Kahaba Ajitamba Kula Uroda na Beckham | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kahaba Ajitamba Kula Uroda na Beckham

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Oct 1, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Kahaba Irma Nici
  Kahaba Irma Nici ameendelea kujitamba kuwa alikula uroda na mcheza soka maarufu wa Uingereza, David Beckham ingawa Beckham anajiandaa kufungua kesi ya madai ya fidia kiasi cha dola milioni 16. Pamoja na kwamba wanasheria wa mcheza soka maarufu wa Uingereza, David Beckham anayesakata kabumbu nchini Marekani wako kwenye jitihada za kufungua kesi mahakamani kumdai fidia ya dola milioni 16, kahaba anayedai kutembea na Beckham ameibuka na kutamba ana ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

  Kahaba Irma Nici mwenye asili ya Bosnia amedai kuwa anaweza kuithibitishia mahakama kuwa alilala na nyota huyo wa soka mjini London na mjini New York mnamo mwaka 2007.

  Nici amedai kuwa Beckham ana alama za kipekee kwenye sehemu zake nyeti hivyo ajiandae kuvua suruali yake mahakamani ili kuzithibitisha alama hizo.

  Nici mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akiwakwepa wanasheria wa Beckham na amekuwa akijificha kwenye hoteli mjini New York.

  Beckham mwenye umri wa miaka 35 anamshtaki Nici kutokana na habari iliyotoka kwenye jarida moja la Marekani kuwa Beckham alinunua penzi la kahaba Nici.

  Nici aliliambia jarida hilo kuwa alishea kitanda kimoja na Beckham wakati Beckham alipofanya mapenzi yaliyowahusisha wanawake wawili kwa mpigo. Mwanamke wa pili aliyezungumziwa katika habari hiyo bado hajajulikana.

  Beckham anamshtaki Nici na jarida hilo kwa kuandika habari za kumpakazia kuwa aliisaliti ndoa yake na Victoria Beckham, 36,

  Beckham pia anamshtaki Nici na jarida hilo kwa habari ambayo imemfanya Beckham aonekane aliyatia maisha ya mkewe hatarini kwa kutembea na kahaba.

  Chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Ma Star wengi ni malaya wakubwa haya tena Beckham unatembea na Makahaba kazi kweli ipo Kasheshe kubwa, ndowa yako Beckham itavunjika kama ndowa ya Tiger Wood ( Chuwi wa mbao)
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huko Ulaya sasa W.Rooney, Beckam ,Tiger wood sijui anafatia nani?
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  FL1 Tatizo hawa jamaa wana hela nyingi pia na fame nayo inawachangia sana ukiangalia age aliyonayo rooney na hela aliyonayo utangundua kuna kitu, ukiangalia tiger woods ameanza kuwa maarufu since he was young kwahiyo kila mtu he's looking at you ukiteleza tu kidogo utaandikwa kwenye vyombo vya habari mpaka hata kama kuna jambo ulilifanya mwaka 95 nalo litafichuliwa tu.
   
 4. E=mcsquared

  E=mcsquared JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kasingiziwa; litakuwa limemfanyia kazi siku nyingi mpaka likafahamu ana alama gani kwenye mwili wake!
   
 5. e

  ejogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ooh! anataka kumuharibia huyu jamaa kwa mkewe!
   
 6. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mmmh!
   
Loading...