Kaka feki wa Askofu Gwajima ajitokeza

Kaka feki wa Askofu Gwajima ajitokeza

Hapo mtànzania ushike moyo. Katika skendo hii ya Gwajima, Makonda ka-exhibit U-CCM zaidi kuliko U-DC. It's a grand shame!
 
Katika sakata linaloendelea katika vyombo vya habari kwa muda wa wiki sasa, mapya yaendelea kujitokeza likiwamo la mtu ambaye alijitambulisha kuwa kaka na msemaji wa familia ya askofu huyo, lakini chanzo hiki kimebaini kuwa mtu huyo ni feki.

Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Methusela Gwajima na kujiita ni kaka na msemaji wa familia ya Gwajima chanzo hiki kimegundua si kweli na kwenda mbali zaidi kumtafuta mtu ambaye ni wa familia ya Gwajima (jina tunaliuifadhi),mtu huyo aliyetuthibitishia hilo na kutaja majina ya kaka zake na Askofu Gwajima kwa majina ambao ni:-

1. Paul Gwajima
2. Samson Gwajima
3. Faustine Gwajima na
4. Makoye Gwajima

Nilipofuatilia habari za Methusela Gwajima nikabaini mtu huyo ni kada wa CCM na ameshawahi kuwa katibu wa CCM wilaya ya Singida na wilaya ya Nzega kwa nyakati tofauti na sasa anafanya kazi kama informer wa usalama wa taifa (TISS) na anaishi Sikansika karibu na mitambo ya IPTL.

Aidha chanzo changu cha habari kimebainisha kuwa Kaka huyo feki aliwahi kupatwa na maradhi ya akili na kuwa alichofanya ni tabia ya kuendelea kuropoka ropoka ambayo pia inadaiwa ni moja kati ya dalili za maradhi hayo ya mtindio wa ubongo.

Chanzo changu cha habari kilichojitambulisha kama mmoja wa wanafamilia halisi wa familia ya Askofu Gwajima alimkana mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Methusela Gwajima na kusema familia imesikitishwa sana na kauli yake na kumuonya kamwe asithubutu kutumika kwa lolote kwa habari ya familia ya Askofu Gwajima.

Huyu methucela ni tapeli mmoja anapenda sana kukaa kwenye bar za maeneo ya Mbezi Beach Africana haswa T square na Nguruko. Akiona watu ni mwepesi wa kuwazoea haswa wakienda wanawake huwa anajipendekeza.
 
Umepata shida yote hiyo ya kubadili hata jina ili uje na huu uzi?
Ungesema akina Gwajima ni wa kutoka nje ya tz ningekuelewa,
tz hatuna utamaduni wa kutukana mtu aliyekuzidi umri hata angekufanyia jambo gani.

Nape na Makonda wanafahamu somo hili?
 
Analazimisha undugu na Gwajima, pole wengi kama yeye wanakuja
Kinachonishangaza ni kuwa Tanzania tuna utaratibu mzuri sana,kwamba kila familia ina msemaji ni bahati mbaya sana msemaji wa familia yetu simfahamu labda muda ukifika naye atajitokeza...vipi wewe msemaji wenu unamfaham au ni wewe.
 
Kinachonishangaza ni kuwa Tanzania tuna utaratibu mzuri sana,kwamba kila familia ina msemaji ni bahati mbaya sana msemaji wa familia yetu simfahamu labda muda ukifika naye atajitokeza...vipi wewe msemaji wenu unamfaham au ni wewe.

Duh! Hata mie nilikuwa sijawahi kuwaza hilo! Ngoja nitafute nimjue msemaji wa familia yetu.
 
Daaaa aiseee kumbe namimi nijitangaze mdogo wake Gwajima ili niwe maarufu maana sasa hivi kila mtu ndugu yake Gwajima...hahahahahahahahah.........Kweli Gwajima ndio habari ya mjini ona sasa mtu mzima kumbe ni kada wa CCM na ameumbuka daa pole mkuu kwa kuaibishwa.......unatuzuga watanzania.......

Sasa kama ana tatizo la akili halafunni TISS si atakuwa anatoa habari ambazo si sahihi? Kama.anafahamika hivyo basi akamatwe kwa kusema uongo.
 
kumbe ndugu yake gwajima aliugua ?. Sasa napata picha hata askofu wetu ayuko salama maana hilo ni tatizo la kifamilia

Bila shaka na wewe unaumwa akili. Umeambiwanhuuo ndugu feki ambaye ni TISS ndo mgonjwa. Sasa umepost nini hapa? Uliishia darasa la ngapi?
 
Umepata shida yote hiyo ya kubadili hata jina ili uje na huu uzi?
Ungesema akina Gwajima ni wa kutoka nje ya tz ningekuelewa,
tz hatuna utamaduni wa kutukana mtu aliyekuzidi umri hata angekufanyia jambo gani.

Hivi huyu ndio yule?
 
Kwa ufupi hii habari ilipotoshwa Kwa makusudi kuficha ukweli wa jambo hili ! Mimi si Kaka yake Bali ni mdogo wake kwa maana ya kuwa Baba yangu mimi methusela na Baba yake mchungaji Josephat ni mtu na mdogo wake, Baba Mmoja na mama mmoja na bahati nzuri wazazi wetu wote Mzee Stiven Gwajima na Mzee Mathias Gwajima wote wapo hai na tunaishi nao hapa Dsm ! Ni kweli Kabisa ya kuwa Mimi Kwa niaba ya familia yangu niliongea na waandishi wa habari kulaani na kukemea ! Kwa ufupi hatukupenda namna ambavyo mtu anayejiita mchungaji kuporomosha matusi Kwa kiwango hicho ambacho ni kinyume na tamaduni zetu sisi Watanzania ! Kwa sababu jambo hili alilifanya publicaly nasi hatukuona sababu ya Kwa nini tusimukemee publicaly Ili kuweka record sahihi ! Bahati nzuri sisi wote tunatumia majina ya Gwajima hivyo ilikuwa ni muhimu sana kwetu kujipambanua ! Kwa hiyo hayo mengine yaliyopindishwa ni siasa Lkn ukweli daima utasimama na ipo siku moja Watanzania watakuja kujua yaliyo nyuma ya pazia.
 
Back
Top Bottom