Kagasheki aliwahi kuwa balozi wapi na lini?

Kagasheki aliwahi kuwa balozi wapi na lini?

Status
Not open for further replies.

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,272
Khamisi Kagasheki, waziri wa maliasili na utalii aliyejiuzulu huwa nasikia anaitwa Balozi. Mtu yeyote aliyewahi kuwa mwakilishi wa nchi katika nchi nyingine kama balozi huendelea kuitwa balozi hata baada ya kustaafu kama vile kwa walimu, madaktari, wachungaji nk. Ninaomba yeyote anayefahamu nchi ambayo Khamisi Kagasheki aliwa kuwa balozi wetu na mwaka au miaka aliyohudumia huko.

Nimeuliza hivyo kwakuwa nimeona andiko mahali linalosema hajawahi kuwa balozi isipokuwa baba yake mdogo ndiye alikuwa balozi na kuwa yeye aliwahi kufanya kazi ubalozini.

Sasa mtu akifanya kazi ubalozini naye anakuwa balozi? Au inawezekana alikuwa balozi wa nyumba kumi? Nimeuliza hivi baada ya kuona majadiliano katika Fb kati ya wadau wanaomfahamu. Nanukuu: "Huwa nashangaa watu wanakomaa na "Barozi Hamisi Kagasheki". Swali langu huwa ni je ubarozi aliupata lini?

Aliwahi kuwakilisha Taifa letu nchi gani? Nina uhakika ukimuuliza hata yeye swali hilo jasho litamtoka. Siamini kwamba katiba yetu ya sasa pamoja na ubovu wake, inaruhusu watu kurithi ‪#‎vyeo‬ vya baba zao au baba zao wadogo. Siamini hilo!" "sikurupuki. Sina chuki na Kagasheki ila nasimamia ninachokiamini.

Ushahidi upo kwamba aliforge vyeti. Mfano mdogo sana kwenye CV yake anaonesha aliwahi kuwa mkurugenzi wa World Intellectual Property Organization, kitu ambacho si kweli.

Pia anasema aliwahi kuwa barozi wakati aliyekuwa barozi ni baba' ke mdogo. Yeye hajawahi kuwa barozi. Tuna ushahidi kaka" "tumia kwanza muda wako kufanya tafiti. Ni rahisi sana kugundua uongo huo.

Aliwahi kufanya kazi kwenye ubarozi lakini hakuwa barozi. Kama hicho ndo unachotumia kama kigezo, you are wrong. Basi hata makarani kwenye barozi zetu ni mabarozi? Haya niambie alikuwa barozi miaka gani? Naomba uamini kwamba mimi si muumini wa siasa za chuki" "sasa ni hivi;

Huyu Kagasheki alimaliza darasa la saba akaenda Nyakato secondary, akafukuzwa kwa kosa la kupiga walimu.

Akahamia Kahororo nako akafukuzwa kwa kosa hilo hilo. Baba yake alikasirika akagoma kumpeleka shule nyingine. Alikimbilia Uganda kwa mjomba wake na akaanza kuhangaika kuingia kidato cha tano. Nako aliulizwa cheti cha form four kikakosa.

Mjomba wake anayeitwa KASIBANTE ambalo ndo jina la redio yake alihangaika hakufanikiwa na badala yake akaforge cha form six. Baba yake mdogo alimchukua na kwenda kusomea ukarani.

Baada ya masomo ya ukarani alifanya kazi ubarozi wa Uganda kwa kujitolea, na baadae Wizara ya Mambo ya nje kama karani. Kwa sababu ni mjanjamjanja akaweza kukwea na ukarani wake" "Nashangaa kitu kimoja, kwenye hiyo CV iliyoko kwenye web ya bunge anasema aliwahi kuwa Director wa World Intellectual Property Organization (WIPO). Sasa ikabidi nitafute waliowahi kuwa directors wa WIPO.

Anyway, nitaangalia hii website ya WIPO kwa undani nijue ukweli. Ningumu kufanya kazi organization kama hii alafu ukagushi vyeti http://en.wikipedia.org/.../World_Intellectual_Property World Intellectual Property Organization - Wikipedia, the free encyclopedia en.wikipedia.org The World Intellectual Property Organization (WIPO) is one of the 17 specialized...See More" "hii kitu imeninyima usingizi, imebidi niangalie kwenye website ya WIPO kwa undani nijue ukweli.

Kama jina analotumia ni Khamis Suedi, basi aliwahi kuwa Assistant Director General kwanzia 2003 japo alikuwepo WIPO tangu 1990. http://www.wipo.int/.../en/prdocs/2003/wipo_pr_2003_352.html Hizi ni baadhi ya nukuu za wanafb zilizonifanya niulize ili nijuzwe maana wadandia vyeo ni wengi mpaka tunashindwa kutofautisha na halisi.


=============

December 24, 2014:

Barua ya Uteuzi wa Balozi Kagasheki

attachment.php
 

Attachments

  • B5on9w0IgAACJLA.jpg
    B5on9w0IgAACJLA.jpg
    21 KB · Views: 344
Hii inakusaidia nini wewe! Acheni unafiki fanyeni kazi mjiletee maendeleo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Khamis Kagasheki

Politician

Khamis Suedi Kagasheki is a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Bukoba Town constituency since 2005. He is the current Minister of Natural Resources and Tourism. Kagasheki also served as ambassador of Tanzania in Switzerland. Wikipedia

Born: Tanzania

Education: Fordham University


Pls Paw funga thread majibu tayali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom