Taswira
JF-Expert Member
- Sep 23, 2012
- 1,198
- 447
David Kafulila
TUSIMUHUKUMU ZITTO KWA UKIGOMA.
Napita kwenye mitandao naona inajengeka dhana ya kijinga kabisa kwamba mgogoro wa CHADEMA unaomuhusisha zitto unajadiliwa na baadhi ya watu kibaguzi na kwa dhana ya historia kwamba watu wa Kigoma wanapenda au ni waroho wa madaraka kwa kutoa mifano ya baadhi ya wanasiasa waliogombea kwenye vyama na kusababisha mvutano.
Mimi niseme tu kwamba Kigoma ni sehemu ya Tanzania na watu wake wana haki zote za kugombea Kama wengine. Nachokijua kuhusu Kigoma ni mkoa wenye kupenda kuhoji na wasiopenda kabisa kubuluzwa au kufugwa akili.
Ndio maana huu ndio mkoa pekee ambao ccm waliburuzwa vibaya..huu ni mkoa ambao ccm ni Chama cha upinzani kwani kina majimbo3 huku upinzani ukiwa na majimbo5.
Hakuna mkoa mwingine uliochapa ccm Kama Kigoma. Ni mfano wa kuigwa na mikoa mingine Kama tunataka mabadiliko kweli. Tusihukumu mkoa kwa kutoa watu wanaopenda kugombea eti ni uroho wa madaraka, no!
Mbona pale bungeni Kati ya vyama 5 upinzani vyenye wabunge vyama vitatu vinaongozwa na wenyeviti wenye asili ya mkoa mmoja wa Kilimanjaro ? Na hatusemi kwamba watu wa kilimanjaro ni waroho wa madaraka kwasababu kila mtu anajua alifikaje alipofika hivyo tusitake kujenga dhana ya watu Fulani hawastahili na watu Fulani wanastahili Bali tuangalie dhamira, upeo na uadilifu, basi. Na sifa hizo sio za kijiografia.