Kailima Ramadhan: Uchaguzi 2015 ulikuwa huru na wa haki, CHADEMA imeshindwa kihalali! Hakuna upendeleo kwa CCM, NEC ni Tume huru

Kailima Ramadhan: Uchaguzi 2015 ulikuwa huru na wa haki, CHADEMA imeshindwa kihalali! Hakuna upendeleo kwa CCM, NEC ni Tume huru

Acha utaahira wewe! Una ushahidi wa kuonyesha Chadema imepeleka malalamiko kwa Mange? Usijidhalilishe kiasi hicho mbele ya kadamnasi!!!

Hata kama Chadema haijapeleka malalamiko haiondoi ukweli kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki.

Na wewe kwa ujuha wako unadhani hicho kitengo cha dikteta uchwara cha wizi wa kura kitatenda haki kwa Chadema?

Kama huna la maana la kuandika kaa kimya badala ya kufanya ubaradhuli kwenye issues za maana.
Mkuu hata utoke povu kiasi gani kubali ndani ya Chadema kunaombwe la uongozi...
 
Chumba cha kupiga kura kina sheria zake ukikiuka ukidundwa virungu na kuswekwa Ndani hutakiwi kupiga yowe

Uliambiwa wamepiga mayowe??Usipende kushabikia upuuzi,tuchuane kwa haki,weka fair ground watu wapige kura kwa haki,leo huyo Diwani hata akitembea anaona haya maana hakuchaguliwa kwa HAKI.Akifikiria jinsi RAIA walivyovuja damu ili ashinde hawezi kuwa na amani hata kidogo,Utakuja kuniambia tu.
 
Si rahisi nchi inayotawaliwa na chama kimoja tangia uhuru ikafanya uchaguzi wa huru na wa haki.Na ni ngumu sana kukiondosha chama hicho madarakani kwa kura
 
Akili yako ya tope kama huyo Kailima tu,hivi wale waliopigwa na kuwekwa rumande jana Arusha walifanya fujo ipi?Au kwa sababu ya kukataa kutoka kwenye chumba cha kuhesabia kurai.
usiangalie idadi ya virungu alivyotwanga kila eneo mwilini na mateke aliyopigwa huyo MTU mmoja wakati wengine walio wengi wakiendelea kupiga kura peaceful .Huyo yaliyomkuta hayaathiri kura sababu wapiga kura hawakususa waliendelea na upigaji kura wakimwacha aendelee kupigana na hali yake
 
Mkuu Mkwepa Kodi, kama sheria, taratibu na kanuni zinakutaka ujaze fomu ya malalamiko ili iende NEC, WEWE UNALALAMIKIA KWENYE MEDIA TUU BILA KUJAZA FOMU, nec WANAKUWA WAKO RIGHT, HAKUNA ALIYELALAMIKA.

Ila hili la umuhimu wa elimu kwa mpiga kura nimelizungumza, na mimi nitajitolea kutoa elimu hiyo bure.

Paskali

Mkubwa.
Naona taratibu unaelekea kutoka kwenye misingi yetu. nakuomba urejee kwenye misingi ya ukweli na uwazi,yaliyojiri na maoni ya wahusika.(sijatazama kipindi,najibu kupitia post yako hii)

Hya masuala ya kufunika funika mambo kwa kigezo cha 'hawakuripoti' rasmi yanaweza kusababisha vurugu na machafuko nchini na hakika waandishi wa habari tunaweza kuwa wa kwanza kuwajibishwa.

Kwa mfano Polepole ameeleza namna walivyojerehuiwa na kufanyiwa fujo,CDM hivyo hivyo,CUF hivyo na ACT lakini wewe kama 'mtu wa kati' hupaswi kuwa kasuku kisa Kailima kasema, just tell us the truth.,what happened? .Vinginevyo hicho kipindi ni promo tu.

Kama ulipanga kutuletea yaliyojiri basi ilitakiwa uende kwa Kailima 'Kubalance' tu kusudi watazamaji ndiyo waamue baada ya kutazama yaliyojiri kwenye 'ground' na tamko hilo la Kailima.

M.Byabato
 
Tatizo la upinzani nchi hii hawan uwezo wakufikiria
wao wanaridhika na Vibendera wa mitandaoni
tena wengi wao wakiwa na Id Fake!
Wanashindwa kuandaa Ajenda na Hoja
kwa kubweteka na Vibendera hawa!

Akili yakujiongeza hawana mwisho wao ni kulialia
mnamtegemea Mange Inst
apost upumbavu uwapatie Viti vya udiwani
!!
Mjaribu kujikosoa kàbla ya kumkosoa jirani yako
 
Kwa ujuha wako unadhani mie natoa povu. Angekuwa ndugu yako wa karibu kapigwa panga na kufa au kujeruhiwa usingeandika huu upuuzi wako. Chadema kuna ombwe ka uchaguzi si ndiyo vizuri MACCM watumie OMBWE hili ka uongozi kuhakikisha chaguzi ni huru na haki ili washinde kihalali badala ya kutumia wizi, hila, mapanga, visu na bunduki kupata ushindi haramu!?

Achana na kuandika upuuzi humu!!!

Mkuu hata utoke povu kiasi gani kubali ndani ya Chadema kunaombwe la uongozi...
 
Narudia tena uchaguzi haukuwa huru na haki sehemu nyingi tu hata kama Chadema wangeamua kujitoa.

Kwenye uchaguzi haramu wa marudio Zanzibar CUF walijitoa kwenye uchaguzi ule. Hebu tuambie CUF walifaidika vipi kwa kuamua kujitoa?

Hata kama ni kutafuta TEUZI lakini si kwa kujitoa ufahamu kiasi hiki na kutetea wizi, dhuluma na udhalimu wa mchana kweupe.

Shida yenu hamtaki kukosolewa
hamtafika kokote
 
Kwa ujuha wako unadhani mie natoa povu. Angekuwa ndugu yako wa karibu kapigwa panga na kufa au kujeruhiwa usingeandika huu upuuzi wako. Chadema kuna ombwe ka uchaguzi si ndiyo vizuri MACCM watumie OMBWE hili ka uongozi kuhakikisha chaguzi ni huru na haki ili washinde kihalali badala ya kutumia wizi, hila, mapanga, visu na bunduki kupata ushindi haramu!?

Achana na kuandika upuuzi humu!!!
Wacha kupanic
Aligombea Babako?
 
Wewe utakuwa na uvumilivu kama Baba yako angekuwa mmoja wa waliouawa au kuumizwa kwa mapanga kisa tu uchaguzi wa Madiwani!?

Hebu tia akili kichwani badala ya kukurupuka. Walioumizwa na kuuawa ni Watanzania wenzio weka utu japo kidogo kuona kama walistahili kuumizwa au kuuawa huku wakiwa hawana hatia yoyote ile.
Chadema ndiyo.wanahitaji.kutia akili,Afrika dola ndiyo yenye nguvu watu maneno tu,Watu walijisahau wakadhani wako ulaya unapiga watu unatusi watu kikwete anasema waacheni,someni.nyakati ukileta fujo siyo hao wachache unaosema wewe,itakuwa kama kenya 2020 viongozi wa upinzani wasipowaambia mtulie na muwe na siasa za kistaarabu,chadema ndiyo wanaanzaga kupiga watu wakijidanganya nguvu ya uma siyo safari hii ndugu yangu,ukiambiwa usitoke kaa nyumbani.
 
Wewe Mayalla hebu acha ujinga!!! Hukuziona picha za majeruhi walioumizwa kwenye sehemu mbali mbali nchini!? Hukusikia yaliyojiri kuhusu wasimamizi wa upinzani kukamatwa au kutolewa ndani ya vituo ili kuruhusu wizi kufanyika?

Utumie akili japo kidogo badala ya kukurupuka ili kutafuta TEUZI.


MONDAY , 27TH NOV , 2017
NA MELLANIA JULIUS
Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia CHADEMA Jacob Boniface ambaye jana alishikiliwa na polisi, ameweka wazi sababu ambayo jana ilimsababishia kukamatwa na jeshi la Polisi na kulala ndani, huku uchaguzi ukiendelea.




case.jpg

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Meya Jacob amesema yeye alikuwa ni msimamizi wa vituo vya kupigia kura ambayo ipo kisheria, lakini baada ya muda alishangaa kuona polisi wanakuja kumkamata kwa tuhuma ambazo hazikuwa za kwlei.

“Nilikuwa nasimamia uchaguzi kama msimamizi wa uchaguzi wa chama changu, nikiwa kituoni nashangaa kuona nakuja kukamatwa na polisi, nilipofika kule wakaniambia kuwa wamepata taarifa kwamba nimejipanga kufanya vurugu na wenzangu, kitu ambacho sio kweli”, amesema Jacob Boniface.

Meya huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi machachari wa CHADEMA amesema mpaka sasa hajajua hatma yake kama anapelekwa mahakamani au la, kwani aliachiwa huru majira ya saa saba usiku baada ya kulipa dhamana, huku uchaguzi ukiwa umeshakwisha.
Sasa we TANAPA unamtusi Pascal kwa kosa lipi hasa?! Hukutaka amuhoji mkurugenzi tume ya uchaguzi kujua nini kimejiri (kwa mujibu wa tume) kote nchini?!
 
Tume ya Uchaguzi imesema haijapokea barua rasmi ya malalamiko kutoka chama chochote kile..

Sasa Chadema badala ya kupeleka malalamiko NEC wanampelekea Da'Mange....upuuzi mtupu.
Nawewe acha ujinga, kwa walizopokea katika chaguzi nyingine walifanya nini? Mambo mengine kwa akili ya kawaida unapata majibu. Sina chama ila CCM iache wizi na uhalifu inaotenda kwa kupitia jeshi la polisi kwa ku harasss wapinzani.
 
Una ushahidi wa kuonyesha Chadema imepeleka malalamiko kwa Mange? Usijidhalilishe kiasi hicho mbele ya kadamnasi!!!

Hata kama Chadema haijapeleka malalamiko haiondoi ukweli kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki.

Na wewe kwa ujuha wako unadhani hicho kitengo cha dikteta uchwara cha wizi wa kura kitatenda haki kwa Chadema?

Kama huna la maana la kuandika kaa kimya badala ya kufanya ubaradhuli kwenye issues za maana.
Kweli kuna matukio mabovu yaliyoathiri uhuru wa uchaguzi lkn ni kwa kiwango gani? Ndio chaguzi zote duniani zinapimwa kwa asilimia kwa sababu kutokuwepo kwa dosari hata moja ni ngumu sana. Vurugu zilizotokea kwenye uchaguzi huu zimepewa kiwango cha 5% ambazo hazijaathiri uchaguzi wa kata zote.
 
Back
Top Bottom