Kafulila: Nina bomu zito la Escrow

Kafulila: Nina bomu zito la Escrow

Hii ni lugha ya wabunge wala rushwa anatishia kwamba niletee mzigo wa hela nisitoe siri.Ndio maana kasema wazi Muhongo limalize ili nisimwage siri.Kusema hadharani ni kutishia kuwa usiponipa hela mimi na wewe.

Kafulila na Zitto ndio staili zao za kudai rushwa si kwamba wana uzalendo.Katika wabunge wala rushwa waliokubuhu ni Zitto na Kafulila.

Kama wangelitaka Rushwa muelewe hata zile report zilizoivuruga CCM zisingesomwa na tusingejua chochote.

Haya ni majembe na Wale Madaktari wa kung'oa meno bil ganzi wameshindwa!!!!

Kifo cha CCM kipo mlangoni kinapiga hodi.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kafulila na ukawa wamefanya sahihi kabisa ,walijua ccm watabadilika kama ilivyotokea sasa.prof.Muongo yuko kwenye ziara wakati alishatakiwa kuadhibiwa.Mkuu wa kaya alisema apewe siku mbili tatu,sasa zimepita wiki ngapi?
Ngoma bado mbichi hii muwabane bunge lijalo hadi walie kukomesha tabia ya wizi kwa viongozi waliopewa dhamana.
Hata haya hawana wakati waTz wanateseka
 
Nimesoma makini alafu nikakuta chanzo ni NIPASHE... teh teh Mengi mwaka huu atakufa na presha.. nahisi Mhongo alimgongea mama Wawili.
 
Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR-Mageuzi David Kafulila amesema kwamba analo bomu lingine kuhusu sakata la uchotwaji wa zaidi ya shilingi bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.Mbunge huyo anasema kuwa bomu hilo likilipuka litatikisa serikali na vigogo waliohusika katika kashfa hiyo akiwemo Waziri wa nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Nini maoni yako?

10917305_1121973744483709_4556993948070054362_n.jpg

==========================

Chanzo: Nipashe

Akamatwe na bomu lake, yaonekana kijana ni gaidi.
 
Hii ni lugha ya wabunge wala rushwa anatishia kwamba niletee mzigo wa hela nisitoe siri.Ndio maana kasema wazi Muhongo limalize ili nisimwage siri.Kusema hadharani ni kutishia kuwa usiponipa hela mimi na wewe.

Kafulila na Zitto ndio staili zao za kudai rushwa si kwamba wana uzalendo.Katika wabunge wala rushwa waliokubuhu ni Zitto na Kafulila.

akili ndogo km hii ndo inayoendelea kuiweka ccm madarakani
 
Hapana, Kafulila usidanganye watu, huo ushahidi unajua kabisa utagusa mpaka aliyesuluhisha ule mgogoro wako na bosi wa chama chako, na kumpooza bosi wako akapewa na ubunge wa kuteuliwa kama sehemu ya make bali another, ya kumpooza kwa kutokukutema. Sasa utaanzaje kumwaga huo ----- wako mdogo wangu?
Ni afadhali ungepiga kimya na hiyo santuri yako, kwasababu mpaka hapo significant tofauti yako na upuuzi , unafiki na ushenzi alioufanya Mwakyembe wakati wa sakata la RICHMOND/DOWANS.Hata akiondoka Muhongo sisi wananchi lazima tukudai utupe huo ushahidi. Vinginevyo na wewe ni mrushwa tu wa kawaida tu. TUTAKUDHARAU.
 
Nayeye kamweka kiporo mwongo,,ananinii huyuu kilamtu anamwogopa,,kaagakwao simchezo,,..
 
Kafulila hatishii, inawezekana kabisa ana ushahidi wa uHAKIka, if you stand for the truth you will always stand alone, simama Kafulila usiogope kusimamia Kweli maana Kweli itakuweka huru no way out mnaotuhumiwa sakata la Escrow achieni ngazi wenyewe hayo madaraka hamkuzaliwa nayo pengine hata hamtakufa nayo, HAKIka hamtaenda mavumbini na vyeo vyenu wakati Mchwa wa ardhini watakapokuwa marafiki zenu
 
Sikiliza wimbo wa Kenny Rogers - The Gambler. Ni lazima ujuwe ni kadi gani na kwa wakati gani uitowe. Na la muhimu zaidi ni kuwa unapocheza kamali, ni lazima ujuwe ni muda gadi wa kunyenyuka mezani na kukimbia kipigo cha kulizwa hela zako.

Sasa ndo nini hiki... Kama unao ushahidi dhidi ya mtu ni bora uutoe hadharani..
Kuzidi kuubana huo ushahidi ni sawa na kumuweka kiporo huyu mtuhumiwa!!
 
Last edited by a moderator:
Pana siku kuna Mchizi mmoja humu ndani JF alikuja na habari yake kuwa Zitto na Filikunjombe wana video ya wale wote waliobeba fedha za Escrow kutoka Stanbic Bank. Hiyo video ndiyo iliyompa nguvu ya Zitto kusema kuwa watu walibeba fedha kwenye Lumbesa, Rambo na mifuko ya sandarusi.

Inawezekana na yeye hii video anayo na Mafisadi wanajua kuwa wakiwa-Ulimboka hawa vijana au kuwa-Kolimba kama siyo kuwa-Kombe basi video itakaa Youtube siku hiyohiyo.

All in all, wameshikwa pabaya sana. Juu chuma na chini chuma, uende wapi?

Kafulila hatishii, inawezekana kabisa ana ushahidi wa uHAKIka, if you stand for the truth you will always stand alone, simama Kafulila usiogope kusimamia Kweli maana Kweli itakuweka huru no way out mnaotuhumiwa sakata la Escrow achieni ngazi wenyewe hayo madaraka hamkuzaliwa nayo pengine hata hamtakufa nayo, HAKIka hamtaenda mavumbini na vyeo vyenu wakati Mchwa wa ardhini watakapokuwa marafiki zenu
 
Sasa ndo nini hiki... Kama unao ushahidi dhidi ya mtu ni bora uutoe hadharani..
Kuzidi kuubana huo ushahidi ni sawa na kumuweka kiporo huyu mtuhumiwa!!

Maneno hayo yalimponyoka tu baada ya #vigeregere & #makofi ya akina #tununu_fijo kule kwetu!

Ni mbuli tu na kuhemewa ndiko kulimfanya akapagawa mithili ya aliyepandwa na Pepo.

Tumsamehe. Amen!
 
Kuna watu umewakera Kafulila.
Baadhi wanaisahihisha hiyo kauri yako.
Wengine wanaidharau.
Wengine wanaipuuza.
Wengine wanaichukia.
Lakini hujawakera bure ,,,umewatonesha kidonda walichodhani kinataka kukauka.

Ushauri: endelea kuwatonesha tu wakome, wamewaumiza mamilioni ya watanzania kwa ubinafsi wao... endelea tu ,, chokonoa , wachokonoe penye kidonda si wamesha kula!
 
Hawezi kuweka hadharani hizo nyaraka,
1: Hana uhakikaka kamili na yaliyomo?
2: kazipata kwa njia za panya (unofficial ways)

Kwa hivyo anahitaji kinga za Bunge aweze kazitoa, wabunge wana kingwa sana na sheria za bunge ndio maana utaona wanauwezo wa kasema lolote bungeni.

Tumsubiri
 
Nimesoma makini alafu nikakuta chanzo ni NIPASHE... teh teh Mengi mwaka huu atakufa na presha.. nahisi Mhongo alimgongea mama Wawili.

HUjasoma vizuri KWA MAKINI bado au kama umesoma huenda una tatizo la kuto kuelewa.

Haya maneno hajasema Mengi bali amesema Kafulila.

Nenda kamuulize Kafulila ili upate uhakika kama ni maneno yake au ya Mengi.

usiongee mambo ya vijiwe vya kahawa na Kashata hapa.

Weka ushahidi tukuelewe.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hawezi kuweka hadharani hizo nyaraka,
1: Hana uhakikaka kamili na yaliyomo?
2: kazipata kwa njia za panya (unofficial ways)

Kwa hivyo anahitaji kinga za Bunge aweze kazitoa, wabunge wana kingwa sana na sheria za bunge ndio maana utaona wanauwezo wa kasema lolote bungeni.

Tumsubiri

Usiwe na papara hata yale mambo ya ESCROW pia alikuwa hakuweka hadharani lakini alisema vyombo halali vya uchunguzi wakihitaji msaada wake atawapatia.

Yule siyo mtu wa kukurupuka kama mnavyofikiria. Ni msomi yule mwenye kuelewa anachosema.

Mwanzo mlimuita TUMBILI, sasa TUMBILI ni nani kati ya Kafulila na wale waliomuita hivyo?????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hapana, Kafulila usidanganye watu, huo ushahidi unajua kabisa utagusa mpaka aliyesuluhisha ule mgogoro wako na bosi wa chama chako, na kumpooza bosi wako akapewa na ubunge wa kuteuliwa kama sehemu ya make bali another, ya kumpooza kwa kutokukutema. Sasa utaanzaje kumwaga huo ----- wako mdogo wangu?
Ni afadhali ungepiga kimya na hiyo santuri yako, kwasababu mpaka hapo significant tofauti yako na upuuzi , unafiki na ushenzi alioufanya Mwakyembe wakati wa sakata la RICHMOND/DOWANS.Hata akiondoka Muhongo sisi wananchi lazima tukudai utupe huo ushahidi. Vinginevyo na wewe ni mrushwa tu wa kawaida tu. TUTAKUDHARAU.

/./././././././. LOADING././././././././.

Result:

No sense
 
Sikiliza wimbo wa Kenny Rogers - The Gambler. Ni lazima ujuwe ni kadi gani na kwa wakati gani uitowe. Na la muhimu zaidi ni kuwa unapocheza kamali, ni lazima ujuwe ni muda gadi wa kunyenyuka mezani na kukimbia kipigo cha kulizwa hela zako.

UNGEWEKA SIKINDE au MSONDO NGOMA twengekuelewa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom