Midekoo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2015
- 47,775
- 257,516
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,
Kwakweli niko njia panda mimi kama dada au mama wa familia nimeshindwa kulitatua, nimeshindwa kumshirikisha mtu yoyote hata ubavu wangu wa pili nimeshindwa kumshirikisha naona aibu nitawavua nguo kaka zangu ila humu naona ni mahala sahihi naweza kupata mwanga kidogo.
Picha linaanza hivi, hapa mjini tunakibanda chetu cha urithi familia tukaamua akae mama pamoja na kaka mkubwa na familia yake uwani kuna vyumba vitatu yupo mpangaji kutokana na changamoto za ndoa kaka na mke wake kwa sasa wana mgogoro wa ndoa yao mke amerudi kwao kwa muda.
Huyu mpangaji yeye anaishi na mke wake lakini yeye ni mganga wa kienyeji shughuli zake anafanyia Arusha pale kabaki mke wake tu.
Kwa mara ya kwanza alivohamia huyu mke wa mganga alitongozwa na mtoto wa jirani akampa taarifa mume wake, kilichotokea mganga alimpigia simu bi mkubwa, yule bwana akatoa mkwara mzito sana, kwa yoyote atakaye toka na mke wake litakalomkuta asije akajuta baadae hili likapita.
Sasa huyu dada kwa kifupi alitoa tu taarifa kwa mumewe kujikosha kumbe kiwembe ukimpa safari tatu na elfu kumi unajisevia vya kutosha mtaani wauza magenge, wauza mabucha, bodaboda wanajisevia.
Sasa miezi kazaa nina kaka angu mwingine makazi yake ni nje ya Dar alikuja mapumziko kumuona mama kilichotokea huyu dada alitembea nae sikujua kama aliijua tabia yake ila ndio hivyo ila muda wa mapumziko ulipoisha aliondoka.
Sasa hivi nimepewa taarifa tena kaka mkubwa ameanza kutembea nae na mchezo wote unafanyika ndani ya nyumba wakati wa usiku kwenye chumba cha huyo dada. Huyu dada mpangaji ana urafiki na mtoto wa mama angu mdogo anaishi hapo nyumbani kwahiyo kila analofanya anamwambia huyu ndugu yangu ndipo habari nazipata
Maswali nayojiuliza je kaka zangu wanajijua wameshashare mapenzi kwa mwanamke mmoja?
Je, kama huyu dada ameathirika inakuwaje?
Je, mume wake akifahamu atafanya nini?
Nimwambie mama mzazi kinachoendelea? (Baba amefariki)
Inaniuma ufuska unafanyika ndani ya nyumba cha kufanya sina kaka zangu nawaona kama baba zangu na wao wananiona mama wa familia sijui pakuwaanzia kuwaeleza hili jambo.
Na uwezo wa kuwashawishi ndugu zangu tumpe notice je nikiulizwa chanzo nini? Kwenye kulipa kodi wako vizuri hawasumbui.
Naombeni ushauri nifanyeje jamani roho naniuma sana japo kuna watu watanishangaa kwanini niumie ila ndio hivyo binadamu tuko tofauti.