Kagera: Mgombea udiwani wa CHADEMA kata ya Buhangaza aliyetoweka, apatikana akiwa hajitambui, CHADEMA walia na Polisi

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
mgombea.jpg

Kampeni za ubunge na udiwani zikiendelea, mgombea udiwani (Chadema) Kata ya Buhangaza wilayani Muleba amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Imeelezwa alipotea Februari 2,2018 alipokuwa akitokea Bukoba mjini kwenda nyumbani kwake Kijiji cha Buhangaza ikidaiwa ametekwa.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Isack Msangi amethibitisha kupokea taarifa za kupotea kwa mgombea huyo.

Amesema kuwa hawana madai kuwa ametekwa bali aliondoka nyumbani na hajarejea.

Msangi amesema polisi inawaomba wananchi kutoa ushirikiano bila kupotosha au kuegemea upande mmoja wa kisiasa kwa kutuhumu upande mwingine bali waungane kufanikisha kupatikana kwake.

Katibu wa uenezi wa Chadema jimbo la Muleba Kusini na mratibu wa chama hicho jimbo la Muleba Kaskazini, Hamisi Yusufu amesema leo Februari 4,2018 kuwa mgombea huyo ni Athanasio Makoti (28).Yusufu amesema Makoti ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la AGT anashiriki uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika Februari 17. Anachuana na mgombea wa CCM, Jenitha Tibeyenda na wa NCCR -Mageuzi, Grason Anaseti.

Amesema Februari 2,2018 saa 12:00 jioni akitumia simu yake ya mkononi aliwajulisha viongozi wa Chadema ngazi ya wilaya kuwa alipanda gari lenye watu wanne kutoka Kijiji cha Mafumbo njia panda ya kwenda Kamachumu akielekea Kijiji cha Buhangaza.

Yusufu amesema baadaye ujumbe mfupi wa maneno (sms) ulitumwa kwa Advera Kalikwela, diwani wa viti maalumu (Chadema) Kata ya Ijumbi ukieleza, “Nimeteremka hapa Mafumbo kabla ya kufuatwa na bodaboda wangu nimezingirwa na gari lenye watu wanne mmoja mwanamke, mbele dereva wa kiume na vijana wengine wawili ni kama nimetekwa.”

Amesema baada ya ujumbe huo, simu ya Makoti iliita bila kupokewa na hadi sasa hakuna taarifa za kuonekana kwake na kwamba familia ilitoa taarifa polisi.

Egbert Makoti ambaye ni mdogo wa mgombea huyo amesema baada ya kuchukua fomu, ndugu yake aliwaeleza kuna watu ambao hakuwataja waliomtaka aachane na kata hiyo wakimtaka apokee Sh8 milioni lakini alikataa.

Katibu wa Baraza la Wazee la Chadema, Rodrick Lutembeka amesema chama hicho kitaendelea kumnadi katika kampeni zinazoendelea katika Kata ya Buhangaza.
Kata hiyo ina vijiji vitatu vya Buhangaza, Kashenge na Buyaga ikiwa na vitongoji 13 ikikadiriwa kuwa na zaidi ya wapiga kura waliojiandikisha 2,500.

Chanzo: MCL

=====

Update: 05 Feb 2018

Mgombea wa udiwani Kata ya Buhangaza, Muleba (Chadema), Athanasio Makoti aliyekuwa amepotea tangu Februari 2, mwaka huu amepatikana. CHADEMA imesema alitupwa barabarani maeneo ya Hospitali ya Kagondo.

Chadema.jpg
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KUHUSU KUTEKWA KWA MGOMBEA WA UDIWANI BUHANGAZA (CHADEMA), NELSON ATHANAS MAKOTI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa tahadhari kubwa tukio la kutoweka katika mazingira yenye utata kukiwa na viashiria vya utekwaji kwa Mgombea wa Udiwani Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Buhangaza, Muleba, Ndugu Nelson Athanas Makoti, huku Jeshi la Polisi wilayani humo likisuasua kufungua jalada la uchunguzi wa tukio hilo kwa siku mbili, hadi alipoonekana usiku wa kuamkia leo akiwa taaban na hajiwezi.

Kutokana na mwenendo uliooneshwa na polisi Wilaya ya Muleba katika tuko hilo na kauli iliyotolewa na polisi ngazi ya mkoa, tunatoa wito kwa jeshi hilo Makao Makuu kuingilia kati ili uchunguzi wa haraka kuhusu suala hilo ufanyike kwa ajili ya haki kutendeka na hatua za kisheria kuchukuliwa.

Mbali ya Jeshi la Polisi Makao Makuu, pia tunatoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBU) kutumia mamlaka yake ya kikatiba na kisheria kuhakikisha tukio hilo linafanyiwa uchunguzi wa haraka na kina kuwabaini wahusika na kuchukua hatua.

Aidha, Chama kinaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoka hadharani kukemea vitendo kama hivyo ambavyo vinatia doa mfumo wa uchaguzi na demokrasia nchini. Ukimya wa Tume ya Uchaguzi unaashiria kuwa wanakubaliana na tabia hii mpya ya utekaji ambayo tuliilalamikia hata wakati wa uchaguzi wa marudio wa Kata 43 ambao ulipelekea baadhi ya Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi wa

marudio uliofanyika Januari 13, vikiwa na lengo la kuwaambia Watanzania na dunia nzima kuhusu ukiukwaji wa misingi ya uchaguzi, zikiwemo sheria, kanuni, maadili na miongozo mbalimbali.

Halikadhalika, tunaomba makundi mbalimbali katika jamii, hususan taasisi za masuala ya utetezi wa haki za binadamu na vyama vya siasa kuendelea kuunganisha nguvu, kulaani na kupinga vikali matukio ya namna hii katika jamii yetu.

Chama kimefikia hatua hiyo baada ya kufuatilia kwa karibu taarifa za tukio hilo tangu habari za kutoweka kwa Ndugu Makoti zilivyopatikana.


Awali tukio hilo lililotokea Februari 2, mwaka huu majira ya jioni, wakati Makoti akiwa njiani kurudi nyumbani kwake, liliripotiwa polisi, kituo kidogo cha Polisi Ijumbi kisha baadae Polisi Muleba mjini.


Jambo la kushangaza ni kwamba, tangu siku ya Jumamosi, Februari 3, mwaka huu, taarifa hizo zilipofikishwa kwa polisi Muleba na viongozi wa CHADEMA wilayani humo, pamoja kufanya kikao na viongozi wa chama na familia ya Makoti, jeshi hilo halikufungua jalada la kesi wala hawakutoa namba ya RB kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo kama taratibu za kisheria zinavyoelekeza, kwa sababu ambazo hazieleweki.


Viongozi wetu waliporejea kituoni hapo siku iliyofuata, Jumapili Februari 4, kufuatilia hatua zilizofikiwa, waliambiwa kuwa jalada halijafunguliwa wala wasingeweza kupata RB Namba kwa sababu anayehusika na majukumu hayo hakuwepo ofisini. Kwa hiyo hakukuwa na uchunguzi wowote uliokuwa unaendelea kwa tukio zito kama hilo.


Katika mtiririko huo huo unaoweza kuhojiwa na kutiliwa shaka, jioni ya Februari 4, Kaimu RPC wa Mkoa wa Kagera, Isack Msangi alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akitoa masharti kwa wananchi ambao wanaweza kuwa na taarifa za kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.


Aliwaambia wananchi wasitoe taarifa za kuegemea upande mmoja wa kisiasa na kuutuhumu mwingine. Jambo hilo si sahihi hata kidogo. Tunaamini kazi ya wachunguzi wa polisi ni kupokea taarifa na kuzifanyia kazi, ikiwemo kuchuja sio kuelekeza zitoleweje na kwa mtizamo gani! Maelekezo hayo ya polisi yanaweza kuwatisha wale wote wanaoweza kusaidia taarifa zenye ushahidi wa tukio hilo.


Aidha yanaweza kuepusha wahusika kujulikana na pengine jeshi hilo kushindwa kupata viashiria vinavyoweza kusaidia kubaini mtandao wa watu 'wasiojulikana' ambao wamekuwa wakidaiwa kupoteza au kuteka watu katika matukio mengine yanayofanana na hilo la Makoti.


Baada ya Ndugu Makoti kuonekana usiku wa kuamkia leo baada ya kutupwa barabarani kisha kusaidiwa kufika Hospitali ya Kagondo akiwa hoi kwa maumivu makali, akilalamika kupigwa sana na watu waliomteka, wakiwa wamejifunika vitambaa usoni, tunasisitiza tena;


Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola vitimize wajibu wake katika tukio hilo la kutoweka kwa Ndugu Makoti, huku vikitambua kuwa CHADEMA mbali ya kulaani vikali tukio hilo, kinasikitishwa na hakiridhiki na hatua na kauli zilizochukuliwa au kutolewa na jeshi hilo wilayani Muleba na mkoani Kagera, hasa ikizingatiwa kuwa tukio la Ndugu Makoti ambalo limetokea katikati ya kampeni za uchaguzi mdogo, limetukumbusha matukio ya kukamatwa kwa wanachama na viongozi wetu na kushikiliwa na polisi Muleba kinyume cha sheria, lakini pia kushambuliwa kwa risasi na watu wa CCM bila hatua yoyote kuchukuliwa wakati wa uchaguzi mwingine wa marudio, Kata ya Kamwani, uliofanyika Januari, mwaka jana. Ni muhimu pia polisi wakajibu swali linaloanza kujitokeza kuna nini huko Jimbo la Muleba Kusini, linaloongozwa na mmoja wa makada maarufu wa CCM mkoani Kagera, Prof. Anna Tibaijuka.


Vyombo vya dola vijikite kuhakikisha, wahusika wa tukio la Ndugu Makoti wanajulikana na kuchukuliwa hatua stahiki ili kukomesha matukio ya namna hiyo yanaoonekana kushamiri nchini.


Ni muhimu sana vyombo vya dola vikaonesha mwenendo ambao utawashawishi wananchi waamini kuwa kweli vinachukizwa na


vitendo vya upoteaji, utekwaji na kushambuliwa kwa risasi kama matukio hatarishi sana ya usalama wa raia na mali zao.


Mojawapo ya dalili za mwenendo sahihi ni kuchukua hatua za haraka za uchunguzi wa matukio ya namna hiyo na kutoa taarifa. Kinyume na hayo, vyombo hivyo vitakuwa vinahalalisha vyenyewe kuendelea kuwekwa katikati ya shutuma na tuhuma kila matukio ya namna hiyo yanapojitokeza.

Imetolewa leo Jumatatu Februari 5, 2018 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA
 

Attachments

  • PRESS Feb5 CDM.pdf
    301.4 KB · Views: 69
Huyu Jamaa Mimi namjua zaidi, I know I may sound crazy but nimeona wameripoti kuwa tangu tarehe mbili Feb amepotea but Facebook yake Jana usiku alikuwa online, means MTU aliyetekwa hawezi kuwa online. Wala jina lake sio hill anaitwa Nelson Mandela Kamugisha.

Ni mchungaji morogoro but sijajua imekuaje ameamua kugombea udiwani huko. Lakini kwa hakika zaidi mtafuteni Facebook Nelson m Kamugisha mtapata hakika ya nini nasema.
 
Hahaha kugombea kupitia chadema ndio njia sahihi kwa wale wanaotafuta kazi serikalini. Nawashauri vijana msio na kazi kadi na uanachama wa chadema ni muhimu sana. Utanunuliwa au utatekwa na kupewa kazi serikalini.
Kumbukeni ccm=serikali.
 
Kuna Taarifa zinasema kuna mgombea Wa udiwani kupitia chadema kapotea.
Lakini kwa majina aliyotambulishwa kwa jina la Athanasio Makoti, ila sisi tunaofahamu haitwi hivyo Bali jina lake halini ni Nelson Mandela Kamugisha.

Huyu ni mchungaji morogoro sijajua ameingiaje kugombea udiwani. Ila kwanza jina sio lake, pili Jana usiku alikuwa online Facebook unaweza mtafuta na kumuona kwa jina LA Nelson M Kamugisha.

Rejea hapa
 
Nadhani huyo mutu hatufai. Tiyari kishaonesha kuwa ni ndumila kuwili. Hata akichaguliwa mtashangaa kabla ya kuapishwa uchaguzi mdogo unaitishwa kwani atakuwa keshapokea ila 8m aliyoisusa
 
Nadhani huyo mutu hatufai. Tiyari kishaonesha kuwa ni ndumila kuwili. Hata akichaguliwa mtashangaa kabla ya kuapishwa uchaguzi mdogo unaitishwa kwani atakuwa keshapokea ila 8m aliyoisusa
Haya ila akija pita waanze uhakiki wa majina kwanza maana, hata humu kuna uzi alifanya fujo kwa dc wa meatu ilikua kama miaka 5 iliyopita.

Labda wazee wa kufukua makaburi wafukue huo uzi
 
Back
Top Bottom