Wanabodi,
Its high time vyama tuanze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, tukubali kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani, badala ya kutafuta visingizio.
Kama hali ya uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania, jee hali itakuwaje uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye sanduku la kura, kuna hatari ya CCM, kuyarejesha majimbo yote ya upinzani mwaka 2020, hivyo Tanzania kuanza safari ya kuelekea kuwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini ukweli tunaelekea kuwa nchi ya chama kimoja.
NB. Kipindi kikiwa tayari, nitakipandisha humu umsikilize mwenyewe.
Wasalaam.
Paskali