Kahawa ya Afrika Inazidi Kupata Umaarufu nchini China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Na Tom Wanjala

Ripoti ya maonyesho ya pili ya kibiashara kati ya Afrika na China yaliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mwezi Septemba mwaka huu katika mjini Changsha mkoani Hunan, inaonyesha kuwa kahawa kutoka Afrika inazidi kupendwa na wateja wa China.

Afrika ni maarufu duniani kwa kilimo cha kahawa, haswa Ethiopia ambayo huzalisha aina mbalimbali za kahawa inayopendwa na mataifa mengi. Habari hii ya China kuanza kutumia kahawa kutoka Afrika, ni habari njema kwa wakulima wa zao hili, ambao siku za hivi karibuni, wamejikutta katika hali ngumu ya kiuchumi kufuatia makali ya janga la virusi vya Corona.

Tangu janga hili lilipoibuka barani Afrika kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, wakulima wengi wakiwemo wa kahawa walifungiwa mipaka ya kuuza mazao yao kwa mataifa ya nje. Lakini sasa, shughuli zimenaza kurejea tena na huu ni ahueni kubwa kwa wakulima.

1634260489762.png


China imeonyesha nia ya kununua kahawa kwa wingi kutoka Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa mtu mmoja hunywa kahawa vikombe 6.2 kwa mwaka nchini China. Hii ni sawa na jumla ya vikombe vya kahawa bilioni 85 kila mwaka.

Kuongezeka kwa unywaji kahawa nchini China kwa mwaka ni asilimia 16, ikilinganishwa na kiwango cha asilimia 2 cha dunia.

Kutokana na maonyesho ya pili ya kibiashara yaliyofanyika kati ya China na Afrika, imebainika kuwa Afrika ina uwezo wa kupenyeza katika soko kubwa la China, na kuuza kahawa yake. Lei Ting ambaye ni mwanzilishi wa Overseas Home, kampuni ya kichina ambayo inaunganisha biashara kati ya China na Afrika, na mmoja wa wadau katika maonyesho hayo, alisema kuwa kahawa ya Afrika ni ya kiwango cha juu mno, na kuifanya Wachina wengi kuipenda.

‘’Afrika ni moja ya wazalishaji bora wa kahawa nzuri zaidi ulimwenguni. Kuna ishara nzuri ya ushirikiano mwema wa kibiashara kati ya Afrika na China, haswa katika sekta ya zao la kahawa. Kuna wakulima wakubwa wa kahawa Afrika ambao wamekosa soko kwa muda mrefu. Sasa wana nafasi nzuri kuuza zao lao katika soko la China,’’ alieleza bwana Ting.

Washiriki 40 wa kuzalisha kahawa kutoka Afrika walipata fursa ya kutangaza kahawa yao kwenye maonyesho ya pili ya kibiashara kati ya China na Afrika, kwa kuweka vibanda, kwa ufadhili wa kampuni ya Overseas Home.

‘’Kutokana na janga la virusi vya Corona, washiriki hawa hawakuruhusiwa kuja hapa wenyewe. Tulishirikiana nao kwa kusafirisha kahawa yao hadi mji wa Changsha. Tuliwatafutia mawakala kutoka China, ambao waliwasaidia kutangaza kahawa zao kwenye maonyesho hayo,’’ alisema bwana Ting.

Fridah Mbaya, ni mkulima wa kahawa kutoka kaunti ya Meru nchini Kenya. Anatarajia kusafarisha kahawa yake nchini China wakati wowote mwaka huu. Mbaya anasema sababu kuu ya kahawa ya Afrika kupendwa nchini China ni kutokana na namna inavyovunwa na kutayarishwa. Anadokeza kuwa kahawa ya Afrika haikaushwi kwa mashine, ila kwa jua. Hii inaisaidia kahawa kutunza uhalisia wake, ambao unaeza ukapotea endapo itawekwa kwenye miale ya nguvu za umeme.

‘’Sababu nyingine ambayo imechangia kahawa ya Afrika kupendwa sana duniani na haswa China, ni kutokana na namna inavyovunwa shambani. Wakulima wengi wa Afrika hawatumii mashine kuvuna kahawa, ila inavunwa kwa mikono, hatua ambayo inahakikisha kuwa kahawa haina uchafu. Hii inasaidia sana katika kuhakikisha kuwa kahawa ni safi bila magugu yoyote,’’ alisema bi Mbaya.

Habari ya uwepo wa soko kubwa la kahawa nchini China imewafurahisha sana wakulima wengi wa zao hilo kutoka Afrika. Bi Mbaya anasema kwamba kwa miaka mingi wamekuwa waking’ang’ania soko la ulaya na Uarabuni ambalo halijakuwa na faida kubwa.

‘’Tumekuwa tukiuza kahawa yetu kwa bei ya chini sana. Ujio wa China kwenye soko la kahawa, huenda ukabadilisha kila kitu kuhusiana na ukulima na uuzaji wa kahawa. Tunatarajia kwamba tutanufaika na kilimo hiki haswa ikizingatiwa kuwa, China ina soko kubwa sana,’’ aliiambia idhaa ya Kiswahili ya CRI Nairobi.

Ethiopia iliuza tani 6,000 za kahawa kwa China mwaka wa 2020. Kwa mujibu wa bwana Lei Ting, kiwango hiki kinatarajiwa kuongezeka hadi tani 10,000 mwaka huu, na ameyasihi mataifa ya Afrika kuhimiza ushirikiano wa kibiashara kati yao na China.
 
Back
Top Bottom