Kagame asitusha msiba wa Mandela

Kagame asitusha msiba wa Mandela

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
5,648
Reaction score
1,729
Alitua ghafla na kwenda kumuaga Mandela
*Aondoka bila kumpa mkono wa pole Rais Zuma

KATIKA hali isiyotarajiwa, Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumatano iliyopita aliwashangaza wengi baada ya kufika ghafla jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuaga mwili Mzee Nelson Mandela na kuondoka mara moja.

Pamoja na kuwasili ghafla bila taarifa Pretoria, Kagame alikwenda moja kwa moja katika majengo ya Union Buildings na kwenda kuaga mwili huo kisha alielekea uwanja wa ndege na kuondoka.

Habari ambazo Rai Jumatano imethibitisha zinasema aliondoka saa chache baada ya kuuaga mwili wa shujaa Mandela na kuelekea Rwanda ambako alikwenda kuongoza Mkutano Mkuu wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF), ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.

Habari za ndani zimesema kuwa Kagame ambaye alikuwa na ulinzi mkali, aligoma kwenda kusalimiana na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Kuja ghafla kwa Kagame na Rais Omar al Bashir wa Sudan katika kumuaga Mandela kulizua maswali mengi, kwa vile Rwanda ilitangaza kuwa Rais Kagame hatahudhuria mazishi hayo na badala yake itatuma ujumbe wa viongozi wa juu wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Afrika Kusini awali ilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa Rwanda, Pierre Habumuremyi, Katibu Mkuu wa RPF Francois Ngarambe, ndio wangeongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazishi hayo.

Clyson Monyela, Naibu Mkurugenzi Mkuu na Msemaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mahusiano ameliambia Rai Jumatano jana kuwa Serikali awali ilipokea jina la Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa RPF, lakini baadaye waliambiwa kuwa Kagame amewasili mwenyewe na ujumbe wa watu wachache.

Monyela alisema walipokea orodha ya maraisi wengi wa Afrika wakiwamo kutoka Kenya, Uganda, Congo DRC na Burundi lakini hawakupokea jina la Kagame ingawa alitokea ghafla na wala hakwenda kumpa pole Zuma, ila alituma ujumbe kwa Rais Zuma na wananchi wa Afrika Kusini.

“Hatukupokea jina la Rais Kagame kwa vile Serikali ya Afrika Kusini haina tabia ya kumualika mtu kwenye msiba wala mazishi, hiyo ni tabia ya wananchi wa nchi hii,” alisema.

Msemaji huyo alisema kuwa hakuna hata Rais au kiongozi yoyote aliyealikwa katika msiba na mazishi hayo, na ilikua ni utashi wa kiongozi kuthibitisha kuwa atahudhuria.

Rais Kagame katika muda wa hivi karibu amekuwa na ugomvi wa chini chini na maraisi Zuma, Kikwete na Banda kutokana nchi hizo wanachama wa jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika (SADC) kupeleka askari wao nchini Congo kuwaondoa waasisi wa kikundi cha M23 wanaosaidiwa na nchi za Uganda na Rwanda.

Naibu Mkurugenzi huyo wa habari aliongeza kuwa Kagame alikwenda katika majengo ya Makao Makuu ya nchi hiyo na alisalimiana na Mchungaji Jesse Jackson wa Marekani.

“Siwezi kujua walizungumza nini lakini walikutana, wakakumbatiana na kuzungumza, ila kwenye misa ya kitaifa ya kumuombea Mandela pale katika viwanja vya FNB hakuhudhuria,” alisema Monyela.

Hata hivyo, taarifa ndani zilizoifikia Rai Jumatano zimedai kuwa mke wa Rais Kagame aligoma kuhudhuria mazishi hayo na kuaga mwili huo kutokana na kutoridhishwa na uhusiano wa nchi ya Rwanda na Afrika Kusini.

Taarifa za uchunguzi ambazo Rai Jumatano imezipata nchini Afrika Kusini zimedai kuwa kulikua na kutokuelewana katia ya Rais Kagame na familia yake kutokana na nia yake ya kuhudhuria mazishi hayo.

Hata hivyo Serikali ya Rwanda kama zilivyo nchini nyingine duniani zilishusha bendera yake nusu mlingoti kuomboleza kifo cha Mandela.

Mandela alifariki Alhamisi wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na viongozi wengi duniani akiwamo raisi wa Marekani Barack Obama walihudhuria ibada maalumu na kuaga mwili wake.

Hata hivyo Kagame aliandika barua kwa familia ya Mandela na ilikabidhiwa familia hiyo na balozi wa Rwanda nchini humo.

Wakati marehemu Mandela alipochaguliwa kuwa Raisi wa kwanza mwafrika nchini Afrika Kusini mwaka 1994, Rwanda ilikua katika machafuko ya mauaji ya wenye kwa wenye kati ya Wahutu na watusi.
 
Kagame anajulikana kama mbabe wa vita
 
huyo jamaa kwa visasi mwisho, ni kati ya marais watakao ondolewa madarakani kwa kuuwawa. ni mbabe mno!
 
Kagame anajulikana kama mbabe wa vita

Unawajua wababe wa vita, wababe wa vita ni wale walioko msituni kudai haki ya wananchi na si haki ya kundi flani kama alivofanya Kagame na anavoendelea kufanya kwa kukanyaga miguuni demokrasia. yule ni insurgency
 
Aende zake kama alishasena hatahudhuria ni kipi kilichompeleka tena? Kihere here tu na bado ataweka chuki na kisasi kwa dunia nzima
 
Naibu Mkurugenzi huyo wa habari aliongeza kuwa Kagame alikwenda katika majengo ya Makao Makuu ya nchi hiyo na alisalimiana na Mchungaji Jesse Jackson wa Marekani.

Marafiki wengi wa Kagame sasa hivi ni watu binafsi siyo maraisi.Hata akisafiri nje ya nchi anakutana na watu binafsi zaidi.Wageni maarufu wanaotembelea Rwanda si viongozi wa Nchi ni watu binafsi kama ma-cerebrities.Hatembelewi na maraisi.Raisi anayeweza mwita rafiki ni museveni na Rafiki wa mashaka Kenyatta.

Hii inaamaanisha kitu kimoja tu FAILED FOREIGN POLICY FOR RWANDA.Raisi asiye na marafiki maraisi ujue shida ipo mahali.
 
Alitua ghafla na kwenda kumuaga Mandela
*Aondoka bila kumpa mkono wa pole Rais Zuma

KATIKA hali isiyotarajiwa, Rais Paul Kagame wa Rwanda Jumatano iliyopita aliwashangaza wengi baada ya kufika ghafla jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuaga mwili Mzee Nelson Mandela na kuondoka mara moja.

Pamoja na kuwasili ghafla bila taarifa Pretoria, Kagame alikwenda moja kwa moja katika majengo ya Union Buildings na kwenda kuaga mwili huo kisha alielekea uwanja wa ndege na kuondoka.

Habari ambazo Rai Jumatano imethibitisha zinasema aliondoka saa chache baada ya kuuaga mwili wa shujaa Mandela na kuelekea Rwanda ambako alikwenda kuongoza Mkutano Mkuu wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF), ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.

Habari za ndani zimesema kuwa Kagame ambaye alikuwa na ulinzi mkali, aligoma kwenda kusalimiana na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Kuja ghafla kwa Kagame na Rais Omar al Bashir wa Sudan katika kumuaga Mandela kulizua maswali mengi, kwa vile Rwanda ilitangaza kuwa Rais Kagame hatahudhuria mazishi hayo na badala yake itatuma ujumbe wa viongozi wa juu wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Afrika Kusini awali ilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa Rwanda, Pierre Habumuremyi, Katibu Mkuu wa RPF Francois Ngarambe, ndio wangeongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazishi hayo.

Clyson Monyela, Naibu Mkurugenzi Mkuu na Msemaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mahusiano ameliambia Rai Jumatano jana kuwa Serikali awali ilipokea jina la Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa RPF, lakini baadaye waliambiwa kuwa Kagame amewasili mwenyewe na ujumbe wa watu wachache.

Monyela alisema walipokea orodha ya maraisi wengi wa Afrika wakiwamo kutoka Kenya, Uganda, Congo DRC na Burundi lakini hawakupokea jina la Kagame ingawa alitokea ghafla na wala hakwenda kumpa pole Zuma, ila alituma ujumbe kwa Rais Zuma na wananchi wa Afrika Kusini.

"Hatukupokea jina la Rais Kagame kwa vile Serikali ya Afrika Kusini haina tabia ya kumualika mtu kwenye msiba wala mazishi, hiyo ni tabia ya wananchi wa nchi hii," alisema.

Msemaji huyo alisema kuwa hakuna hata Rais au kiongozi yoyote aliyealikwa katika msiba na mazishi hayo, na ilikua ni utashi wa kiongozi kuthibitisha kuwa atahudhuria.

Rais Kagame katika muda wa hivi karibu amekuwa na ugomvi wa chini chini na maraisi Zuma, Kikwete na Banda kutokana nchi hizo wanachama wa jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika (SADC) kupeleka askari wao nchini Congo kuwaondoa waasisi wa kikundi cha M23 wanaosaidiwa na nchi za Uganda na Rwanda.

Naibu Mkurugenzi huyo wa habari aliongeza kuwa Kagame alikwenda katika majengo ya Makao Makuu ya nchi hiyo na alisalimiana na Mchungaji Jesse Jackson wa Marekani.

"Siwezi kujua walizungumza nini lakini walikutana, wakakumbatiana na kuzungumza, ila kwenye misa ya kitaifa ya kumuombea Mandela pale katika viwanja vya FNB hakuhudhuria," alisema Monyela.

Hata hivyo, taarifa ndani zilizoifikia Rai Jumatano zimedai kuwa mke wa Rais Kagame aligoma kuhudhuria mazishi hayo na kuaga mwili huo kutokana na kutoridhishwa na uhusiano wa nchi ya Rwanda na Afrika Kusini.

Taarifa za uchunguzi ambazo Rai Jumatano imezipata nchini Afrika Kusini zimedai kuwa kulikua na kutokuelewana katia ya Rais Kagame na familia yake kutokana na nia yake ya kuhudhuria mazishi hayo.

Hata hivyo Serikali ya Rwanda kama zilivyo nchini nyingine duniani zilishusha bendera yake nusu mlingoti kuomboleza kifo cha Mandela.

Mandela alifariki Alhamisi wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na viongozi wengi duniani akiwamo raisi wa Marekani Barack Obama walihudhuria ibada maalumu na kuaga mwili wake.

Hata hivyo Kagame aliandika barua kwa familia ya Mandela na ilikabidhiwa familia hiyo na balozi wa Rwanda nchini humo.

Wakati marehemu Mandela alipochaguliwa kuwa Raisi wa kwanza mwafrika nchini Afrika Kusini mwaka 1994, Rwanda ilikua katika machafuko ya mauaji ya wenye kwa wenye kati ya Wahutu na watusi.

sitaki nataka! wewe kagame ndiyo yako iwe ndiyo na hapana iwe hapana
 
Raisi anayeweza mwita rafiki ni museveni na Rafiki wa mashaka Kenyatta.

Hii inaamaanisha kitu kimoja tu FAILED FOREIGN POLICY FOR RWANDA.

KKK washauriane namna ya kuleta amani Sudan ya Juba,sio kutaka kuwatumia kiuchumi tuu
 
Hili jembe la Africa tuache chuki zisizokuwa na maana.
Personally nimetembelea nchi yake on official business mtu asikudanganye jamaa wameibadilisha sana nchi yao.Actually naweza kusema wanakimbia wakati tutembea na hawana natural resources zozote uki compare na zetu.

Jamaa ana vision kubwa, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Ana bifu na serikali ya SA imempa hifadhi ya kisiasa yule generali ambaye alitorekea huko na anajua ishu yote jinsi PK alivyoshiriki kumuua Juvenal Habyarimana 06th april 1994 akiwa pamoja na raisi wa burundi Cyprien Ntaryamira kwenye ndege,so anaogopa jamaa asije akampangia mission ya kumuua-ukiishi kwa mtutu utakufa kwa mtutu
 
Hili jembe la Africa tuache chuki zisizokuwa na maana.
Personally nimetembelea nchi yake on official business mtu asikudanganye jamaa wameibadilisha sana nchi yao.Actually naweza kusema wanakimbia wakati tutembea na hawana natural resources zozote uki compare na zetu.

Jamaa ana vision kubwa, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Umetembelea nchi ya Rwanda au umetembelea Kigali? umefika vijijini wewe? Taabu watu wengi wakitembelea kigali wanarudi na kusema wametembelea Rwanda na kuona ina maendeleo si kelele hizo watarudi na kutukana hadi nchi kuwa Tanzania bure Kabisa.Rwanda sio KIGALI pekee.
 
Marafiki wengi wa Kagame sasa hivi ni watu binafsi siyo maraisi.Hata akisafiri nje ya nchi anakutana na watu binafsi zaidi.Wageni maarufu wanaotembelea Rwanda si viongozi wa Nchi ni watu binafsi kama ma-cerebrities.Hatembelewi na maraisi.Raisi anayeweza mwita rafiki ni museveni na Rafiki wa mashaka Kenyatta.

Hii inaamaanisha kitu kimoja tu FAILED FOREIGN POLICY FOR RWANDA.Raisi asiye na marafiki maraisi ujue shida ipo mahali.

M7 naye sio rafiki tena maana amemshauri aongee na FDLR
 
Back
Top Bottom