo kwamba rais akatubu, sijui rais hakosolewi na upuuzi mwingi tu.

Kwa jicho la tatu unaweza kuamini kuwa yale hayakuwa maneno ya KAKOBE bali alilipwa na kutumwa kufanyakazi ya wanasiasa ambao kupitia kwa viongozi wa dini aina ya Kakobe wanaweza kupambana na serikali ambayo kimsingi imeonesha kuzikonga nyoyo za wananchi wake kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.

Hivi Unawezaje kutofautisha maneno ya Kakobe na porojo za wanasiasa kwamba kuna utawala wa kidikteta, kuminya demokrasia, kutokubali kukosolewa? Hivi hayo madhaifu ya Serikali yanaonekana machoni mwa wana siasa na akina Kakobe? Wanachi wa kawaida ambao kiu yao ya siku nyingi ya kutaka kuona watoto wao wanasoma bure, madawa yanapatikwpana mahospitalini, madini yao, gesi yao, Mafuta yao hayaibiwi na wajanja, Barabara za juu na chini zinajengwa, Reli ya kisasa inajengwa, bei nzuri ya mazao, urasimu katika kupatikana kwa pembejeo na mbolea unatokomezwa, wanafunzi wanapata mikopo kwa wakati , wao hawana macho?

Najiuliza tu:

Kwanini upinzani unajipa kilema cha kujimaliza kwa hoja na mbinu nyepesi nyepesi sana kiasi hiki kupambana na Serikali mahiri kama hii ya awamu ya tano? Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 upinzani utachomoka kweli kwa hoja za akina Kakobe kweli? Eti serikali haikosoleki, kweli? Mwananchi apigie kura upinzani kwa sababu hiyo tu? Sawa haikosoleki lakini tuna maji, tunapata mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati, watoto wetu wanasoma bure na wale wa vyuo vikuu wanapata mikopo kwa wakati, madawa yako hospitalini n.k. Hivi wananchi wakiwapa hizo kama sababu za kumchagua tena JPM mtakuwa na la kuwashawishi tena?

Wapinzani mnapoteza muda kukwapua mashambulizi ya akina kakobe na kuyafanya agenda zenu , mtaumbuka, muwe wabunifu wa hoja nzito za kwenda nazo kwa wananchi siyo hizi za kuwanunua nunua wenye njaa kama akina Kakobe na kuanza kuzikomalia.

Mnachekesha sana. Hivi mnategemea Mshinde uchaguzi kupitia waumini wa Kakobe ambao hata kanisa lake pale Mwenge pamoja na kuwa dogo lililojibananisha pale njiani halijai? BAVICHA mmoja akasema CCM msimpuuze Kakobe ana waumini wapiga kura mil.10. Ujinga mtupu. Watanzania hatujafikia mil.50. Watoto ambao hawajafikia umri wa kupiga kura ndiyo wengi, wanaojiandikisha kupiga kura ni wengi lakini wanaojitokeza kupiga kura hata mil.10 hawafiki. Ina maana wote wanaokwenda kupiga kura wote wanatoka kwa Kakobe? Hizi ni akili za Makarai ya Zege kwelikweli.

Waumini wa Kakobe wenyewe ni kama watu waliokata tamaa ya maisha sijadhani kama wanakuwa na hata wazo la kupiga kura. Ni wale wanaokwenda kuvuliwa mikufu ya dhahabu na Kakobe na kuiuza kwa ajili ya kujipatia fedha huku akiwahadaa kwamba vitu hivyo vya thamani ni chukizo kwa Mungu, hawa watapata muda wa kupiga kura? Ni wale ambao wanaabudu kwa kusikiliza ujumbe wa Mungu wao (KAKOBE) redioni maana akisafiri hakuna ruhusa ya mtu mwingine kuendesha ibada. Hawa wanapiga kura kweli?

Wapinzani jitafakarini sana, waaseni vijana wenu mitandaoni wabuni mbinu mpya za kupambana na serikali ili kupitia kwao siku moja mshike dola. Hamuezi kushika dola kwa Hoja za akina Kakobe.
 
Je wewe pia umetumwa kuja kuuliza huu ujinga humu? Aliyeambiwa atubu yupo kimyaa ila inzi wake ndiyo mmechanganyikiwa kabisa kila mtu anataka kutafuta kiki kwa mkulu ili aonekane kadri mnavyozidi kuchokonoa ndivyo mnavyozidi kusambasa moto ni heri mgekaa kimyaa tu yawezekana na watu tungekuwa tuliisha sahau habari hii ya kutubu.
 
Et juhudi za rahic pumbavu kabisa wewe huyo rahic wako alikuta uchumi unakuwa kwa wastani 7:7% leo umeshuka mpaka 6:8% according to Dr mpango bado unasema juhudi? Juhudi za kuua uchumi wa nchi? Kwataarfa yako wa tz waleo syo wajinga kama wale wa zidumu fikra za mwenyekiti.most of them they know what's going on
 
mkuu, kakobe ana kanisa kila mkoa na wilaya zote hapa tz, sio pale mwenge tu, halafu makanisa makubwa hapo dsm na kwingine hayo ya walokoke wengi wao ni waumini wake/walikuwa waumini wake/yeye ni mwalimu wao. hivyo that attack is not only against full gospel members wa kakobe, mimi sisali full gospel, but imekuwa attack kwangu, ni attack kwa kundi kubwa sana. kwani ulishawahi kwenda kusali pale, pale mwenge ana waumini si chini ya alfu ishirini, ambao ni watu wazima, kila mkoa ana waumini, walokole wapo kila mkoa na wilaya na kijiji...wapumbavu kama wewe ndio wanaoligawa taifa hili kwa ku strike icon persons....nchi hii tumekabidhi wa watu wasiojulikana kabisa aisee.
 
KAKOBE ALITUMWA? MBONA WAPINZANI WAMEFANYA MASHAMBULIZI YAKE DHIDI YA RAIS MAGUFULI KUWA AGENDA ZAO? WAMEKOSA AGENDA ZA KUJISHINDANISHA NA SERIKALI YA CCM KWA WANANCHI?

Tangu Kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(FGBF), Zacharia Kakobe atumie Madhabahu kumshambulia rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe Magufuli, Wanasiasa wa Upinzaji wamedandia shutuma za Kakobe na kuzifanya agenda zao kuendeleza kwa kasi ya ajabu porojo za kutaka kuwafanya viziwi na vipofu Watanzania waache kuona na kusikia juhudi za Serikali chini ya Rais Mahiri kabisa, JPM za kuijenga Tanzania mpya na badala yake waamini uzushi, porojo na vimaneno maneno vya hovyo hovyo kwamba rais akatubu, sijui rais hakosolewi na upuuzi mwingi tu.

Kwa jicho la tatu unaweza kuamini kuwa yale hayakuwa maneno ya KAKOBE bali alilipwa na kutumwa kufanyakazi ya wanasiasa ambao kupitia kwa viongozi wa dini aina ya Kakobe wanaweza kupambana na serikali ambayo kimsingi imeonesha kuzikonga nyoyo za wananchi wake kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.

Hivi Unawezaje kutofautisha maneno ya Kakobe na porojo za wanasiasa kwamba kuna utawala wa kidikteta, kuminya demokrasia, kutokubali kukosolewa? Hivi hayo madhaifu ya Serikali yanaonekana machoni mwa wana siasa na akina Kakobe? Wanachi wa kawaida ambao kiu yao ya siku nyingi ya kutaka kuona watoto wao wanasoma bure, madawa yanapatikwpana mahospitalini, madini yao, gesi yao, Mafuta yao hayaibiwi na wajanja, Barabara za juu na chini zinajengwa, Reli ya kisasa inajengwa, bei nzuri ya mazao, urasimu katika kupatikana kwa pembejeo na mbolea unatokomezwa, wanafunzi wanapata mikopo kwa wakati , wao hawana macho?

Najiuliza tu:

Kwanini upinzani unajipa kilema cha kujimaliza kwa hoja na mbinu nyepesi nyepesi sana kiasi hiki kupambana na Serikali mahiri kama hii ya awamu ya tano? Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 upinzani utachomoka kweli kwa hoja za akina Kakobe kweli? Eti serikali haikosoleki, kweli? Mwananchi apigie kura upinzani kwa sababu hiyo tu? Sawa haikosoleki lakini tuna maji, tunapata mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati, watoto wetu wanasoma bure na wale wa vyuo vikuu wanapata mikopo kwa wakati, madawa yako hospitalini n.k. Hivi wananchi wakiwapa hizo kama sababu za kumchagua tena JPM mtakuwa na la kuwashawishi tena?

Wapinzani mnapoteza muda kukwapua mashambulizi ya akina kakobe na kuyafanya agenda zenu , mtaumbuka, muwe wabunifu wa hoja nzito za kwenda nazo kwa wananchi siyo hizi za kuwanunua nunua wenye njaa kama akina Kakobe na kuanza kuzikomalia.

Mnachekesha sana. Hivi mnategemea Mshinde uchaguzi kupitia waumini wa Kakobe ambao hata kanisa lake pale Mwenge pamoja na kuwa dogo lililojibananisha pale njiani halijai? BAVICHA mmoja akasema CCM msimpuuze Kakobe ana waumini wapiga kura mil.10. Ujinga mtupu. Watanzania hatujafikia mil.50. Watoto ambao hawajafikia umri wa kupiga kura ndiyo wengi, wanaojiandikisha kupiga kura ni wengi lakini wanaojitokeza kupiga kura hata mil.10 hawafiki. Ina maana wote wanaokwenda kupiga kura wote wanatoka kwa Kakobe? Hizi ni akili za Makarai ya Zege kwelikweli.

Waumini wa Kakobe wenyewe ni kama watu waliokata tamaa ya maisha sijadhani kama wanakuwa na hata wazo la kupiga kura. Ni wale wanaokwenda kuvuliwa mikufu ya dhahabu na Kakobe na kuiuza kwa ajili ya kujipatia fedha huku akiwahadaa kwamba vitu hivyo vya thamani ni chukizo kwa Mungu, hawa watapata muda wa kupiga kura? Ni wale ambao wanaabudu kwa kusikiliza ujumbe wa Mungu wao (KAKOBE) redioni maana akisafiri hakuna ruhusa ya mtu mwingine kuendesha ibada. Hawa wanapiga kura kweli?

Wapinzani jitafakarini sana, waaseni vijana wenu mitandaoni wabuni mbinu mpya za kupambana na serikali ili kupitia kwao siku moja mshike dola. Hamuezi kushika dola kwa Hoja za akina Kakobe.
Madhara ya kuwanyima watu/vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa hata kama yapo kisheria ndo hayao sasa.huwezi kuuliza agenda za vyama vya upinzani kama havikutani na wanachama wao. Mtoa uzi ulitaka agenda za vyama vya upinzani wakazisome ili wewe na unaowatumia mzisikie pale maelezo? Kwani hizo agenda za ifisadi toka vyama vya upinzani ambayo imepotea wewe ulizisika kupitia forums gan by then? Naogopa yawezekana wenye agenda ndo wamepoteza. Unatwambiaje kuhusu kusimamishwa/kutumbuliwa kwa bwana mramba kwa miezi 12 huku akila stahiki zote za ukurugenzi na leo karudishwa tanesco?
 
KAKOBE ALITUMWA? MBONA WAPINZANI WAMEFANYA MASHAMBULIZI YAKE DHIDI YA RAIS MAGUFULI KUWA AGENDA ZAO? WAMEKOSA AGENDA ZA KUJISHINDANISHA NA SERIKALI YA CCM KWA WANANCHI?

Tangu Kiongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(FGBF), Zacharia Kakobe atumie Madhabahu kumshambulia rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. John Pombe Magufuli, Wanasiasa wa Upinzaji wamedandia shutuma za Kakobe na kuzifanya agenda zao kuendeleza kwa kasi ya ajabu porojo za kutaka kuwafanya viziwi na vipofu Watanzania waache kuona na kusikia juhudi za Serikali chini ya Rais Mahiri kabisa, JPM za kuijenga Tanzania mpya na badala yake waamini uzushi, porojo na vimaneno maneno vya hovyo hovyo kwamba rais akatubu, sijui rais hakosolewi na upuuzi mwingi tu.

Kwa jicho la tatu unaweza kuamini kuwa yale hayakuwa maneno ya KAKOBE bali alilipwa na kutumwa kufanyakazi ya wanasiasa ambao kupitia kwa viongozi wa dini aina ya Kakobe wanaweza kupambana na serikali ambayo kimsingi imeonesha kuzikonga nyoyo za wananchi wake kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.

Hivi Unawezaje kutofautisha maneno ya Kakobe na porojo za wanasiasa kwamba kuna utawala wa kidikteta, kuminya demokrasia, kutokubali kukosolewa? Hivi hayo madhaifu ya Serikali yanaonekana machoni mwa wana siasa na akina Kakobe? Wanachi wa kawaida ambao kiu yao ya siku nyingi ya kutaka kuona watoto wao wanasoma bure, madawa yanapatikwpana mahospitalini, madini yao, gesi yao, Mafuta yao hayaibiwi na wajanja, Barabara za juu na chini zinajengwa, Reli ya kisasa inajengwa, bei nzuri ya mazao, urasimu katika kupatikana kwa pembejeo na mbolea unatokomezwa, wanafunzi wanapata mikopo kwa wakati , wao hawana macho?

Najiuliza tu:

Kwanini upinzani unajipa kilema cha kujimaliza kwa hoja na mbinu nyepesi nyepesi sana kiasi hiki kupambana na Serikali mahiri kama hii ya awamu ya tano? Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 upinzani utachomoka kweli kwa hoja za akina Kakobe kweli? Eti serikali haikosoleki, kweli? Mwananchi apigie kura upinzani kwa sababu hiyo tu? Sawa haikosoleki lakini tuna maji, tunapata mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati, watoto wetu wanasoma bure na wale wa vyuo vikuu wanapata mikopo kwa wakati, madawa yako hospitalini n.k. Hivi wananchi wakiwapa hizo kama sababu za kumchagua tena JPM mtakuwa na la kuwashawishi tena?

Wapinzani mnapoteza muda kukwapua mashambulizi ya akina kakobe na kuyafanya agenda zenu , mtaumbuka, muwe wabunifu wa hoja nzito za kwenda nazo kwa wananchi siyo hizi za kuwanunua nunua wenye njaa kama akina Kakobe na kuanza kuzikomalia.

Mnachekesha sana. Hivi mnategemea Mshinde uchaguzi kupitia waumini wa Kakobe ambao hata kanisa lake pale Mwenge pamoja na kuwa dogo lililojibananisha pale njiani halijai? BAVICHA mmoja akasema CCM msimpuuze Kakobe ana waumini wapiga kura mil.10. Ujinga mtupu. Watanzania hatujafikia mil.50. Watoto ambao hawajafikia umri wa kupiga kura ndiyo wengi, wanaojiandikisha kupiga kura ni wengi lakini wanaojitokeza kupiga kura hata mil.10 hawafiki. Ina maana wote wanaokwenda kupiga kura wote wanatoka kwa Kakobe? Hizi ni akili za Makarai ya Zege kwelikweli.

Waumini wa Kakobe wenyewe ni kama watu waliokata tamaa ya maisha sijadhani kama wanakuwa na hata wazo la kupiga kura. Ni wale wanaokwenda kuvuliwa mikufu ya dhahabu na Kakobe na kuiuza kwa ajili ya kujipatia fedha huku akiwahadaa kwamba vitu hivyo vya thamani ni chukizo kwa Mungu, hawa watapata muda wa kupiga kura? Ni wale ambao wanaabudu kwa kusikiliza ujumbe wa Mungu wao (KAKOBE) redioni maana akisafiri hakuna ruhusa ya mtu mwingine kuendesha ibada. Hawa wanapiga kura kweli?

Wapinzani jitafakarini sana, waaseni vijana wenu mitandaoni wabuni mbinu mpya za kupambana na serikali ili kupitia kwao siku moja mshike dola. Hamuezi kushika dola kwa Hoja za akina Kakobe.
Maneno mengi kumbe yote pumba tu kama rais wako. Yaani ukiwa ccm akili upotea
 
Kakobe wala hajaanza leo kuropoka ovyo dhidi ya serikali na mamlaka, hasa baada ya kanisa lake kuingia katika migogoro. Anadhani kuingia siasani kutanusuru jina lake katika dini. Anazidi kupotea na mwisho wake hautakuwa mzuri. Mtaniambia
 
Mzee kweli kitubio kinamuhusu. Kwa kweli Kakobe kapanikisha watu, naona hata kauli za niombeeni makanisani na miskitini zitapungua sasa!!.

Kama hii track ya kutuba itaendelea mpaka jtatu, lazima mzee wa kutubu anadamkia bandari kwenda kukamata makontena ya magari. ili kuanzisha new kiki.

Ila KUTUBU MUHIMU.
 
Kakobe wala hajaanza leo kuropoka ovyo dhidi ya serikali na mamlaka, hasa baada ya kanisa lake kuingia katika migogoro. Anadhani kuingia siasani kutanusuru jina lake katika dini. Anazidi kupotea na mwisho wake hautakuwa mzuri. Mtaniambia
Kwa taarifa yako tu huyu ndugu kakobe yupo tangu kipindi cha nyerere na hizo harakati za kutubisha watu ameanza muda mrefu sana. Kama kupotea alitakiwa apotee tangu hata wewe hujazaliwa.

Nyie pambaneni na kutubia chenu tu kwasasa
 
Kakobe wala hajaanza leo kuropoka ovyo dhidi ya serikali na mamlaka, hasa baada ya kanisa lake kuingia katika migogoro. Anadhani kuingia siasani kutanusuru jina lake katika dini. Anazidi kupotea na mwisho wake hautakuwa mzuri. Mtaniambia
Halafu haya haya makarai yatamkimbia na kumtelekeza.
 
Back
Top Bottom