Pole sana kwa mkasa wa ndugu zako.
Nani mkubwa kati yako wewe na hao kaka zako? Hili litasaidia tu kuchagua njia ya kuongea nao.
Huna namna zaidi ya kuongea nao juu ya hali hiyo hasa huyo anayeishi naye nyumba moja. Usipofanya hivyo kuna hatari zaidi ya hiyo inaweza kufuata. Fikiria huyo kaka yako mkewe hatupo kwa sasa,mganga naye hakai sana hapo. Tatizo ni huu uhuru walionao unaweza kufanya mapenzi yakakolea zaidi,badala ya kujiiba wakahisi wana haki ya kufanya hivyo.
Pia,kwa tabia aliyonayo huyo dada ni kwamba hakuna usalama hapo,kama siyo leo ni kesho.
Si vema kupoteza ndugu kwa tatizo unaloweza kulitatua. Wakikulaumu ni kwa muda tu,mapenzi yakiwaisha rohoni kinyongo kitaisha pia. Ila jiandae kwa lawama kwamba unawafuatilia(si kosa kwa ndugu unayemjali).
Ukikaa kimya pia,ipo siku mmoja atakulilia kwanini hukusema ilihali unajua.
POLE