VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,481
- 1,450
Katika Mkutano na Waandishi wa habari Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amekea wanaotegemea wachawi na kuhisi wao ndio wanaowapa ushindi badala ya kutegemea mafunzo na maandalizi mazuri kwenye soka.Aidha Rais Kagame aliwataka Wanamichezo na Mamlaka za Michezo kukuza vipaji katika michezo mbalimbali badala ya kutegemea uchawi.Rais Kagame amesema kuwa kilichomuweka pembeni na kuacha kwenda uwanjani kuangalia mpira, ni mambo machafu yakiwemo rushwa na uchawi.Nchini Rwanda kadiri miaka inavyosonga mbele, rushwa, ufisadi vinaendelea kuripotiwa na kuwa chanzo cha kudidimiza soka nchini humo.