Kagame ni Shujaa

MAHORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
7,585
Reaction score
2,571
Wakuu, Nimefatilia Mkutano wa viongozi wa Afrika na Obama huko Marekani.

Kagame kampa za uso Obama na kumwambia aachane na hotuba za miaka nenda miaka rudi.

Kwakweli huyu Raisi ameonyesha kwamba yeye siyo legelege kama naniihii.
 
Tumuombe awe rais wa tz. Yy amewahi kusema bandariya dar pekee inatosha kupaisha uchumi wa tz.
Kwenye miti hakuna wajenzi
 
nikishapata hotuba nzima ya alichokuwa anazungumzia na muktadha ulikuwa ni nini nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusema chochote ngoja nitafute
 
nchi yake ni kama mkoa mmoja hapa nchini

Hii kauli siipendi maana imeficha uvivu nyuma yake.
Kuwa mkoa mmoja kumbuka ni.hasara kwan rasilimali mali zitakuwa ndogo hivyo kuweza kuzitumia sawa sawa na kuleta maendeleo lazima tumpongeze.
Kwanini tusitumie kigezo hicho kuigawa nchi katika zone ama majimbo ili nasi tupate maendeleo kama wao?
 
yaani kumwambia obama aachane na hotuba na miaka nenda rudi ndo kimekufanya umuappreciate kiasi hiki au kuna kingine.
 
... Wakuu, Nimefatilia Mkutano Wa Viongozi Wa Afrika Na Obama Huko Marekani, Kagame Kamupa Za Uso Obama Na Kumwambia Aachane Na Hotuba Za Miaka Nenda Miaka Rudi........ .. Kwakweli Huyu Raisi Ameonyesha Kwamba Yeye Siyo Regerege Kama Nanihihi.!

nimeskia kwenye magazet ya leo,na kuna wakat aliwah kunukuliwa na BBC akiwananga viongoz wa kiafrika wanaopenda kwenda ulaya na amerika kupiga picha na viongoz wa huko badala ya kukaa na kujadil matatizo ya wananchi wao
 
nchi yake ni kama mkoa mmoja hapa nchini

zanzibar unaweza kuizuru kwa baskel,na ukipiga filimbi wabunge na wawakilishi wanaskia,
issue ya hapa ni determination,tunadanganywa na udogo wa Rwanda,na tunakubali,je mapato yao yakoje?na sisi yakoje?
 
nimeskia kwenye magazet ya leo,na kuna wakat aliwah kunukuliwa na BBC akiwananga viongoz wa kiafrika wanaopenda kwenda ulaya na amerika kupiga picha na viongoz wa huko badala ya kukaa na kujadil matatizo ya wananchi wao

Kwani yeye hajapiga tena kapiga yeye na binti yake na Obama na mkewe kwenye mkutano huo Marekani hakupigia hiyo picha rwanda.
 
Nchi yetu kubwa na rasilimali nyingi pia,unakuta mkoa mmoja unarasilimali zaidi ya tatu.Na zote ni valuable and marketable.
Tatizo letu kubwa ni luck of determination,transparence and accountability.
 
Tumuombe awe rais wa tz. Yy amewahi kusema bandariya dar pekee inatosha kupaisha uchumi wa tz.
Kwenye miti hakuna wajenzi

.... Mi Mwenyewe Ningependa Iwe Hivyo Mkuu, Jamaa Ni Mchapakazi Na Mzalendo Siyo Kama Hawa Wachumia Tumbo Wetu
 
yaani kumwambia obama aachane na hotuba na miaka nenda rudi ndo kimekufanya umuappreciate kiasi hiki au kuna kingine.

..! Huu Ni Mwendelezo Tu Kuonyesha Kwamba Huyu Ni Kiongoz Shupavu, Kuna Mengi Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…