BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,423
- 8,229
Kagera: Mfanyabiashara apigwa faini ya Tsh. Milioni 1 kwa kuwasilisha Nyaraka za Uongo
Ni uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kyerwa dhidi ya Jackson Kalikawe ambaye ni Mfanyabiashara aliyekutwa na hatia ya Makosa mawili ikiwemo kuwasilisha nyaraka zenye taarifa za Uongo
Kwa mujibu hati ya Mashtaka, Mshtakiwa alitumia nyaraka zilizoghushiwa na kubadilishwa tarehe ya mwisho wa matumizi na kujipatia Kibali cha kusafirisha Kahawa kinyume na Sheria
Mshtakiwa aliamriwa kulipa Faini ya Tsh. 500,000 kwa kila kosa au kwenda Jela kwa miaka 7 ambapo alifanikiwa kulipa fedha hizo na kuachiwa huru.