Kagera: Katibu Tawala aagiza uchunguzi wasababu ya Walimu wengi kuomba kustaafu kabla ya kufikisha miaka 60

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora amewaagiza maofisa wa idara ya elimu katika mkoa huo kutathimini sababu zinazochangia wimbi kubwa la walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo za kuchukua uamzi wa kuomba kustaafu kazi kabla ya kufikisha umri wa miaka 60 wakati hawana matatizo yoyote ya kiafya.

Prof. Kamuzora ametoa agizo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za msingi kutoka kwenye wilaya zote zilizoko mkoani humo waliohudhuria mafunzo maalumu yanayotolewa na wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu (ADEM), amesema uamzi huo unachangia kudhoofisha suala zima la taaluma kwani unapunguza nguvu kazi.
 
Sasa Nani atataka kuwa na morali ya kufanya kazi katika mazingira haya yaliyojaaa Vitisho kudhalilishwa kunyanyaswa na Kudhulumiwa stahili zako kinguvu? Mi niliamua kustaafu nikiwa na 37. Bora kidogo nachopata kwa Amani kuliko kikubwa Cha manyanyaso. Heko walimu mnaojitambua.
 
Tuna viongozi wa ajabu kweli kweli. Hili nalo linahtaji uchunguzi wakati ni dhahiri watumishi wengi wanakimbia Kikokotoo cha 2023? Mnatengeneza sheria za kuumiza wananchi halafu Waziri wa sheria anaropoka eti hakuna sheria kandamizi Tanzania!!!
 
Hii ngoma hakuna kutema wala kumeza!

Ukistaaf kwa hiyari kosa, ukiacha kazi kwenda private kosa, ukifundisha tuition kosa, ukidai nyongeza kosa, ukidai promotion kosa!

2015

Bango la Walimu 2015 '… Shemeji (JK) unatuachaje…'

Jk '… Hahaah nmeliona bango lenu la nawaachaje…teh teh ( cheko la kebehi)… mie sina maneno nawaacha na Mwalimu mwenzenu…'


Huenda maombi ya kustaafu kwa hiyari kabla ya 2023 yataanza kukataliwa
 
Niseme wazi Pamoja na kuwa sikutaka kuwa mwalimu Lakini napenda Sana Kufundisha ingawa kipaji changu Ni Ufundi. Nilifundisha kwa miaka michache. Nashukuru Kuna watu mkono wangu binafsi umewavusha kimaisha ni kama ndugu leo. Mazingira ya kazi yalinivunja Moyo Sana.

Licha ya kipato kidogo Lakini changamoto zilikuwa nyingi Sana. Nashangaa mno kwa Nini Elimu tumeiweka Nyuma Sana. Mimi naamini Maarifa kichwani ndiyo msingi wa kumwinua mtu kiuchumi, Kijamii,Kimaadili pia. Lakini Siyo kwetu. Haya angalia wastaafu wanavyosotea Haki zao mtu anakaa miaka miwili hajapata Haki yake na bado Tena Unataka kuvuruga kwa Nini asikimbie?

Elimu yetu imekosa ushindani kabisa imebaki kukariri tuu.. Soko la ajira la kimataifa hatuwezi kufika huko. Naamini Kama Kweli tungewekeza kikamilifu katika Elimu yetu na kuwajali wasimamizi na watoaji wa Elimu basi hata miradi mingi nchini ingefanywa na wazawa.
 
Katibu Tawala Kagera unataka kufanya uchunguzi wa nini kama siyo kuharibu rasilimali? Ndungai alisema walimu waongezewe masomo, sasa limeongezwa somo la Historian ya Tanzania ambalo walimu watalifundisha bila semina.

Serikali imepanga kuleta kikokotoo, yaani kila mnachowaza ni kukandamiza walimu. Waache wastaafu ili Serikali iajiri wengine mbona vijana wapo wengi tu mtaani?

Waache walimu wastaafu. Yaani kama ingewezakana kustaafu katika umri wa 40,45 au 50 wangetoka wengi sana. Unawabana iweje? Waache wastaafu.
 
Kikokotoo.
Mwehu tu ndio hajui
... wanawahi grace period inayoishia 2023 kwa formula ya zamani. Baada ya hapo ni kilio na kusaga meno. Thanks Mkuu kwa kulitambua hili kabla hata utafiti alioagiza Profesa haujaanza.
 
Wafanye maslahi ya Walimu yawe kama ya Wabunge, watumishi wa BOT, TPA, TBS na sekta nyengine afu waone kama watataka wastaafu na miaka 60.
Sisi kama serikali hatuwezi walimu wako wengi sana hatuna hayo mahera.

Benki kuu, TRA, nk hizo haziko kila kata kama shule. Hawa tunawalipa vizuri kwa sababu ndio wanaotutunzia pesazetu hatutaki washawishike kuiba.

Walimu wafanye kazi mpaka wakati wa kistaafu tutawapa magao yao.
 
Back
Top Bottom