Uchumi unaoongelea hapa ni wa enzi za adam smith enzi za mawe.Hiyo theory haina ukweli wowote.Nikupe mfano una nchi ambao pato la nchi ni milioni 100 na ina watu wawili tu wanaishi kwenye nchi hiyo.Na hao watu wawili mmoja pato lake kwa mwaka ni milioni 100.Huyo mwingine ni mlemavu na ombaomba asiye na pato lolote anaishi kwakula matunda pori na kuokota matakataka ya kula barabarani.Kutafuta pato la mtu kwa mwaka unachukua milioni hiyo 100 unagawa kwa wakazi hao wawili.Jibu utakalopata ni kuwa income per capita au pato la mtu mmoja kwa mwaka ni milioni 50!!! kWA Hiyo watu hao wawili wana maisha mazuri sana!!! Sio kweli mwenye maisha mazuri hapo ni mmoja tu.
Kwa hesabu hizo ulizotoa jibu ni hilo hilo wenye maisha mazuri sana kwa formula yako si wanyarwanda wote. Wenye maisha mazuri sana wako kigali.Hao wengine wamejumlishwa tu vichwa ili formula ya uchumi koko itoe jibu koko lisiloonyesha maisha halisi ya watu.Katika formula kichaa za uchumi koko ni hii uliyoitumia.