Kagera: Ateketea kwa moto gesti

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
13,766
20,154


MTU mmoja mkoani Kagera aliyetajwa kwa jina la Neema Bayo (49) aliyekuwa ndani ya moja ya vyumba vya nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Anti iliyoko wilayani Muleba mkoani Kagera amepoteza maisha kwa kuteketea kwa moto ulioteketeza nyumba hiyo ambao hadi sasa chanzo chake hakijajulikana baada ya kushindwa kujiokoa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Kamishina Msaidizi, Revocatus Malimi alifika kwenye eneo la tukio na kupata maelezo ya awali kutoka kwa mhudumu wa hoteli hiyo.

Baada ya kupata maelezo hayo akielezea juu ya tukio hilo amesema kuwa marehemu huyo alikuwa ni mmoja wa watu watano walikuwa wamefikia kwenye nyumba hiyo ya wageni ambao walinusurika kifo baada ya kujiokoa kufuatia moto huo.
 
Ajali zitokanazo na moto zimetamalaki mwezi huu. Jeshi la Zimamoto lijipange kutoa elimu kuhusu kupambana na moto katika makazi ya watu.
 
Elimu ya moto iliyitolewa kkoo bado haijawafikia wengi eeh
Moto ni hatari muda mwingine wazima moto huwa wanateketea na moto hatuna vifaa vya kisasa vya kupambana na moto na majengo mengi hayana vile vifaa vya kutoa taarifa ya moto hasa hotel,shule na masoko ilitakiwa viwepo na majengo marefu hilo Bunge tuu halina vifaa vya kisasa vya kutoa taarifa ndio tuzungumzie mtaani...Elimu ya moto ni pana sana sio ujanja ujanja
 
marehemu huyo alikuwa ni mmoja wa watu watano walikuwa wamefikia kwenye nyumba hiyo ya wageni ambao walinusurika kifo baada ya kujiokoa kufuatia moto huo.
“Marehemu alikuwa ni kati ya watu watano ambao walinusurika kifo baada ya kujiokoa na moto huo.”

Kwa hiyo ina maana moto aliufaiti lakini alipopigwa panga la mbavu na mwemye mume ndipo alipokufa, got it.
 
“Marehemu alikuwa ni kati ya watu watano ambao walinusurika kifo baada ya kujiokoa na moto huo.”

Kwa hiyo ina maana moto aliufaiti lakini alipopigwa panga la mbavu na mwemye mume ndipo alipokufa, got it.
Maybe
 
Back
Top Bottom