Kahama: Manispaa isiyo na barabara za lami za mitaa

Kama Mji sio Makao Makuu ya Mkoa hakuna mtu ana habari nao.
Zamani sana miaka sabini Kahama ilikuwa na inapendeza ikiwa na warembo wengi sana. Kuna wakati nilikuwapo Kahama pale akaja marehemu Mbaraka na bendi yake ys Super volcano kupiga muziki kwenye ukumbi fulani ukiitwa community. Wakati huo ndio Mh Jumanne Kishimba alikuwa anaanza biashara angali kijana, na kulikuwa na mfanya bishara mwingine akiitwa Kulwa Salumu ambaye aliwahi kuwa mpiga rhythm wa Morogoro Jazz kabla haijavunjika. Siku hiyo ukumbi ulijaaa warembo wengi sana, halafu Mbaraka akamkaribisha Kulwa Salum kubeba rhythm guitar na kuliporomosha ukumbini. Ulikuwa usiku wa maraha sana. Kwa bahati mbaya sikuwahi kurudi Kahama hadi baada ya 15 nikakuta mji umebadilika sana ingawa nilikuwa dissapointed kuwa ile barabara ya lami kwenda Rwanda ilikuwa imepita pembeni mwa mji; ilionekana kama vile mji umekuwa wa matapeli tapeli tu. Leo ni miaka mingi sana imepita kwa hiyo sijui itakuwaje tena.
 
Kahama ni kijiji kikubwa chenye darasa la saba wengi wenye ukwasi. Kuitwa Manispaa ni kulazimisha kama lilivyo Jiji la Mbeya.... Hata Dar es salaam barabara za mitaani baadhi ni vumbi tupu. 😷
 
Manispaa ya kigoma ujiji pale kigoma wana barabara za mtaani za lami kuliko Ruvuma, njombe, singida, wakati ukiangalia mkoa kama njombe unamapato makubwa sana sana
BILIONI 3.2 ZAIWEZESHA TARURA KUJENGA KILOMITA 51.28 ZA BARABARA MKOANI NJOMBE - Mhe. Ndejembi

Na: James Mwanamyoto (OR-TAMISEMI)

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita katika Mwaka wa Fedha 2022/23 ilitenga bilioni 3.2 zilizoiwezesha TARURA kujenga barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 51.28 mkoani Njombe.

Mhe. Ndejembi amesema hayo akiwa katika Halmashauri ya Mji Makambako, mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza na wakazi wa eneo hilo.

Mhe. Ndejembi amesema, kabla Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani TARURA ilitengewa shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Njombe, na kuongeza kuwa Mhe. Rais aliongeza bajeti iliyofikia shilingi bilioni 3.2 ili kuongeza wigo wa ujenzi wa barabara mkoani humo.

“Mhe. Makamu wa Rais katika kilomita 51.28 za barabara zilizojengwa mkoani Njombe wananchi wa hapa Makambako wamenuifa na kilomita 12 zilizojengwa katika mji huu wa Makambako,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, katika mwaka huu wa fedha 2023/24 Serikali imetenga bilioni 1 kwa ajili ya kujenga barabara za kiwango cha lami ambazo zitawekewa taa katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.

Aidha, Mhe. Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri ya Mji wa Makambako ilipokea zaidi ya shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kitisi.

Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amesema katika kata ya Kitandililo Serikali imeleta milioni 583 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari na inaendelea na ujenzi wa kituo cha afya ambacho kimetengewa milioni 250 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake.
 
Ina maana Kahama wanazidiwa hata na wilaya ya temeke kwa lami hadi uchochoroni kote taa na lami kwa wilaya za Dar angalau temeke wameupiga mwingi
 
Zamani sana miaka sabini Kahama ilikuwa na inapendeza ikiwa na warembo wengi sana. Kuna wakati nilikuwapo Kahama pale akaja marehemu Mbaraka na bendi yake ys Super volcano kupiga muziki kwenye ukumbi fulani ukiitwa community. Wakati huo ndio Mh Jumanne Kishimba alikuwa anaanza biashara angali kijana, na kulikuwa na mfanya bishara mwingine akiitwa Kulwa Salumu ambaye aliwahi kuwa mpiga rhythm wa Morogoro Jazz kabla haijavunjika. Siku hiyo ukumbi ulijaaa warembo wengi sana, halafu Mbaraka akamkaribisha Kulwa Salum kubeba rhythm guitar na kuliporomosha ukumbini. Ulikuwa usiku wa maraha sana. Kwa bahati mbaya sikuwahi kurudi Kahama hadi baada ya 15 nikakuta mji umebadilika sana ingawa nilikuwa dissapointed kuwa ile barabara ya lami kwenda Rwanda ilikuwa imepita pembeni mwa mji; ilionekana kama vile mji umekuwa wa matapeli tapeli tu. Leo ni miaka mingi sana imepita kwa hiyo sijui itakuwaje tena.
Community center.
Nyihogo.
Wakati huo Mji ule ulikuwa mzuri sana.. mdogo ila wenye utaratibu sana.
 
Back
Top Bottom