Kaini alipata wapi mke wake?

Kaini alipata wapi mke wake?

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
33,735
Reaction score
55,384
HOJA YA MSINGI

“Ikiwa Adamu na Hawa walikuwa na wana wawili, Kaini na Abeli, na baadae Seth, Je, mke wa Kaini alitoka wapi?”
Biblia ina habari za kutosha kujibu swali hilo kwa njia inayofaa, na kwenye hii mada tutajibu hili swali linalo wachanga sana watu.
MUKTASARI:
Katika Mwanzo sura ya 3 na ya 4 tunapata habari zifuatazo:

(1) Hawa alikuwa “mama ya kila mtu anayeishi.”

(2) Muda fulani ulipita kuanzia wakati Kaini alipozaliwa mpaka wakati alipotoa dhabihu ambayo ilikataliwa na Mungu.

(3) Baada ya kufukuzwa na kuwa “mwenye kutanga-tanga na mkimbizi,” Kaini alikuwa na wasiwasi kwamba huenda ‘mtu yeyote akakutana naye’ na kujaribu kumuua. [Angalia hoja hapa "Kaini anaogopa kuuwawa na watu wengine"] Hapa panaonyesha kuwa Kaini alikuwa na ndugu wengine.

(4) Mungu aliweka ishara ya kumlinda Kaini, jambo lililoonyesha kwamba ndugu au dada zake, au watu wengine wa ukoo wangejaribu kumuua. Kumbe basi Kaini alikuwa na ndugu wengine zaidi ya Abel na Seth.

(5) “Baadaye” Kaini alilala na mke wake “katika nchi ya Ukimbizi.”—Mwanzo 3:20; 4:3, 12, 14-17.

Naomba majibu tafadhari.
 
Nahisi Ni kwa sababu biblia inataja vizazi vya watu kwa kupitia watoto wa kiume mfano Ni :Adam kumzaa kain,Abel na Seth so hii haimaanishi kuwa hao waliotajwa ndio peke yao tu walizaliwa na ADAM NA HAWA ukute Kain hata hakuwa wakwanza kuzaliwa kwa Hawa Bali waeza kuta walizaliwa wa kike wengi alafu yeye Ndo akafatia na kwa kuwa biblia kuhesabu watu ilikuwa inahesabu wanaume tu peke yao labda ndio maana
 
Sawa
 
Nilishwahi uliza swali hili kwa mchungaji wangu mmoja na alinipa majibu haya.

1. Biblia tunayotumia haina rekodi ya kila kitu kilichotokea mwanzo, yaani siyo vyote viliandikwa na inasemekana kuna biblia ambayo ina record ya yote yaliyotokea mwanzo ( binafsi sijawahi kuiona ).

2. Matukio ya kwenye Bible yalikuwa yanaandikwa baada ya kupita muda fulani, yaani utaratibu wa kukusanya mistari ilikuwa ikifanyika ambapo kuna mistari ilibeba rekodi za miaka kadhaa mpaka mstari mwingine kutokea.

Kwa mfano hilo la Kaini, haijulikani ni baada ya miaka mingapi tukio hilo lilitokea na ndani ya huo muda Je, Adam na Hawa hawakufanikiwa kupata watoto wengine ? Ambao nao walitapakaa maeneo tofautitofauti.

3. Kupitia sababu hiyo ya pili ndipo hapo Kaini alipata mke ambaye inaonekana alikuwa ndugu yake either wa damu au alikuwa ndugu yake na ndugu zake wa damu.

Nilimuuliza mchungaji, kwanini sasa kwasasa mtu kumuoa dada yake au ndugu yake ni dhambi ilihali hapo zamani Kaini aliweza kufanya hivyo??

Alinipa jibu hili:

Kwa kipindi kile Mungu aliruhusu iwe hivyo ili watu waendelee kuzaliana na kuijaza dunia hivyo haikuwa dhambi tofauti na inavyotafsirika leo.

Baada ya kunipa ufafanuzi huo nilikuwa na maswali mengi sana ila nilimuaga mchungaji ili nisijeibua maswali yasiyokuwa na majibu
 
Soma Biblia vizuri, ukishindwa jaribu kuongea na viongozi wako wa dini.

Changamoto ipo ktk usomaji wako, na pia kuna changamoto ya kimapokeo na lugha yetu adhimu kutokuwa na misamiati ya kutosha.

Adamu na Eva walikuwa kama reference point ya biblia, watu wengine wanaozungumziwa na Kaini hawakuwa ndugu zake.
 
Sasa kwa nini watupatie biblia ambayo haijakamilika kwa mafundisho yote?
Mkuu ni maswali ambayo niliona kupata majibu ya uhakika isingekuwa rahisi maana hata maisha ya Yesu Biblia inaonyesha kuzaliwa, kisha maisha yake akiwa na umri wa miaka 12 kisha maisha yake kuelekea kusulubiwa. Kuna miaka ya katikati ambayo hatukuelezwa alikuwa akiishi vipi na aliyokuwa anayafanya.
 
Sawa mkuu
 
Adamu aliishi miaka 900 na ushee. Katika muda huo alizaa watoto kibao. Familia ya Yakobo ilikaa Misri miaka 400 na wakatoka watu 2m.

Sasa fikiria Kaini labda alioa miaka 500 baada ya kumuua ndugu yake, si alikuta dunia imejaa vitukuu na vituu vya Adamu. Vingine ni vidangaji havijali kuwa wewe ni Kaini au umevipita miaka 460.
 
Hoja fikirishi sana
 
Back
Top Bottom