Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
Kufuatia kukamatwa kwa Dr. Slaa, Lissu Pamoja na Wanachama wengine wa CDM waliokuwa kwenye mkesha wa Amani, Kamanda Mpwapwa jana alishindwa kueleza sababu za jeshi hilo kushindwa kuwachukulia hatua vijana wa CCM, walioandamana na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali licha ya jeshi hilo kuyapiga marufuku."Pamoja na matukio haya kufanana na eneo la tukio kuwa sawa, lakini polisi tunashughulikia kila shauri kulingana na mazingira yake. Kisheria mtu huwezi kutenda kosa kwa sababu mwingine naye ametenda kosa kama lako," alisema Mpwapwa baada ya waandishi kuhoji kwa nini Chadema wamekamatwa kwa kosa linalofanana na lililotendwa na vijana wa CCM ambao hawakuguswa?
Hapa kamanda anadhihirisha kuwa humu nchini CCM wakifanya kosa Sheria si lazima kufuatwa na si lazima hatua kuchukuliwa dhidi ya uhalifu wa wanaCCM. Anataka kuueleza umma kuwa Polisi wapo makini zaidi na makosa ya baadhi ya watu/chama fulani. Kama vivyo ndivyo basi mishahara nayo kwanini msilipwe na CCM??Mbona mnatubagua wakati ni kodi zetu ndizo zinazowapa maisha?? Hivi utendaji huu wa kipuuzi kabisa utaisha lini????Kwanini sheria za nchi zinawabana watu au kikundi cha watu wachache tu???Hii nchi kweli inafuata utawala wa sheria au ni ushenzi mtupu??
Source Mwananchi 09/11/2011