KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 699
Ama kweli matukio mengi nchini huitwa - ONLY in Tanzania.
Hivi kweli umewahi kusikia askari akishindwa kumkamata mwizi kwa sababu mwizi huyo katumwa..
Wezi wengi Ulaya hata ktk Benk hutumwa, master planner hubakia kutazama mchezo unavyokwenda...Wauza unga toka Columbia hutumwa lakini wote hawa hukamatwa na wakafungwa pamoja na kwamba wametumwa. Leo Tanzania mtu alotumwa kuiba sii mwizi..Basi kama kweli ipo sheria hiyo tutaibiwa sana..Na hakika ya maneno haya itafungua ukurasa mpya wa sheria kiasi kwamba kesho mahakamani wezi watashinda kesi zao, kwa sababu WAMETUMWA.
you are absolutely right mkuu.mi naona tunachezeana akili tu na huu upuuzi wa EPA.Vitu viko very clear wanaleta mazingaombwe.Najuuta kuongozwa na JK kama rais wangu .Naona aibu kwa kweliKagoda case closed.
Ukisikia mtu mkubwa kama Feleshi bila aibu anasema tumpelekee habari Kagoda ni nani wakati Mwanakijiji alimpa kila detail, sasa sijui anataka zipi zaidi.
Kamata RA atawataja wote aliokula nao. La sivyo amwache aendelee kutamba na afute kesi zile zingine zote ili sisi ikifika wakati tuamue nini la kuwafanya. Full stop. Wasituchezee akili.
wewe kama hujatumwa basi umehusika kwa kiasi kikubwa sana, mawazo yako ni sasa na kutia supu nazi....huwezi kukaa kimya kwenye hili la ufisadi kwa mambo makuu ninayoyaona mimi:tusiposema, tukawataja, tukawachukulia hatua na kuwataka warudishe pesa zetu;hakuna haja ya kujadili kagoda kama ufisadii kwani kwa ujumla wake CCM na serikali yake ndo waliotufikisha kwenye wizi wa aina hizii (ufisadi wa fedha na madaraka).
tunahitaji kuhamasisha maendeleo ya jumla kama maji safi na salama, elimu, afya, umeme, barabara, utawala bora, kilimo na viwanda na kukemea vipingamizi vyake kama vile uongozi mbovu(wizi, ulafi, uwezo mdogo) na sera na sheria kandamizi (katiba ya wote ipatikane) katika kufikia maendeleo hayooo...
hatuna haja ya kutoa nafasi kubwa ya media kuzungumzia feleshi na kagoda!!! haijengi wa kuhamasisha maendeleo ya msingi kwa mlalahoi..
inawezekana kuleta mabadiliko kwa kuwa na uongozi mbadala kuanzia kijiji hadi taifa..
maendeleo yanawezekana kwani iweje barabara za kuunganisha mikoa zijengwe ndani ya muda mfupi tena baadhi kwa kodi yetu..gafla leo hata umaliziaji wa km 5 (sam mujoma) ni taaabuuuu????
lagosi ilihamia abuja from nothing na leo miundo mbinu ya abuja ni ya kuigwaaa...waliwezajee???
CHANGE WE CAN BELIEVE IN..
Kama DPP bwan Feleshi anasema akimkamata mtu aliyechukua fedha za KAGODA haimsaidii kumpata mtu aliyemtuma mtu aliyechukua fedha basi hakuna haja ya yeye kuwepo kwenye cheo hicho kwa maana HAFAI
Wanasheria mnisaidie; fedha za EPA kupitia kagoda zimeibiwa Benki Kuu (BOT). Kisai cha Tsh. 40bil zimeibiwa kwa staili ya kuforgi nyaraka. DPP anasema walikuwa wanazichukua hizo fedha wanajulikana ila hawezi kuwashtaki eti walitumwa tu. Sasa anatafuta waliowatuma.
(a) amejuaje kwamba hao jamaa walitumwa?
(b) kama walitumwa si watakuwa wamewataja mabossi wao?
(c) fedha nyingi kiasi hicho si unaweza ku-trace kwa kuangalia bank transactions na kuzifuatilia akaunti husika?
(d) kama aliyewatuma ni Rais, au CCM, DPP atachukua hatua gani? atawaachia hao jamaa anaodai walitumwa?