Kagera: Watu wawili akiwemo Askari wa JWTZ wafariki ajalini wakisafirisha mitihani ya kidato cha nne ya majaribio

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Watu wawili akiwemo askari wa Jeshi la Wananchi ambaye alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakisafirisha mitihani ya majaribio ya wanafunzi wa kidato cha nne wamepoteza maisha mkoani Kagera baada ya gari aina ya Iveco mali ya Jeshi la wananchi lenye namba za usajili 5821 JW 09 walilokuwa wakilitumia kupinduka katika eneo la mteremko mkali ulioko kwenye barabara ya kumnazi wilayani ngara.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Kamishina msaidizi Revocatus Malimi amesema gari hilo lilikuwa likitokea mkoani Mwanza na amewataja waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi Anthon Kisiza ambaye ni afisa mteule daraja la pili mwenye umri wa miaka 54 na Ibrahim Mkoromo ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya uchapishaji ya kisomo.

Amesema jeshi la polisi limeanza uchunguzi chanzo cha ajali hiyo ili liweze kubaini kama ilitokana na uzembe wa dereva ama la, nakutumia nafasi hiyo kuwataka madereva wawe makini katika kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ili wajiepushe na ajali hasa zinazotokea kutokana uzembe walionao baadhi ya madereva.
 
Siku hizi hiyo mitihani ya majaribio inasafirishwa na Jeshi?R.I.P Afande.
 
Sijaelewa mitihani ya majaribio ndani ya Iveco ya baka baka?

Halafu RPC naye,dereva wa JW hata akichunguza akakuta ni uzembe atafanya nini kwa mfano?
Pole familia ya marehemu WO2 Kisiza
 
Mamlaka ya polis Ni makubwa sana kushinda unavyodhani,kitakachofuata wote hao watoto wa baba mmoja Ni mwendo wa kuandika ripot na dereva kuadabishwa kijeshi tu hakuna namna hapo
 
Sijaelewa mitihani ya majaribio ndani ya Iveco ya baka baka?

Halafu RPC naye,dereva wa JW hata akichunguza akakuta ni uzembe atafanya nini kwa mfano?
Pole familia ya marehemu WO2 Kisiza
Kwa akili yako unadhani Polisi hawawezi kuchunguza JW? Wanapoua uraiani wanapelekwa wapi? Akili ya kijiweni kudhani JW wako juu ya kila kitu na hawaguswi ziache huko huko.
 
Back
Top Bottom