Kagame Oyeee, Kikwete Ziii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagame Oyeee, Kikwete Ziii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tizo, Jun 11, 2010.

 1. T

  Tizo Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rwanda arrests football head on way to World Cup  Brig-Gen Jean Bosco Kazura (Photo from Ferwafa - ferwafa.rw/fed) Jean Bosco Kazura served in Sudan's Darfur region

  The head of Rwanda's Football Federation, Brig-Gen Jean Bosco Kazura, has been arrested for travelling to the World Cup in South Africa.

  An army spokesperson said as he was also a soldier, the football official needed permission to leave the country.

  He was recalled and detained for "insubordination", spokesman Jill Rutaremara told the BBC.

  He denied it was to do with the general contacting two senior officers who recently fled to South Africa.

  They left Rwanda earlier this year after falling out with President Paul Kagame, who later reshuffled the military leadership ahead of elections due in August.

  "Even though he serves in the private sector with the football federation, he still has to obey military law," Lt-Col Rutaremara told the BBC's Great Lakes service.

  Brig-Gen Kazura was put in charge of training and operations after the reshuffle.

  Before joining the football federation, he had served with Rwandan peacekeepers in Sudan's troubled Darfur region.

  He was also involved in the military campaign conducted by the Rwandan Patriotic Front (RPF) to end the 1994 genocide, as were two other top-ranking officers arrested in April.

  August's elections will be the second presidential polls held since the genocide when Mr Kagame, the RPF leader, came to power.

  The World Cup kicks off in South Africa later on Friday - the first time it being held in Africa.


  MAONI:

  HIVI HUYU 'RAHISI' WETU SI KAMA KICHUGUU KWA HUYU MLIMA KILIMANJARO KAGAME AMBAYE AMEKUJA KWENYE SIASA JUZI TU????

  Rais gani hana clue ya uongozi??? Raisi gane mzembe hivi wakati taifa linakwenda ovyo ovyo wakati yeye na mawswahiba wake wanakula kuku.

  Cheki mwanaume huyu Rwanda. Kazi kwanza, starehe baadaye. Wakwetu- Kila siku starehe. Mweeeeeeeeeeeeeeeeeeee.Tufwire wanyambala
   
 2. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sijaelewa, ni kitu gani Rwanda imefanya hapo kinachomzidi kikwete kutokana na post hii...
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Huyu Kagame naona kajipambanua mapema; atakuwa ndo Rais wetu wa kwanza wa EAC.
   
 4. T

  Tizo Member

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa Mpeni sifa yesu, nini usichoelewa? Labda ni lugha ya kiingereza ngumu kwako?

  Angalia uthubutu wa kagame ku dhibiti hata majenerali wa jeshi wa ngazi za juu wanapopotoka. Huyu Mkuu wa soka na jenerali wa jeshi alitaka kwenda SA bila ruksa, akakamatwa. Hapa Mafisadi kina chenge, karamagi, rostam aziz, Lowasa na wengine kibao wanakula maisha wakati ni wahaini wakubwa kwa nchi. Unadhani kagame angekuwa prezidaa wa bongo tungekuwa hapa na mafisadi wakitamba hivi??? Waaaaaapiiii. Ni Hapa ukwereni tu ndo unaweza kuiba na ukachekewa.
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwanini unamwita rais ziiiiiiiiiiiii, hata kama ana makosa unayoyaona?
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mimi huwa mara nyingi nachukia generalization za aina hii. Hivi ni nini alichofanya Kagame ambacho Kikwete asingeweza kukifanya kutokana na hiyo story? Tuwe waungwana ndugu zangu, tunapoamua kutoa lugha ya fedhuli ni vema tukajenga hoja makini ya kutetea sababu zetu za kutoa lugha ya aina hiyo. Kama Kikwete hawezi uongozi, watanzania tunayo nafasi ya kumwondoa madarakani mwezi October. Hakuna sababu ya kuanza kumuandika vibaya namna hii. Bado ni mkuu wa nchi huyu, ni vizuri tuheshimu position yake hata kama ana mapungufu. Kutoonekana majina yetu kusitupe ticketi ya kusema tu hovyo.
   
 7. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yap! ni kweli, lugha ya kingereza kwangu mimi ni n ngumu, its more of a second language for me, si kama nyie wenzangu ambao ni mother tongue!.

  Well, kuhusu kagame kuthibiti majenerali, haina uhakika kama ni kupiga vita ufisadi, hapo utakuwa umetoa mtazamo wa juu juu mno...hao majenerali wote wanaokimbia na kutafuta asylum souz, walikuwa pamoja nao msituni muda wote, wanajuana kiundani sana na wanamabifu yao ya ndani kwa ndani ambayo wengi hatujui...na wengi wanakimbia nchi kwa kumuogopa yeye si lazima wawe wameiba pesa, ila wanaogopa kifo kwasababu wao ndio wanazijua siri za kagame kiundani sana ndio maana wanakuwa na kiburi kwake.

  yule aliyekuwa balozi wa rwanda nchini india, alitoa allegation nyingi ambazo ukiangalia kiundani utakuta ni legitimate kwa kiasi fulani kumfanya kagame naye achunguzwe...unajua raha ya udictator, ni kupiga mkwara watu wafanye chochote utakacho, ukipiga marufuku kumkashifu rais, ukiwaweka watu kwenye situation ya kukuinua hata kama haujafanya kitu, funga midomo vyombo vya habari etc...kama alivyofanya nyerere hapa kwetu, na ndivyo kagame anavyofanya..hivyo sifa nyingiii ambazo kagame anapata duniani, wengi wameshuhudia kuwa ni siasa za mdomoni tu.

  pia, siafiki wewe kuwaita watu hapa kwa kuwataja majina kama ni wahaini na mafisadi, kesi zingine ziko mahakamani, na hakuna hata mmoja wao ambao mahakama imetoa judgement kuwa ni fisadi au haini kama unavyosema, hivyo si vyema kumtukana mtu kihivyo, labda ungesema "wale ambao wanashutumiwa kuwa wahaini au mafisadi"etc...hata hivyo, hii thread naona umeileta kwa ushabiki fulani ambao si wa ki utu uzima...hivyo hata mlengwa uliyekuwa unampa message, anaweza asiipate vizuri kwasababu ataidharau mwanzoni kutokana na approach yako..sijafurahia uliposema kikwete ziiiiiiiiiiiii....hakuna kitu cha maana sana ambacho kagame kafanya kumfanya kikwete awe ziiii kabisa..

  however, sishabikii mafisadi, na msimamo wangu mimi ni mzuri tu kuhusu hili, ya kuwa Mheshimiwa Rais wetu hajapiga vita mafisadi kwa kuridhisha kama ilivyokuwa inatakiwa....watu wengi ilibidi wachunguzwe na sheria ichukue mkondo wake...kuanzia wale wa epa, richmond etc..na wanasheria wetu siwaelewi kwanini muda wote huwa wanakosea kwenye kudraft charge sheet inayofanya watu kama kina mzee wa twin towers...na zombe etc kutoka kiulaini kwasababu makosa yaliyoko kwenye charge sheet yanakuwa magumu kumkamata mwizi....huo ndo mtazamo wangu.
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Kwani Kikwete raisi???? mfananishe Kagame na Maraisi bwana!!!
   
 9. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ziiiii! No it's too much for him! even if !

  Mix with yours
   
 10. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete sio rais? kumbe ni nani? acheni kashfa jamani hata kama ......

  Mix with yours
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  This is too much. Yaani tumefikia kushabikia kiongozi wa dola lingine na kumdhihaki rais wetu. Kama raia una haki ya kuwa critic kwa viongozi wako lakini hiyo haina maana as irresponsibly as this. Yaani hata story umeshindwa kuilewa. Ni wazi huyu hakukamatwa kwa kutoomba ruhusa ambayo ukweli walimkatalia kwani Kagame hivi sasa anaogopa kila mwanajeshi mwenzake. Wakati ninavutiwa na uongozi imara wa Kagame lakini ni wazi huyu jamaa taratibu ana evolve kutoka kuwa benevolent dictator to just another Africa's sad story.

  Ndugu zangu tuwe makini, kinachoendelea Rwanda ni zaidi ya "utawala imara". Very soon tutaanza pokea wakimbizi upya. Kagame is losing and he is losing fast.....
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jun 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nadhani hukutafakari habari hiyo sawasawa. Huyu jamaa kakamatwa siyo kwa sababu alikwenda kwenye mashindano ya WC nje ya nchi, alikamatwa kwa vile ni mwanajeshi na Kagame ana wasiwasi kuwa huneda anakwenda kukutana kisirisisri na wale wanajeshi wengine waliokorofishana na Kagame wakakimbilia South Africa.
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sasa tayari ameshapata adui mwingine tena, uyo General tayari ameshakuwa kundi moja na wale waliokimbia..jamani, hivi kuna nini huko Rwanda, pamoja na kwamba kagame ana mapungufu mengi, lakini at least wanakaa kwa amani, washukuru Mungu hata iyo amani chini iliyoko chini ya kagame (hata kama insufficient), wanaenjoy kuliko vita na ukimbizi kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma...hawa naona wananusa mapinduzi hawa na kagame asipokaa vizuri wanaweza kumpindua, na akipinduka tu, ile kesi yake wafaransa waliyokuwa wanamnyemelea itaibuka upya na atakuwa nyuma ya nondo si muda..nakwambia watamkamata kagame akitoka tu madarakani...Rwanda bado inaishi kwa visa sana, wahutu ambao ni 85% bado hawana upendo na watusi ambao ni wachache, na wamejaa kwenye selikali na jeshini kama ilivyokuwa kipindi cha wabelgiji...jeshi limejaa watusi, selikalini wamejaa watusi..wahutu ambao ni majority hawana hata hamu...

  magereza yamejaa maelfu ya watu ambao kesi zao haziishi, wengine wamesingiziwa tu kwasababu ni wahutu...wamewekwa ndani..ile roho ya kisirani na kisasi kutokana na kuchinja watusi bado ipo, na ndio maana Rwanda inaongoza kwa kuwa na jela hatari kuliko zote duniani bila shaka...kesi tu za mauaji ya halaiki inasemekana kama wakiamua kumshitaki kila mtu, zitaisha si chini ya miaka mia...labda apeleke mahakamani wahutu wote, ambao ni more then 80%...hatakuja kuwapa wahutu wengi waingie madarakani na jeshini, kwasababu watampindua muda huohuo..wahutu waliwaua watusi sana, na mpaka leo imewaumiza sana moyo, na kuwa nyima sauti ndo maana hawana sauti sana kwasababu wameshaonekana wabaya na hawataki kuendelea kuonekana wabaya duniani...pressure tu waliyoipata toka kwa kagame tangu ateke kigali, ni jehanum ndogo na wamefumbwa mdomo, ndo maana hata wanaogombana ni watusi kwa watusi...ambao population yao ni ndogo...akiweka wahutu wengi jeshini na selikalini wanampindua...na wahutu wengi ndo walikuwa wakimbizi watusi wakilindwa na RPF ya watusi...na hawataki kabisa icho kitu kitokee bora watawaliwe kidictator kuliko kurudia...hata kama walikuwa wauaji lakini wamejifunza kutokana na makosa...wamepata cha moto..na bado ni wanadamu wenzetu...ndo maana ajabu wanaogombana ni watusi kwa watusi..ajabu..

  sisi Tanzania tunafanya nini ili kuwanusuru hawa watu, kwasababu wakianza ukimbizi wenye mzigo ni sisi, watakimbilia kwetu...na ile kusikika kwa vita watalii wanapungua kwetu...what is tz doing to prevent another atrocity from happening in Rwanda?
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nafikiri ukweli uko katikati.

  Hata Putin walimlaani sana ila kwa Urusi, sasa hivi wamepanda juu sana kutokana na ubavu wake.

  Rais anatakiwa kuwa Rais jamani na si mshikaji. Huu upuuzi wanaomfanyia Rais wetu na yeye anawachekea, mhhh.

  Sasa weee gari la Rais lina ng'oka tairi, yeye anafurahi tu. Wakambeba akafungue daraja la kwenda Msumbiji, na kumbe daraja hata halijaisha. Wamemdanganya kwenye mradi wa Maralia, wamemdanganya kwenye ....... na hatujasikia mtu kakosa kazi. Sasa unafikiri hata wananchi wataanza kukupa heshima?

  Acheni kumdanganya Kikwete jamani na inabidi afahamu kuwa yeye ni Rais. Ana uwezo wote na siyo akina Lowassa/Rostam wamuamulie maswala ya nchi. Kesho mambo yakienda vibaya, ni yeye atapanda kizimbani na siyo hao akina Lowassa.

  Kagame, na mapungufu yake yote, yuko imara sana katika kuibadilisha nchi. Kama ni kuchagua Rais yupi awe Tanzania basi ntachagua Kagame. Kwani Kikwete wapinzani wake aliwafanya nini? Au tu kwa sababu hakuwakamata na kuwauwa? Kisiasa aliwamaliza kabisa na wengi wao sasa ni MAREHEMU katika siasa. Kama mtu haamini, basi kamuulize Sallim A Sallim au Malecela. Sallim hata hamu hana tena, kajichokea na kujificha kwenye mgongo wa Nyerere Foundation.
   
 15. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  mkuu hapa umenena,nikiongea mimi wananiambia namimi muhutu,kwa hali ilivyo rwanda,tutegemee lolote mda wowote,haki za binadamu zinakiukwa waziwazi,nasasa kagame amemshikilia lawyer famous aliyesue ile arrest warrant ya kagame wakati kaenda marekani peter erlinder,kosa anasema ni genocide denial,google hilo jina ukasome vituko vinavyotokea huko na statement za goverment zilivyo kichekesho,mda si mrefu wamarekani watamchoka jamaa maana kiburi alichonacho sasa kinaenda mbali.
   
 16. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sawa omari huyu mleta mada hajui asemalo
  Mix with yours
   
 17. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Heshima utaipata kwa matendo yako na itaondoka kwa matendo yako pia. Hivyo irrespective of him being a prezidaa mambo hanayofanya hayaendani na nafasi aliyopo hivyo wananchi wana haki ya kutoa maoni yao hata kama ni mabaya vipi.
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Jun 23, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Sasa kumbe ilikuwa ni janja ya nyani tu? Mungu inusuru Afrika na watawala wanaotetea Maslahi yao tu bila kujali maisha ya watu wengine.
   
 19. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  SO a ticket to SA is the biggest corruption in Rwanda...lol. Kagame is silencing his opposition under the cover of 'fighting corruption' Ndio Rais mnae mtaka, mawazo yaki n'gombe n'gombe nahisi watu wengine ata elimu haiwasaidii? Kama anaipenda nchi yake sana mbona anafanya arbitrary arrests and detention! Huu ni upumbavu. Huyu mtu ni muuaji na malafi wa madaraka that is all. Tuombe uzima 2020 atakuwa bado Rais, hawa ndio watu waJInga wanao turudisha nyuma Africa. Shame shame shame on his blood stained face!
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi unaelewa sababu ya kukamatwa kwa huyo Genarali? (its just a smokescreeeeen!). Tafadhali fuatilia thread nyinge inayoendelea hapa JF kuhusu kupigwa risasi kwa Lt-Gen Nyamwasa kule Jozi ndio utaelewa kinachendelea huko Rwanda..
   
Loading...