Kafulila: Tusimhukumu Zitto kwa uKigoma bali dhamira, upeo na uadilifu

Status
Not open for further replies.
Tatizo kubwa hapa ni kwamba kila mtu anatafuta nafasi kubwa kukinga njaa. Full stop.
 


David Kafulila


TUSIMUHUKUMU ZITTO KWA UKIGOMA.

Napita kwenye mitandao naona inajengeka dhana ya kijinga kabisa kwamba mgogoro wa CHADEMA unaomuhusisha zitto unajadiliwa na baadhi ya watu kibaguzi na kwa dhana ya historia kwamba watu wa Kigoma wanapenda au ni waroho wa madaraka kwa kutoa mifano ya baadhi ya wanasiasa waliogombea kwenye vyama na kusababisha mvutano.

Mimi niseme tu kwamba Kigoma ni sehemu ya Tanzania na watu wake wana haki zote za kugombea Kama wengine. Nachokijua kuhusu Kigoma ni mkoa wenye kupenda kuhoji na wasiopenda kabisa kubuluzwa au kufugwa akili.

Ndio maana huu ndio mkoa pekee ambao ccm waliburuzwa vibaya..huu ni mkoa ambao ccm ni Chama cha upinzani kwani kina majimbo3 huku upinzani ukiwa na majimbo5.

Hakuna mkoa mwingine uliochapa ccm Kama Kigoma. Ni mfano wa kuigwa na mikoa mingine Kama tunataka mabadiliko kweli. Tusihukumu mkoa kwa kutoa watu wanaopenda kugombea eti ni uroho wa madaraka, no!

Mbona pale bungeni Kati ya vyama 5 upinzani vyenye wabunge vyama vitatu vinaongozwa na wenyeviti wenye asili ya mkoa mmoja wa Kilimanjaro ? Na hatusemi kwamba watu wa kilimanjaro ni waroho wa madaraka kwasababu kila mtu anajua alifikaje alipofika hivyo tusitake kujenga dhana ya watu Fulani hawastahili na watu Fulani wanastahili Bali tuangalie dhamira, upeo na uadilifu, basi. Na sifa hizo sio za kijiografia.
nenda mikoa ya pemba uulize ccm imepata majimbo mangapi ndio uje useme kuwa kigoma ni namba ngapi.
 
Badala ya kumshauri ndugu yako alie na aombe radhi mbele ya kamati kama ulivyonyenyekea na kulia wewe kama mtoto mbele ya Mbatia,unamdanganya eti ana dhamira na uadilifu!Kama ni dhamira ya zzk basi ilikuwa Mbaya tangu mapema,kama ni uadilifu ni ziro huwezi kuwa kiongozi halafu --------- na wapinzani kuhujumu chama chako mwenyewe.Kweli watu wa Kigoma ni waroho wa madaraka na wana tabia ya uchawi ya bora tukose wote

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
pole kafulila ila kweli ww ni kafulila maana umesahau yaliyokukuta mpaka unalia kwa kulia machoz
 
Sukutegemea kama Kafulila nawe ni wa aina hii, hakuna mtu mwenye mawazo ya kijinga ila kila mtu ana haki ya kuwasilisha mawazo yake kwa uhuru, umetoa mfano wa wenyeviti wa chama watatu toka Kilimanjaro, je? Ni viongozi wa mkoa gani waliokuwa upinzani na kununuliwa na Ccm kwa kupewa vyeo Ccm na juusaliri upinzani kama sio Kigoma?? Huvyo na Zitto unaona anayofanya ni sawa??? Sijaona mantiki ya ukucho andika zaidi ya kukoroga watu! Kama unamuonwa huruma Zitto mchukueni Nccr, kwani hata wewe ni masalia
 
For this Zitto has nothing!
Instead
1.negative dhamira
2.negative uwezo
3.myopia upeo.
Tupa kule.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom