Utakua unamkomoa nani ukipiga msitu wa sao hill moto? Napenda kutofautiana kimtazamo hapa. Misitu ni mali ya watanzania wote na hivyo ni lazima iuzwe kwa watanzania wote bila kujali dini, rangi, kabila wala sehemu anayotoka.Mkuu mwache atunyime tu. Mbona kazi ni ndogo tu, njiti moja tu ya kiberiti inaangamiza na hapo atawajua wanamufindi sasa. Mwezi wa nane vibali huwa tayari lakini sasa tunautafuta mwezi wa kumi ye kakalia ngoja aonyeshwe..
Mbona mlima kilimanjaro watu wote wanapandisha watalii bila kupendelea wachaga ingawa na wao wanazima mioto?
Mbona kwenye madini watu wote wanapewa fursa sawa. Sikubaliani ni mtazamo wa kuwabeba wanamufindi eti kwa kuwa ndo wanazima moto. Sikubaliani pia na wazo la kuuza kwa mnada kwa makampuni makubwa. Ila ninachotaka ni tutumie neno watazania badala ya wanamufindi.