kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,809
Tundu Lissu, mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chadema, ni mwanasheria nguli sana mwenye asili ya kutopenda kushindwa na kung'ang'ania jambo, alipigwa risasi nyingi mwilini mwake lakini Mungu amemsaidia amerudi akiwa hai japo amepata hitilafu kadhaa katika mwili wake.
Najaribu kumuangalia huyu ndugu kwa jicho la tatu, atakuwa tayari kweli kuwa mtulivu pale matokeo ya urais yatakapotangazwa na matokeo kutokuwa upande wake? Hivi ataweza kweli kuwa na kifua kama cha Lowassa mwaka 2015? Tanzania itarudi tena moja baada ya uchaguzi wa mwaka huu? Najiuliza sana haya maswali, napatwa na hofu kidogo.
Mbaya zaidi nikiangalia upande wa pili yaani CCM, mgombea wao Magufuli naye si mtu wa diplomasia, kipindi Lissu labda akiamua kupinga matokeo endapo akishindwa, Magufuli atakuwa na kifua cha kuvumilia na kuacha upepo upite? Maana nayeye ni mtu wa hasira na maamuzi ya haraka, hataiingiza nchi kwenye machafuko?
Magufuli na Lissu ni kama wana uadui mkubwa, na hawa ndio wanaogombea katika vyama vikubwa vya siasa hapa Tanzania, na wote ni watu wenye maamuzi ya haraka na wenye ujasiri naweza sema kupita kiasi, na ni kama hawanaga asili ya uoga, na wapo tayari kwa lolote kuliko waonekane dhaifu,hawa jamaa watatuvusha salama kweli??
Najaribu kujiuliza, BAADA YA UCHAGUZI HUU TANZANIA TUTATUDI KUWA WAMOJA TENA KAMA CHAGUZI ZILIZOPITA??