Kagoma kutoa mtoto aliyekubali kuzalishwa.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagoma kutoa mtoto aliyekubali kuzalishwa....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Leornado, Jan 20, 2011.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nina rafiki yangu huu mwaka wa kumi na sita kaoa ila mkewe wa ndoa bahati mbaya hazai, jamaa yeye hana tatizo. Mkewe kamruhusu baada ya yeye kumwomba azae nje then amchukue kachanga huyo wamlee wao kama mtoto wao. Mtoto kazaliwa nje ya ndoa sasa ana miaka mitatu ila huyu mwanamke pamoja na kuingia mkataba na wanandoa hawa kagoma kumtoa mtoto mwaka wa tatu sasa na ndoa ya watu iko hati hati kuvunjika maana huyu bibie mdogo anawavuruga sana. Nimejaribu kusuluhisha kwa kila namna imeshindikana na kumbembeleza bibie kasema mtoto hatoi. Naombeni mawazo yenu.

  Thanx in advance.
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hata ningekuwa mimi nisingemtoa si ana mama mtoto, cha muhimu baba mtu ni kutoa mahitaji yote kwa mama na mtoto.
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwanza samahani naanza kwanza na wewe, Unamshauri huyo dada amtoe mtoto ake akiwa mdogo hivo? To me sio sawa!! Huyo baba atumie akili za kiume hapo, kama kweli anamtaka mtoto atoe matumizi na amlee mtoto vya kutosha akiwa kwa mama ake.

  Kwa sababu mtoto ameshazaliwa sitakiwi kusema sana, lakini mkataba waliowekeana hawa watu sio mzuri. Mtoto wa binadamu sio kama wa mnyama useme utamtenganisha na mama yake hivi hivi tu.
   
 4. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  yo veeery rite. Kikubwa amhudumie tu mpaka akue
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Yaani hadi sasa haujalala kesho kesi mimi na wewe
   
 6. L

  Leornado JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimewaelewa, sasa kwa nini huyu dada alikubali hiyo dili halafu sasa hivi ameleta matatizo makubwa sana. Baada ya kuona kuwa anapewa matumizi makubwa kwa matunzo ya mtoto kwa mwezi na wanandoa hawa maisha yake yamekuwa mazuri. Tunahisi anataka kumtumia mtoto kama mtaji. Najua kuwa ana uchungu na kiumbe wake,lakini baba mtu je?? its crazy wajameni. Kibaya zaidi ucku wa manane anapiga simu kwa wanandoa hawa kuwa mtoto kazidiwa baba wa watu huyooo, kumbe uongo. Can u imagine this?
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Maji ukiyavulia nguo huna budi kuoga, damu ni nzito kuliko maji
   
 8. LD

  LD JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Aisee hapa wala hatuitaji maombi wala kuomba, akili tulizopewa na Mungu zinatosha hapa. Usitegemee huyo bi mkubwa akawa na heshima kwa bi mdogo hata siku moja, bi mdogo ana mtoto huyo mwingine hana. Kama we Msomaji wa biblia Sara mke wa Ibrahimu alikuwa duni kwa kijakazi wake ingawa ni yy alimruhusu Ibrahimu aingie kwake.

  Haiwezekani mtoto wa umri huo akae mbali na mama yake akiwa yupo hai, tena anaweza. Hata sheria hairuhusu.

  Huyu baba lazima awe attention na maswala ya mtoto, hata kutoroka saa sita za usiku kwa sababu ndo mtoto pekee aliye nae.Haijalishi amedanganywa au hajadanganywa.

  Hakuna cha makubaliano hapo, walikubaliana jambo ambalo haliwezekani kabisa. So wewe pamoja na mwenzio tumieni akili ya kiume hapa, mtoto na mama ake waendelee vizuri. Na kama anaipenda ndoa yake aipiganie pia.

  Acha kuwashauri wenzio vibaya, hakuna mtoto anaetengwa na mama yake akiwa mdogo hivo!!

  Nalala kesho nikute umebadilisha mawazo ulionayo juu ya huyo mama mtoto.
   
 9. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hii post imetosheleza kabisa kujibu hii sredi, tunaomba sredi ifungwe rasmi.
   
 10. L

  Leornado JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mie pia ni msuluhishi tu na nimeshindwa kabisa ndo maana natafuta masaada. Tumeshaenda hadi kwa wachungaji na wazee wote wa ukoo bila mafanikio. I am feeling sorry kwa rafiki yangu maana hawakutegemea na mkewe kuwa huyu bibie angewageuka baada ya mtoto kuzaliwa. Hii kitu ya ya kuzaana kutoa mtoto alelewe na baba yake mbona ipo sana. Pkease tuangalie pande zote mbili.

  Ingekuwa wewe ndio huyu mke wa ndoa usiezaa ungefanyaje? huyu mwanamke mwingine hatambuliki kokote na hana uhusiano wowote na baba mtoto. Huu mwka wa tatu tunapiga kwata hadi mtoto keshajua mama yake halisi.
   
 11. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Mimi naona ni huyo bi mdogo anataka kuota pembe ingawa kwa namna moja au nyingine upande wa wanandoa umekosea pia.

  Huyo bi mdogo ni anatamaa na pesa ila labda wajaribu kufanya mipango ya child support then mtoto akiwa na umri wa miaka saba ,waende court for full child custody.

  Wanandoa wamekosea kwa kutofanya research kama Tanzania wanaruhusu hiyo biashara ya mama kuwa kama surrogate tu ila mtoto ni mali ya wanandoa. ingawa hii najua ipo USA na nchi nyingine zilizoendelea, pia wangewashirikisha upande wazazi na ndugu wengine wa bi mdogo.

  Kama vipi atafute mtu mwingine wafanye taratibu zote za kisheria na kuhusisha pande zote ili azae mtoto mwingine, ila huyo bi mdogo ampotezee iwe ni kutoa matumizi ya mtoto na kumuona mtoto tu ikibidi ananunua mwenyewe mahitaji au anaenda na mkewe kumuona mtoto.
   
 12. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Wewe unawashauri kama nani kwanza?? Ulikuwepo wakati wanaandikiana huo mkataba???

  Halafu watoto mbona sio shida sana waende msimbazi centre au mburahati kuna watoto wachanga kabisa pale unajichagulia tu kisa cha kuleta mwanamke mwingine nini???

  Huo uamuzi si sahihi. na una hakika mwanaume hana shida yoyote?? Wamethibitisha hospital??

  Mambo mengine sio uchawi ni akili zetu wenyewe zinakuwa finyu
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mpaka umri wa miaka saba ndipo mtoto anaweza kuruhusiwa kukaa mbali na mama yake kisheria. Kawatembelee Ustawi wa Jamii. Kwa sasa amtunze mama na mtoto hadi wakati huo.
   
 14. LD

  LD JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante Dena.
   
 15. Clearing

  Clearing Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole yake muathirika, huyo baba alikua anawaza nini kumwambia huyo dada kwamba tuzae mtoto halafu utupe tumlee mimi na mke wangu? kwanza kitendo cha huyo mdada kumkubalia tu ilikuwa inamaanisha kuna kitu anataka kutoka kwao so aliwawekea mtego maridhawa. Na huyo baba inaonyesha alikurupuka tu hakuomba ushauri kwa watu hasa wazazi na wengi tu waliomzidi umri. Hata kama angekua hatoi matunzo ni ngumu sana mama abebe mimba na mikash kash yote ya ujauzito achilia mbali kujifungua alafu aje akupe mtoto. Huyo baba hakushangaa hata mtoto alivyo mchungu mtu azae akupe hiyo ni ngumu. Ni bora angekubali kuzaa na mtu wakubaliane akifika umri wa miaka saba ndio apewe ila kwa upande wa huyo mama yuko kibiashara zaidi kwani alijua kabisa hawezi kutoa mtoto alelewe na mama mwingine. Kwa huyo baba namshauri apoe tu matumizi awe ananunua yeye asimpe mama pesa na mtoto akiumwa yeye ndio aende ampeleke hospitali na kutoa gharama asimpe huyo dada hata senti nusu kwani huyo dada ni mshenzi (mtanisamehe wadada) ila huyo baba suala la kupewa mtoto kabla ya miaka saba alifute kabisa akilini mwake. NITARUDI
   
 16. LD

  LD JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama inawezekana hili. Wakubali tu wote walikosea, baba ampe mama matumizi ya mtoto kama anavyostahili tu.
   
 17. Clearing

  Clearing Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huoni huyo dada anamtumia mtoto kumkomoa huyo baba kitu ambacho si kizuri?
   
 18. B

  Binti Lawrence Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mtu unapoapa mbele ya kanisa/msikiti "kwa shida na raha" huwa ina maanisha nini??. Sikuona sababu ya mwanaume kuomba kuzaa mtoto nje ya ndoa kwani huko ni kumsononesha mwenziwe na ni kinyume na kiapo.Kwangu mimi naona kitendo cha huyo dada kung'ang'ania mwanae ni ka adhabu kadogo Mungu amekatoa kuwaadhibu wanandoa hao

  Ok, imekwishatokea nadhani baba asiwe na wasiwasi maadamu mtoto ni wake atabaki kuwa wake hata akilelewa na mamaye, kikubwa apeleke matumizi yote muhimu kwa mama na mtoto
   
 19. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nina rafiki yangu huu mwaka wa kumi na sita kaoa ila mkewe wa ndoa bahati mbaya hazai, jamaa yeye hana tatizo. Mkewe kamruhusu baada ya yeye kumwomba azae nje then amchukue kachanga huyo wamlee wao kama mtoto wao. Mtoto kazaliwa nje ya ndoa sasa ana miaka mitatu ila huyu mwanamke pamoja na kuingia mkataba na wanandoa hawa kagoma kumtoa mtoto mwaka wa tatu sasa na ndoa ya watu iko hati hati kuvunjika maana huyu bibie mdogo anawavuruga sana. Nimejaribu kusuluhisha kwa kila namna imeshindikana na kumbembeleza bibie kasema mtoto hatoi. Naombeni mawazo yenu.
   
 20. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kosa lililo fanyika ni kumweleza huyo bi mdogo ukweli yeye ange act as if anaiba nje then akisha zaa anamlaghai kwa maneno laini lazima ange mpa huyo mtoto,sasa hivi ni ngumu maana bi mdogo anataka aingie ndani ya nyumba awe m/house,kitu ambacho si kizuri kwa maisha yake ya mbeleni,lililobaki jmaa aachane na huyu bi mdogo atoe tu pesa ya matunzo pindi akipata mtu wake atamleta mtoto mwenyewe bila kumuomba yangu ni hayo tu
   
Loading...